Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 18,069
- 25,172
Mimi siyo mdogo wako kwa vile unaelekewa kujau mambo mengi ya kusimuliwa kuliko mimi ninayejua yaliyokuwa yanatokea moja kwa moja nikiwa ni kijana mwemye akili zangu. Nyie mnaosomasoma maoni ya watu mbalimbali ndio mnaohitaji kusaidiwa kuelewa ukweli. Yote unayoongea ni ya kuambiwa kwani unaelekea hujui kuwa wakati Msumbiji inapigana vita ya msituni, Zimbabwe pia ilikuwa inapigana, Nambia nayo ilikuwa inapigana na Angola nayo ilikuwa inapigana. Notion ya kuhamishia mapambano kutoka Msumbiji kwenda Zimbabwe ni ya kinadharia inayootokana na kusoma hadithi mbalimbali na haisemwi na mtu mwenye kuelewa mabo kikamilifu.Bado unazunguka tu mdogo wangu. Unagusia gusia tu vitu vichache.
Hapa Key point ni Putin kuwepo Tanzania.
Nimekueleza sababu zipo nyingi tu za Putin kuwepo Tanzania.
1. MPLA ilikuwa inasaidiwa na Tanzania pomoja na USSR
2. Baada ya kuikomboa Msumbiji mapambano yalihamia kuikomboa Zimbabwe. Na kuna kambi zilizokuwepo zikiendelea na Mafunzo moja wapo ni Bagamoyo na Kongwa.
Sasa wewe umeng'ang'ania mwaka mmoja tu wakati hapo imeandikwa Putin akiwepo Tanzania 1973 - 1977.
Nimekuuliza Kuanzia 1975 mpaka 1977 Putin alikuwa wapi? Umebaki kubwabwaja tu.
Usiende nje ya mada. Hapa tunamuongelea Putin. Issue za Mnangagwa kwenda china sidhani kama ipo kwenye context.
WEWE LETA PROOF KUWA PUTIN HAJAWAHI KUWEPO TANZANIA DURING STRANGLE.
Elewa kuwa uhuru wa Msumbiji na Angola ulisaharakishwa baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyowaondoa Americo Tomas na Marcel Caetano madarakani huko Ureno. Wanajeshi walichoka kupigana vita isiyo na mwisho hivyo wakawaoandoa vinara hao wa ukoloni na kuweka serikali iliyoanza kuachia makoloni.