Huyu jamaa atawachosha tu ndio maana binafsi huoni nikireply kwao bali kwenu.
Niandikie tena kwa herufi kubwa kua HAJUI CHOCHOTE, wala HAJUI HATA NINI ANAZUNGUMZA.
Nilisema mwanzo hawa kuna sayari yao wanaishi ina mambo yao ambayo obviously haya correlates na uhalisia uliopo ambao mie na wewe tunauona.
Katika watu wenye fikra mvuke basi ni hawa ndugu zetu. Huezi maliza paragraph mbili unasoma kinachomtoka kichwani mwake.
Duniani kuna aina mbili kuu za Makampuni, Private Companies and Public Companies. Private Companies haya hisa zake haziuzwi kwa Umma na kinyume chake ndio Public Companies. Katika hayo ndani yake kuna vijiaina vidogo dogo ambavyo hupatikana kulingana na sheria na mwongozo wa nchi husika. Lakin aina zote kwa wingi ama upana zina fall katika hizo category mbili. Public an Private Owned Companies.
Hata kama beneficiaries ni Government bado linaeza kua Private endapo hisa zake haziuzwi kwa Public au iwe Public Company kama hisa zake ziko free kuuzwa ama kununuliwa na kila mtu. Hii elim changa juu ya makampuni ambayo Mzee mmiliki haijui kabiiiiisa.
Wenzetu walivyo na ujinga mwingi utakuta wanashupaza kuisemea US af hawajui chochote kuhusu taifa hilo. Nimetoa mifano kwa ndugu
IFAC wakati nasema nae lakini bado kwa ndugu mtanzania hapo huenda jina kweli lina sadifu yaliyomo. Asili ya ile mambo utaivunja jioni asbuh mchwa wamefanya yao.
Kampuni kua Privately owned haina maana ya kujifanyia mambo yake nje ya taratibu zilizo ainishwa na State lilikopewa "residency".
Mfano Tanzania huezi kuta kampuni lina suffix ya Inc. LLC, AG, Corp. etc kwenye jina lake kwasababu sio ndani ya mwongozo wa sheria na taratibu zilizopo nchini. All companies registered in Tanzania zinabeba "LTD" ama "Limited" kwani ndio utaratibu wa nchi ulivyo hata kama unalimiliki huezi kwenda kinyume na hilo unless ufunge ukafungue sehem nyingine.
Kila sector iko under Taasisi ama Wakala wa serikali husika anayefanya kuratibu shughuli zake zifate mwongozo na matakwa ya serikali husika. Ndio ile tunasema kutii mamlaka na ipo kikatiba sio ombi alas. Kama alivyo Raia, tumesema hapo juu Company ikishakua registered inakia legal entity ambayo inapaswa kuendeshwa kwa kufata sheria na taratibu lengwa.
Ndio ile tunasikia kampuni, limeshitakiwa, kampuni limepigwa faini, hivi na vile kama kwani linatakiwa lifate taratibu na sio kujiamulia tu A Ba Cha Da. Tuna Banks hapa nchini, zipo PLC kama CRDB na Private Exim lakini zinafata mwongozo wa BoT na haziendi kinyume na hapo. Tuna kampuni za Sim lakini zinafata mwongozo wa TCRA, Ushawah sikia TIGO wanasema sie ni kampuni binafs hatufati maagizo ya Serikali?, Makampuni ya Madini chini ya wizara ya Madini n.k
Sasa kama mifano tu ambayo hata hapa hapa nchini ipo mtu hawezi ng'amua ya kuvuka Pacific anayujulia wapi?
Pale US upande wa biashara kuna DoC, I mean US Department of Commerce. Ambayo inashughulikia all businesses, Universities, Communities na National Workers. Amtafute Gina Raimondo Secretary wa hiyo department amuulize vizuri au atembelee website yao akajifunze
www.commerce.gov,
All companies registered ndani ya US, al maarufu "kampuni za kimarekani" zinasikiliza nini hao wehu wanataka. Wakisema No to flani kila company inafata na wakisema Yes to flani wanafata vile vile. Otherwise wafunge wakajiandikishe sehem nyingine!
Sasa atwambie wapi waliwahi toa Onyo af hizo kampuni zikabisha! Au pale inapotangazwa vikwazo vya uchumi kwamba marufuku kufanya biashara na kampuni za hapo US, hizo kampuni huwa ni za Serikali kwamba zingine ziko zina Immune na Amri hiyo?
Aisee hii dunia bn, Tumetoa hadi mfano wa HUAWEI na Google LLC, Kwani Google ilikua ni Kampuni ya Trump wajameeeeeeeneee 🤣🤣🤣 Jamaa alivyokaza shingo sasa wakati anachokizungumza wala hakijui.
Akiii, Bado tuna safari ndefu sana ya kupata Uhuru wetu ili tuweze kujikomboa.
Yah, I mean it for sure..... Uhuru wa Kifkra!