Ka mji kadogo hako Supa-pawa anapigana kukatwaa toka mwaka jana, ataiweza kweli NATO huyu ?
Hivi nyie pro NATO na USA kweli mna uwezo wa kutambua mambo sawasawa?
Hivi kweli Kwa akili Yako unaweza kuupima upinzani wa kijeshi Kwa kuangalia ukubwa wa eneo?au kwa ubora wa silaha na askari?
Je unaichukuliaje nchi kama Israel kieneo na uwezo wake wa kijeshi kukabiliana na nchi kubwa kieneo za kiarabu kwa pamoja Tena zenye uchumi maradufu dhidi ya israel?
Je sio wewe na NATO ubwabwa wenzako ambao Kila siku mnashangilia misaada ya masilaha na masilaha anayopewa Ukraine,Tena mna neno lenu, package.
Tena wewe ndio kinara,mara Kila siku unafurahia ujio wa Patriot,mara Himmers,mara juveline,mara Abraham's, leopard na challengers.
Sasa huoni hapo Urusi ilikua inapigana na adui aliejificha ndani ya mji mdogo lkn aliepewa Kila silaha Bora kabisa kutoka nchi zaidi ya 31 zinazoogopeka kabisa hapa Duniani?
Tena na ushauri wa juu kabisa wa kijeshi na taarifa za kijasusi kutoka Kwa majasusi wabobevu wa NATO na Satellite zaidi ya 70 ziko angani zinampa maelekezo Ukraine?
Si wewe na NATO wenzako mnaofurahia Kila siku kile mnachokiita package ya vikwazo vipya?
Na je sio wewe unaefurahia Kila siku maandalizi ya counter offensive inayopangwa pentagon?
Sio wewe?
Je Urusi kuchukua mda mrefu kuwafukuza Ukraine pamoja na NATO walikua wamejichimbia Barkhmut huoni kama Urusi ni shujaa?
Je unaijua vizuri miundombinu ya Barkhmut?
Unajua Kuna mahandaki sawa na vijiji?
Je kwa Nini hutaki kukubali kua Urusi ameipiga Barkhmut kwa akili sana kuepuka hasara kubwa kwa upande wake?
Nyie pro NATO mbona mnajifanya hamayaoni haya.
Sasa nakuuliza na wewe ilikuaje kwa USA akisindikizwa na marafiki zake wa NATO na wasio wa NATO alikaa miaka 20 vitani Afghanistan akipambana na Kikundi Cha Watalaban na Al qaida amabao hawakua wanatumia silaha nyingine zaidi ya AK-47 peke yake,bila vifaru,ndege, satellite,meli,nyambizi wala gunship helkopta.
Wala wakiwa hawasaidiwi na nchi yoyote hapa duniani?
Sasa Leo hii Ukraine iliyofundishwa na NATO toka 2014 Hadi Leo mnaokota Hadi walemavu, Ukraine imepewa Kila aina ya silaha Bora kabisa kutoka NATO wote na wasio NATO.