Msaada kwenye tuta. Leo tunaona mataifa mbalimbali yana mpa Ukraine ndege za Mig-29 azitumie kumpiga Urusi hivyo Russia anakabiliana na ndege alizozitengeneza mwenyewe, sio issue sana maana haziko complicated sana najua anaweza kudeal nazo bila shida kabisa.
Vita hii imetudhihirishia kwamba kumbe kuna situations zinaweza kupelekea wewe kupambana na siraha ulizoziunda we mwenyewe.
Tunaambiwa ndege ambazo ni stealth zinaonekana kwa kiwango kidogo sana au hazionekani kabisa kwenye radar hali inayopelekea kwamba endapo stealth plane imeingia anga zako unaweza kuiona ila kutengeneza ile kill chain ikashindikana
So kama US kasupply F-35 kwa mataifa kama Holland, Japan, Israel, Uingereza nk. Ikiwa US mbeleni huko akaingia vitani na moja kati ya hizi nchi au akavamia nchi fulani na hizi nchi zika donate F-35 kwa hii nchi ili ipambane na US, je US ataziangusha vp F-35 za adui?