(wakati Uingereza imeshaacha mambo hayo na kurudi nyumbani. )
kwa kauli yako hiyo hapo juu .......[emoji115][emoji115]
swali ::: nimeskia jumuia ya madola ama kwa lugha ya huko( comonwearth )
jumuia ya madola ina husika na nini na mwanzilishi wake ni nani ...na hiyo jumuia kiongozi wake ni nani ?
umshana
maana unasema urusi wana ubeberu na hawa hapa chini
tuwaite kina nani [emoji116][emoji116] au tuwaite wana democracy .....
View attachment 2626717View attachment 2626719
Mkuu hao wa Jumuiya ya Madola - ni ushirikiano wa hiari wa nchi zilizokuwa koloni za Uingereza, kwa jumla nchi 56. Kati ya hizo 15 zinaendelea kumtumia mfalme wa Uingereza kama Mkuu wa Dola (lakini bila mamlaka yoyote) na nchi wanachama 36 ni jamhuri zikiwa na raisi yao.
Ukitaka kujua kwa nini nchi hizi zinaendelea hivyo -kwa nini Tanzania ni mwanachama ? Nahisi ni utamaduni, historia, hasa mapokeo ya kisheria na mfumo wa mahakama...
Unaonaje??
Kuhusu picha ya marais wa Marekani, hili ni jambo tofauti. Demokrasia ni utaratibu wa ndani, ubeberu ni uhusiano wa nje.
Historia ina mifano ya diketa kuwa beberu, na mwanademokrasia kuwa beberu - au wote pia kinyume.
Pointi yangu ni: Uingereza walielewa kwamba siku za ubeberu zimekwisha, waliacha. kuhusu nchi kadhaa walijaribu kuendeleza mfumo huo kidogo, mfano jaribio la kuingilia Misri 1956. Lakini waliacha kwa sababu waliona wakati umeshapita.
Baadaye walijaribu kutumia ushawishishi wa kiuchumi kwa nchi kadhaa na kwa muda...
Lakini hatujaona jaribio la kurudisha ukoloni jinsi Putin anavyojaribu nchini Ukraine, pamoja na Moldova.
Kutokana na matagazo yake ni dhahiroi kwamba anaona mwisho wa ubeberu wa Kirusi kama kosa kubwa anajaribu hatua ya kulisahihisha. Hatua hii Waingereza hawakujaribu baada 1956 / Misri.
Majaribio hayo ni hatari kubwa kwa amani duniani.