Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


NATO wanalinda demokrasia ipi acheni kuwa wapumbavu hata kama mahaba yamezidi mnakua mapimbi. Kule Libya mliona NATO walichofanya, Iraq?. NATO ni kichaka cha US katika kufanikisha Agenda zake.
 
Kama ni kwa nchi washirika, walifuata nini afganistani, Libya, syria iraq, nk?
 
Muda sio mrefu Saud Arabic itakuwa Kama Libya. Ngoja wajidanganye na Majini yao
Hio haiwezi kutokea kwani Saudi wamenunua vifaa vipya na vya kisasa vya ulinzi na khasa ADSs kutoka kwa haohao US/ West.

Saudi Arabia wana miradi mikubwa kabisa ya Utalii yaitwa Red Sea Global RGS na IMAALA ambayo yanatarajia kuwa na hoteli zipatazo 48 kufikia 2030.

IMAALA ni kama vile Kigamboni yaani ni ukanda wa pwani utambaao hoteli za kitalii, vituo vya michezo na huu mradi utakuwa na hoteli zipatazo 25 na mwisho kuna kisiwa kitwacho Shura ambacho sasa hivi chajengwa hoteli 11 za kitalii na zote zitakuwa tayari mwaka 2027.

Mwisho hapohapo bahari nyekundu pana kiwanja cha ndege kipya Red Sea International Airport na visiwa mbalimbali katika bahari hiyo nyekundu vyote kuboreshwa.

Ndo maana Saudi akona aanze mapema kutafuta watalii na ni jambo la uzuri kuanza na majirani zake Iran na mshauri ni ... China maana yeye tayari ana wananchi wake wenye mahela tayari kwenda huko kama watalii.

Wenzetu wapiga hatua zaidi za maendeleo na sisi Tanzania twahangaika na ripoti za CAG, mara hadithi za asali na kadhalika.

Soma zaidi hapa kuhusu mradi wa Red Sea Global https://www.arabianbusiness.com/ind...as-red-sea-global-everything-you-need-to-know

Na hapa ni habari ya wachina kuwapatanisha wasaudi na Iran ili yeye aendeleze biashara zake na ajijenge zadi - Saudi Arabia, Iran focus on regional security, economy in first meeting since China-led breakthrough
 
Warusi wamekwisha bipatia mwarobaini, ni kweli kinacho ungua ni kilorry kinacho tumika ku-launch HIMARS rockets ambazo hata zenyewe siku hizi zinatunguliwa kama nzi na ADS za Urusi baada ya kusifanyia uchunguzi wa kina kwenye maabara ya kijeshi mjini Moscow kwa zile zilizo tekwa au kuuziwa na wanajeshi wa Ukraine.
 
Hizo silaha alizopewa mpaka sasa ni kwa ajili ya kujilinda tu ndio maana hajapewa silaha zenye uwezo wa kushambulia mpaka Urusi (Atacms) .......

wangekuwa na nia ya kuidhalilisha Urusi huenda hali ya Vita isingekuwa hivi ilivyo.
Kwa nini wasimpe hizo silaha!? Wanaogopa nini!? Njia pekee ya kuzuia Urusi asiishambulie Ukraine ni pale Ukraine atapokuwa na uwezo wa kujibu mashambulizi kwenye ardhi ya Urusi. Kwa nini hawampi huo uwezo!?
 
Wewe jamaa bana,unajaribu kupindisha ukweli lakini unashindwa.
Hebu ona hapa.umesema NATO iliundwa kwa ajili ya USSR.

Kwani ussr ilikua inazitishia amani nchi Gani?

Kwamba NATO ya Sasa baada ya ussr inatatua migogoro ya nchi wanachama.

Ni migogoro Gani hiyo ya nchi wanachama wa NATO?

Je migogoro hiyo imekuja baada ya kuvunjika ussr?

Kwamba NATO ya Sasa baada ya kuvunjika ussr inazilinda nchi wanachama dhidi ya vitisho vya Urusi.

Urusi ilikua inazitishia nchi Gani na kwa sababu Gani?.

Je Iraq,Syria,Libya,taleban,Yugoslavia na Sasa Ukraine ni sshemu ya NATO?

Aisee wewe jamaa propaganda unazipenda lkn kwa kweli huziwezi.
Sijakutukana lkn.
 
πŸ˜†πŸ˜† Panick not dogo πŸ˜†πŸ˜†. You know what? I am the age of your grandparents.

Kuniita bwana mdogo umenikoesa heshima sana. Rekebisha hapo tafadhali.
Puuuu! My mom is 68 unatarajia hao grandparents wako hai?

I know am young to you ila sio kivile bwana mdogo na huenda nikawa najua vingi kukushinda.
Watu wenye umri kama wewe mimi ni ma brother zangu na tumechapana ngumi sanaaa mitusi mingi sanaa.

Tuendelee na mada dogo
 
Ka mji kadogo hako Supa-pawa anapigana kukatwaa toka mwaka jana, ataiweza kweli NATO huyu ?
Hivi nyie pro NATO na USA kweli mna uwezo wa kutambua mambo sawasawa?

Hivi kweli Kwa akili Yako unaweza kuupima upinzani wa kijeshi Kwa kuangalia ukubwa wa eneo?au kwa ubora wa silaha na askari?
Je unaichukuliaje nchi kama Israel kieneo na uwezo wake wa kijeshi kukabiliana na nchi kubwa kieneo za kiarabu kwa pamoja Tena zenye uchumi maradufu dhidi ya israel?

Je sio wewe na NATO ubwabwa wenzako ambao Kila siku mnashangilia misaada ya masilaha na masilaha anayopewa Ukraine,Tena mna neno lenu, package.
Tena wewe ndio kinara,mara Kila siku unafurahia ujio wa Patriot,mara Himmers,mara juveline,mara Abraham's, leopard na challengers.
Sasa huoni hapo Urusi ilikua inapigana na adui aliejificha ndani ya mji mdogo lkn aliepewa Kila silaha Bora kabisa kutoka nchi zaidi ya 31 zinazoogopeka kabisa hapa Duniani?
Tena na ushauri wa juu kabisa wa kijeshi na taarifa za kijasusi kutoka Kwa majasusi wabobevu wa NATO na Satellite zaidi ya 70 ziko angani zinampa maelekezo Ukraine?
Si wewe na NATO wenzako mnaofurahia Kila siku kile mnachokiita package ya vikwazo vipya?

Na je sio wewe unaefurahia Kila siku maandalizi ya counter offensive inayopangwa pentagon?
Sio wewe?
Je Urusi kuchukua mda mrefu kuwafukuza Ukraine pamoja na NATO walikua wamejichimbia Barkhmut huoni kama Urusi ni shujaa?
Je unaijua vizuri miundombinu ya Barkhmut?
Unajua Kuna mahandaki sawa na vijiji?
Je kwa Nini hutaki kukubali kua Urusi ameipiga Barkhmut kwa akili sana kuepuka hasara kubwa kwa upande wake?
Nyie pro NATO mbona mnajifanya hamayaoni haya.

Sasa nakuuliza na wewe ilikuaje kwa USA akisindikizwa na marafiki zake wa NATO na wasio wa NATO alikaa miaka 20 vitani Afghanistan akipambana na Kikundi Cha Watalaban na Al qaida amabao hawakua wanatumia silaha nyingine zaidi ya AK-47 peke yake,bila vifaru,ndege, satellite,meli,nyambizi wala gunship helkopta.
Wala wakiwa hawasaidiwi na nchi yoyote hapa duniani?

Sasa Leo hii Ukraine iliyofundishwa na NATO toka 2014 Hadi Leo mnaokota Hadi walemavu, Ukraine imepewa Kila aina ya silaha Bora kabisa kutoka NATO wote na wasio NATO.
 
Misaada tu ndiyo kigezo cha kuwa NATO, mbona huonyeshi akili japo wewe mkubwa ?

Hata Tz huenda ipo NATO maana inapewa misaada sana na US, UK, France
Ila wewe jamaa unajitahidi sana kupindisha vitu lkn huwezi.
Stolnsberg katibu Mkuu wa NATO Kila siku anatoa matamko dhidi ya Urusi,je hua anatoa kumuwakilasha nani?
Ni kweli kabisa unavyosema kua Ukraine sio memba wa NATO sawa.
Lakini anapokea misaada kutoka nchi zote za NATO.na msemaji wa NATO huendelea kuhimiza nchi wanachama ziongeze misaada ya silaha.
Unajaribu kupindisha ukweli lkn huna ujanja huo.
Jana TU wewe mwenywe umefurahia Finland kujiunga na NATO.
Kwani NATO inauhusiano Gani na vita hii na kwa Nini Finland imeamua kujiunga na NATO Sasa hivi?
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ€πŸ€πŸ€πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…