Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Ukiidaka tuu...inalipuka na hunter yko unapoteza mara 2
Si wanasema zililetwa mwanzo
Wakati mwingine tuwe makini na baadhi ya habari hizi za kuchongwa na CNN akishirikiana na waandishi wa habari wa Ukraine yenyewe, kama ingekuwa ni kweli Jeshi la Ukraine linafanya vizuri kwenye vita hii iweje yena leo Jenerali wa jeshi la Kimerikani anaye heshimika sana ana jitokeza adhalani na kukiri kwamba Kiev may fall in 72 hours,repeat fall in 72hours hiyo ni kauli ya Generali sio yangu.

Inakuwaje sasa sisi watu baki ndio tujifanye we know better masuala ya vita kuliko Majenerali wa VITA!!

Propaganda nyingine zinashangaza sana - na wapo baadhi ya wana JF wanao support adithi hizi za kutunga utasikia kwamba "eti Putin anafanya ziara nchini mwake akiambatana na watu watatu wanao mfanana - hivi mwanajeshi mwenye cheo cha Ukanali kama Putin umuogope nani mpaka kifikia hatua na kuwa na his double au triple etc. Adithi za magharibi hasa za tabloid ni burudani tosha.
 
Crypto iko vizuri tuu mkuu..inatumika zaid individualy na kwa baadhi ya makampuni makubwa, Nchi km North korea ndio njia yake kuu ya international transaction, wana expert wazuri kwenye tech ya crypto maana ndio moja ya loophole survivng yao ilipo..
 
Mkuu unauliza maswali ya ajabu kidogo. "LGBT society" - sidhani kitu kama hiki kianwezakana. Kila jamii inategemea kuzaa na kulea watoto - na watu hao hawazai. Ninavyojua wako kote duniani kama asilimia ndogo ya watu watu, labda %% 2-3? Ninawaona kama hao wote walio tofauti na "wastani" au "kawaida" - watoto wanazaliwa zeruzeru, vipofu, wenye vipaji vya pekee au wale wanaokosa uwezo fulani . Wako huntha wanaozaliwa na dalili ya jinsia zote mwilini, na wengine wanaojisikia kuwa na jinsia tofauti tangu utotoni.
Naona changamoto ya kila jamii kukubali na kuwapa nafasi watu wote wasio na tabia ya kuudhi wengine hata kama "si kawaida". Kwa macho ya dini nawaona wote kama sehemu ya uumbaji wa Mungu.
Ukiangalia historia ya binadamu, jamii tofauti zilikuwa na njia tofauti kushughulika changamoto hiyo. Kuna jamii ambako watu walifundishwa kuhofia walio tofauti na hata kuwaua (mfano kuua mapacha, au watoto walemavu), kuna jamii zilizokuwa tayari kuishi nao na kuwapa nafasi fulani. Mbinu hizo tofauti utaona kote duniani, kama ni Afrika au Asia au Ulaya au wapi.
Siamini ni kweli kwamba hao washoga hawakuwepo Afrika, walikuwepo na wako kama kila sehemu ya dunia.
Hasa katika majadiliano yetu kuhusu vita ya Ukraine sioni itasaidia kitu chochote kuingia katika kelele kuhusu "mashoga" au "nchi za lgbt".
Niliuliza wachache hapa wana sababu gani kuita viongozi au wanasiasa fulani kwa jina hilo - sijaona jibu (ila matusi hapa na pale...)
 
Aione kipanya hii
Au muandikie kwa kiswahili🤣🤣
 
Kuna watu bado hawaelew maana ya hii SMO .......hii ni ku demilitarize ukrine plus ku buy time ili kuleta economic hardship Kwa EU

Ukibisha jibu swali hili

Kama hypersonic missile za Russia haziwezi kuwa intercepted.......kwanini asivunje ikulu ya zelensky na hizo missiles....ili kumfuta kabisa .......
.the answer is Russia anapigana friendly ili ku buy time[emoji1179][emoji1179][emoji1179][emoji1179][emoji1179]

Nukuu
Xi jinping: we're the one driving these changes
Putin: I agree

Je ni changes Gani hizo
 
Mkuu umeamua kumsifu jenerali Mark Milley kwa sababu unapenda nukuu "Kyiv might fall in 72 hours"???? Samahani lakini unachekesha kidogo. Alichosema ilikuwa maoni yake kabla ya uvamizi wa Urusi. Sia sababu wala utaalamu wa kumpinga - nadhani kama Warusi wasingefanya makosa yale mapunbavu waliyofanya labda wangeweza!
Ila jenerali Milley anaendelea kuongoza jeshi la marekani hadi leo. Ukitaka kujua jinsi alivyoona mwendo wa vita, usiridhike na nusu setensi aliyosema kwenye Februari 2022.
Ungeweza kuangalia interview yake ya juzi hapa

Hapo anasema Urusi imeshadhindwa kutimiza malengo yake. Anataja sababu kama vile Urusi ilishindwa kutawala anga juu ya Ukraine, halafu mtindo wa uongozi upande wa Urusi ni bado ya zamani (amri kutoka juu) ilhali Ukraine imekabidhi maazimio mengi kwa makomanda uwanjani.
Sipendi kumsifu jenerali wa US lakini ukimpenda, basi sikilita anachosema.
 
Mkuu unapata wapi picha kwamba "Russia anapigana friendly"????
Uharibifu kwenye nyumba za watu raia na mauaji kwenye miji ni "friendly"??

 
Ndio tunajiuliza hayo majeshi yatavamia ardhi ya US ili kuleta Vita ?..Na kama ni hivyo, je yatavuka bahari au yatapitia mipaka ya Mexico na Canada ili kuifikia ardhi ya US ?
Kuna manyambizi ya kutosha, manowari za kitosha, kuna ma-icbm mkorea kaskaz ana mdude unatembea umbali wa kilomta 15k wakat kutoka US had kwke ni kilomita 11.5k uchina hvohvo mzigo wake unatembea kilomt 12k na kutoka us had uchina ni kilomita 11.6k sasa urusi si mdomo na pua kbs...visiwa vyake vinakaribiana na alaska kbs ht kilomita 100 nying..unahis Uk na visiwa vyake atasubutu atawazuia hao jamaa na icbm zao? Zikija usawa wa anga lako hata uzipasulie huko juu hyo uranium itakutesa japan cha mtoto
Sanasana Canada ndio atatoa msaada..japan hasubut ata kurusha bom la mkono...maana katopedo kamoja tuu kanainua bahar inaifunika japan kwa masaa mawili..maji yakiisha tunakuta samaki tuu wanakula watu..kama samaki watakuepo hai lkn..south korea ndio atataman ajigeuze jiwe la baharini asizamishwe..maana ni kakipisi ka muundo wa kigamboni hivi..huku na huku maji...australia nae hana jambo, kwanza anataka ajitoe chini ya ukoloni wa UK, wanaimba kila leo King Charles sio mfalme wao...why wanaish chin ya sheria za Uk?..
Mbinyo wa US unambana kwelkwel..na US alivyo mpiga dili anataka amuuzie Australia manyambizi 5, huku operation ni kulinda base za jeshi la AUKUS...US anawafanya wazungu waonekane wajinga kukithiri
 
Mkuu unapata wapi picha kwamba "Russia anapigana friendly"????
Uharibifu kwenye nyumba za watu raia na mauaji kwenye miji ni "friendly"??
Mkuu basi tufanye Urusi haimwezi Ukrain....ndio maana hashindi vita..unakisia nini km Urusi itashinda hii SMO kwa haraka?
West hawatagharamika kama sasa..
West wataamua kumwongezea chokochoko russia
West wataamua kuhamishia nguvu uchina, na uchina ataumia kwa vikwazo na uchumi utadorora asia nzima..
India atahadaika na gilba za US kumuandama mchina kwenye swala la mipaka yao ambayo haijakaa vizur..
Baada ya hapo hii SMO itakua kazi bure..isiyo ya mafanikio..na west watakua wameshinda na kuweka mizizi mikuu asia..
 
Mkuu naona hatari ya Urusi kuporomoka. Kwa sasa si rahisi kuona jinsi watakavyomaliza. Putin aliongeza ugumu wa kupatana na Ukraine kwa kutangaza mikoa hii ya Ukraine kuwa sehemu za Urusi. Ukraine haitakubali kamwe (isipokuwa jeshi la Putin linafaulu kuteka Kyiv) na Putin hawezi kurudi nyuma. Zele ametangaza baada ya mauaji ya Bucha (kabla alikuwa tayari kupatana) anapaswa kupata kila kitu pamoja na Donbas na Krim.
Kwa hiyo ama Urusi anafaulu kushinda kabisa (ambayo sioni) au Urusi inapigwa hadi inapaswa kukubali aondoke.
na hapa naona hatari ya kuporomoka kwa Urusi (Medvedyev mwenyewe alisema vile). Hii ingekuwa hali ya hatari kwa Asia ya Kati.
Au wataendelea kuchinjana hadi kuchoka kabisa pande zote?
 
Unawaza ujinga wenzako toka smo inaanza walisema urusi inaanguka kiuchuni mpaka leo urus inapanda kiuchuni

Russia sio zimbabwe kwa hakika

Russia hakuna maandano
Ila ulaya yapo kila kona
Kisa au sababu ni uchumi tu kwenda yombo

Urus juzi katia kiberit drone ya super power
Mpaka saiv kimya

Na jana amepitisha drone zake eneo ambalo liko chini yake usa na ameambiwa alipue aone
Watu wanafanya trip daily na hakuna cha kumfanya

Russia sio zimbabwe
Akili zenu za kinyumbu pelekeno hukoo
 
Mkuu mbona unakopi propaganda ya kijinga kabisa na kutuletea??? Hii ni picha kutoka China, si Ukraine.
[emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635]
The head of the Joint Chiefs of Staff of the US Armed Forces, General Mark Milley, called Volodymyr Zelensky's goals, including the return of Crimea to Ukraine, "maximalist" and "extremely difficult" to achieve militarily.

Also today it became known that Kyiv refuses to negotiate peace even with its Western patrons, if they do not include Crimea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…