LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
wengi hamjui kwa nini russia anataka kumtwanga ukraine sababu ni yeye na msimamo wake wa kutaka kujiunga na nato na kwa sasa yeye ukraine ametamka anajifikiria upya kuamua kujiunga na nato ameona wanaomkingia kifua wamelegeza misimamo yao uingereza kaondoa vikosi vyake marekani anasema hapeleki jeshi kuokoa raia wa marekani endapo vita ikianza je ana maana gani hapo
 
Kutokana na yanayoendelea donbas,luhansck na donesck wanasiasa wa Ukraine wapo makini sana na maamuzi yao kwa sabab makosa kidogo tu hayo majimbo matat watayakosa jumla na nchi itavurugika.

Na ktk mapambano kuwa na silaha kali hakukupi dhamana ya kushinda pambano tumejionea kwa saudia na washirika wake dhidi ya wahouth.

Ingawaje unasema kuwa Ukraine wana silaha za nyuklia lkn sidhan km zinaweza wasaidia km hawapo vzr kiujasus,unapotaja nchi zinazotamba ktk ujasus huwez kutoitaja urus,us na nato licha ya ubabe wao lkn mara nyingi tu huwa wanalalamika kujasusiwa na urus sasa Ukraine unadhan amesalimika vp na ujasus wa urus ilhal juzi tu wamesema tovut yao ya usalama imedukuliwa kwa siku mbili mfululizo???
 
Mchokoza mada unaleta utani vita sio lelemama kiongozi wa Ukraine anastahili kutunukiwa shahada ya amani silaha za Nyuklia zkitumika hakuna mshindi.
 
Ukraine ilikuwa sehemu ya urusi hivyo wanaifahamu moscow kuliko wewe na kitu usichokijua ni kwamba kipindi cha soviet union Ussr ilijitahidi kusambaza silaha kila kona ya himaya yao hivyo ukraine anaifahamu vilivyo urusi kuliko hata NATO.

Hata hivyo vidude alivyo navyo ukraine ni less than 1/10 ya madude yaliyopo urusi maana kuna midude kama vile Bulava, Topol, bila kusahau Satan usikute na Lucifer sasa hayoote yatue Ukraine hivi unadhan hadi kuufyata ufaikiri hawajui kilivhopo Russia?
 
Eti na lucifa [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Unajua andiko lako linatoa picha gani kuhusu wewe?

1. Mwili wako umejaa makovu na ngeu kila mahala.
2. Huna rafiki anayekuamini ila tu watu wanakuwa na wewe kama kuna kitu wanahitaji kwako.
3. Unaweza kuwanyoa watoto wako vipara siku moja kabla ya harusi waliyondaliwa wasimamie.
4. Mkeo hajumuiki.
5. Hujawahi kuchaguliwa kuwa hata mjumbe wa kamati yoyote maishani mwako.
6. Kwenye mikutano ya jumla kazi yako ni kushambulia meza na wanakujua hivyo wanakuachaga kama ulivyo.
7. Una mahusiano ya mbali sana na hata majirani zako wakati huo huou huweze kuendana na hata ndugu zako wa damu.
8. Unatabia za kufuatilia na kukuza mambo na kwako kila jambo ni kubwa.
10. Uanjiona mpweke lakini ukwlei watu wanakukwepa kwa tabia zako za kupend ligi.
11. Unapenda kusutana kama genge la waimba taarabu.
12. Ni kama mtu umekua bila kupendwa na ukaachwa ujilinde na kujitegemea toka ukiwa umri mdogo, na bahati mbaya ukaishi kwenye mazingira ya visasi na kutokujali wengine.
13. Huamini katika amani na uvumilivu bali ni "Kama mbwai na iwe".
14. Huna sifa za uongozi.
15. Selfish.
16. Katili na hujali maisha ya kesho kwa yeyote.
17 Mihemuko kwa sana.
18. Kilakitu unafanya kwa kujihami na kuthibitisha.
19. Limitations kadhaa.
Pole sana ndugu.
Wingi wa watu, siyo nguvu wala uwezo.
Ngumi si suluhisho la kila changamoto.
Vita haina sura moja.
Hekima ni bora kuliko misuri.
Umeonyesha ni namna gani wewe si mtu sahihi wa kufanya maamuzi mikakati na ndiyo sababu hakuna mtu anayeweza kukuamini kukupa hiyo nafasi.
Mchana mwema.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤸🙆🙆🙆🙆
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wingi zi hoja ndugu mradi maarifa.
Zelewsky ametumia busara sana kukaa kimya. Anajua ataua watu wengi na madaraka watampora warusi.
Vita siku hizi hazitumii maguvu wala idadi. Technolojia ndugu ndo sana. Idadi kubwa na kuwa karibu na adui ni vikolombwezo tu.

Angalia Tsar bomba na Satan et na Lucifer [emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
 
Nikukosoe Kidogo.

Ukraine Hana hata Kombora moja la Nyuklia. Baada ya kusambaratika kwa USSR mwaka 1990,Ukraine ilijitenga rasmi na umoja wa Kisoviet na kuwa nchi huru mwaka 1991.

Wakati huo,Ukraine ilikuwa na Makombora ya Nyuklia 1,900 ambayo yalikuwa ni moja ya Siraha za Umoja wa Kisoviet. Ili kupata Uhuru wake kamili,Mkataba Kati ya USA na Russia ulifikiwa na makubaliano yalikuwa Kama ifuatavyo:

1.Ukraine akabidhi Siraha zote za Nyuklia na 90% ya ndege za Kivita na 85% ya Vifaru na 100% ya viwanda vya Kutengeneza Siraha kwa Urusi.

2. Urusi kutoivamia Ukraine na Ukraine kuwa nchi huru dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Mwaka 1991 mwezi June ndipo Ukraine akakabidhi Kila Kitu kwa Urusi. Hivi tunavyosema,Ukraine alikuwa Hana hata Ndege moja ya Kivita,Ndio imeanza kununua Siraha za Kivita za zamani za Urusi kutoka Latvia,Bulgaria baada ya Urusi kulinyakua Jimbo la CRIMEA.

Ingelikuwa unayoyasema kwamba Ukraine ina Makombora yake 1900 ya Nyuklia,nadhani Urusi asingelithubutu hata Kurusha Risasi huko Kievu kabisa. Walikuwa wajinga kukubali mikataba ya kwenye makaratasi huku wakikabidhi Siraha zao za Nyuklia kwa Urusi. Now Urusi anajimegea TU maeneo. Mwaka huu washukuru NATO wamejiingiza moja kwa moja kwenye huo mgogoro na hivyo Urusi imeona maji mengi na hasara kubwa endapo watavamia hata Kama wataiteka Ukraine.

North Korea kasaidiwa na Nyuklia mpaka USA kaogopa kumvamia kijeshi,laa sivyo North Korea kungelikuwa ni Moshi wa mabomu TU.

USHAURI.

Kosa kubwa atalokuja kulifanya Iran ni kuacha Mpango wake wa Nyuklia ili aondolewe vikwazo. Iran itabidi ikomae na vikwazo kwa Hali yoyote ile lakini wapate japo Mabomu 10 ya Nyuklia. Huo ndio utakuwa Usalama wa Irani. Si Israel Wala USA atakaye thubutu Kuvamia TAHRAN akijua Kuna NUKES.

Huu umebaki kuwa Ulimwengu wa wenye Nguvu TU. Kama wewe NI udhaifu utabaki kuwa kibaraka wa China,Russia au USA TU.
 

Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imetoweka mtandaoni, muda mfupi baada ya tangazo la kufukuzwa nchini kwa Naibu Balozi wa Marekani Bartle Gorman nchini Urusi. Tovuti hiyo ilionyesha barua ya taarifa ya kufukuzwa kwa balozi huyo.

Urusi ilimtaka mwanadiplomasia huyo anayeiwakilisha Marekani nchini Russia, kuondoka nchini humo bila kutoa sababu ya hatua hiyo ya kumfukuza.

Katika taarifa nyingine iliyothibitishwa na mtandao wa Netblocks imeonyesha kupotea kwa huduma za mifumo mingi ya kibenki na inayotoa huduma mtandaoni nchini Ukraine, kutokana na mashambulio ya (DDOS) kutoka kwenye chanzo ambacho hakijathibitishwa.

Matukio haya yanakuja huku kukiwa na mvutano mkali kati ya Ukraine na Urusi.

 
Hawa watu wakae mezan wajadiliane wayamalize. Wasije wakaanzisha Nuclear War. Dunia itasambaratika.
 
Hakuna aliyetayari kutumia nuclear
 
Baada ya kuangu Kwa umoja kisoviet walizirudisha Urussi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…