Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mkuu inaelekea unafaidika sana na hila za Ulaya..

Makubaliano ya Urusi na NATO ni kwamba wasisogeleane mipakani ikiwa kila mmoja hataki kuhesimu sera za mwenzie...
Ulaya na US haijashika makubaliano hayo zaidi inajisogeza mipakani mwa Urusi kila kukicha

ULAYA imetumia mianya hyo kama silaha kwa zile nchi zinazokataa sera za kimagharibi ikiwemo kulazimisha ushoga, basi hupenyeza viongozi mamluki(puppet leaders) katika serikali zinazokinzana na sera zao, wakishindwa kuwaingiza kwa amani wanatumia (coup) kupindua serikali zilizopo madarakani kwa kisingizio cha udikteta..watatumia kufadhili upinzani ndani ya nchi yako au kuifadhili nchi jirani yako...

Kwa mfano EAC kuna nchi kama sio moja ni mbili zinafadhiliwa na serikali za ulaya na US kuleta taharuki ya hofu na machafuko kwa nchi jiran yake..hata wewe unalijua hili..
Mkuu tafadhali lete vyanzo na ushahidi kwa madai yako!
Mikataba inayoweza kutajwa ni kwa mfano Mapatano ya Helsinki ya mwaka 1975. Wakati ule nchi zote za Ulaya, pamoja na Urusi-Umoja wa Kisovyeti, zilipatana kuheshimu mipaka, haki ya kila nchi kujiamulia kuhusu ushirikiano na nchi nyingine, na ahadi ya kutotumia nguvu kama hali ya kutoelewana inatokea. (ona hapa)
Tangu mwisho wa Umoja wa Kisovyeti, Urusi na nchi zote zilizotokana na USSR zilithibitisha mapatano ya Helsinki. Mapatano ya Helsinki zimekuwa sheria ya kimataifa ya Kimsingi wa Ulaya.
Hakuna mapatano au mkataba kuhusu kuzuia nchi yoyote kujiunga na EU au NATO.
Ukiamini yako, lete ushahidi na matini yake!
(Nimeweka link ya Helsinki hapo juu)
 
US:
"Ukraine must stop the use of Patriot Systems until the investigation of the damaged system is completed"
-
Translation:
Patriot got wrecked.
Wamesha anzo hapo USA inatafuta kisingizio cha kuanza kuilaamu Ukraine kwamba Patriot ilitiwa kiberiti na Kinzhal kitokana na uzembe wa wa Ukraine walio kuwa wana- man US Patriot ADS wanatufanya wajinga kwamba hatujia kwamba all US mission critical arsenals eg Patriot and HIMARS zinakuwa manned na wanajeshi wa Merikani na si Waukraine kutokana na USA kuto amini wanajeshi wa Ukraine wana wasi easi kwamba Warusi wanaweza kuwashawishi Waukraine kuauzia silaha hizo za kimerikani au zinaweza kutekwa kirahisi na Warusi - waseme ukweli hapa kwamba silaha za Urusi zimeshinda kete silaha za Kimerikani wasianze kutafuta visingizio vya kulaahumu watu kumbe tatizo ni silaha zao za mchongo na si watumiaji - wairudishe kwenye drawing board Patriot air defense system au wawaombe Warusi wawafundishi jinsi ya kudesign silaha kiboko yao kama ilivyo AK-47 ambazo zimeusika zaidi ya millioni 50 Dunia nzima., hata Merikani wamejenga kiwanda cha kuunda AK-47 bila ya kuomba kibali kutoka Urusi - kwa nini??
 
Kwa nini waendeleze Ukoloni kwenye visiwa vya Chagos?

Hao Watu waliokubali kuwa koloni la Uingereza Wana asili gani?

Hii ina tofauti gani na ina maana gani?

Uingereza walivamia nchi zilizo mbali kabisa hazina hata Vinasaba nao.

Urusi ilichukua himaya baada ya kuwapiga Wamongoli.

Je, maeneo hayo zilikuwa nchi zinazo jitegemea?
Jibu ni hapana kwani ilikuwa nchi Moja chini ya Mongolia empire.

Sasa Kuna ubaya yeye kurithi maeneo baada ya kushinda Vita.

Je, Jamhuri ya Tuva haikuomba kujiunga yenyewe?
Huu nao Ukoloni?

By the way Uingereza ni mkoloni Toka kale mpaka Sasa.

Cheki hivi Visiwa anavyovishikiria

British overseas territories (formerly known as British dependent territories or Crown colonies) are: Anguilla; Bermuda; British Antarctic Territory; British Indian Ocean Territory; British Virgin Islands; Cayman Islands; Falkland Islands; Gibraltar; Montserrat; Pitcairn, Henderson, Ducie and Oeno Islands; St Helena and St Helena Dependencies (Ascension and Tristan da Cunha); South Georgia and South Sandwich Islands; Sovereign Base Areas of Akrotiri and Dhekelia (Cyprus); and The Turks & Caicos Islands (Foreign and Commonwealth Office: List of Crown Dependencies & Overseas Territories).
Mkuu umecheki mwenyewe?
Sehemu kubwa ya maeneo hayo yanakaliwa na watu weusi hasa huko Visiwa va Karibi (wajukuu wa watumwa wa zamani) walioamua kwa hiari yao kubaki chini ya mfalme wa Uingereza. Ama kwa njia ya kura kuhusu uhuru, au kwa njia ya kupigia kura vyama vya kisiasa vinavyotaka kuendelea vile.
Maeneo mengine kama St Helena ni ndogo vile hakuna anayetaka kubeba gharama za kujiendesha kama nchi huru; pia wana hali ya maisha iliyo juu kuliko majirani wengine.

Hapo pia sababu ukijiuliza kwa nini wenyeji wa Visiwa vya Mayotte (vilivyopo kati ya Msumbiji na Madagaska) walipiga kura mara mbili kukataa uhuru na kukataa umoja na Komoro. Sasa wako raia wa Ufaransa na wa Umoja wa Ulaya wenye haki zote. Hata wakiwa eneo maskini zaidi ndani ya Ufaransa, hata hivyo hali ya maisha ni juu kabisa kuliko visiwa vingine vya Komoro.


# Ona Bermuda: walipiga kura mwaka 1995 kuhusu uhuru. Asilimia 74 waliamua waendelee kama British Overseas Territory. (Je koloni gani ya Urusi ilipewa rukhsa kupiga kura kuhusu uhuru??)
# Gibraltar: walio wengi kabisa ni wenyeji; walipiga kura mara mbili kutoungwa na Hispania mwaka 1867 na mwaka 2002 (Je koloni gani ya Urusi ilipewa rukhsa kupiga kura kuhusu uhuru??)
# Falklands : asilimia 99.8% za watu wa Falkland walipiga kura kuendelea kama Overseas Territory (Je koloni gani ya Urusi ilipewa rukhsa kupiga kura kuhusu uhuru??)
 
"President Vladimir Putin [warned] that the destruction of the systems was an absolute certainty should they be deployed in Ukraine. He assured that with Washington now saying that they can put a Patriot in Ukraine, "Okay, let them do it. We will crack...”
 
"President Vladimir Putin [warned] that the destruction of the systems was an absolute certainty should they be deployed in Ukraine. He assured that with Washington now saying that they can put a Patriot in Ukraine, "Okay, let them do it. We will crack...”
Maneno haya aliyatamka miezi minne iliopita.

Kuna wajinga wakayachukulia kuwa ni mzaha
 
"We knew Ukraine's leader was expected to address the G7 leaders on Sunday, but via video link - though there had been speculation that he might turn up in person."

- BBC
 
Jumapili wana kikao kizito cha G7 mjini Hiroshima Japan.

Hiroshima ni mji ulipigwa bomu la majaribio la Nyuklia na Marekani pamoja na mji wa Nagasaki na kumaliza vita ya pili ya dunia mwaka 1945.

Zelensky ataungana na kikao kupitia simu ya video au teleconferencing.

Safari hii hakuna kuruka na ndege kaambiwa akae mahala (jina kapuni) lakini yahisiwa ni nchi mojawapo ya NATO.

Kwa kuwa Russia imezidisha mashambulizi mjini Kiev hali ya usalama viongozi wa Ukraine si nzuri.
The meeting will be historical.
 
Pointi yangu ni: Uingereza walielewa kwamba siku za ubeberu zimekwisha, waliacha.
Kama unadhani ukoloni na ubeberu umeshaisha duniani, tafakari tena mara mbili mbili, mkuu. Colonialism is alive and well.

Just because colonial powers don't actually occupy sovereign states, doesn't mean it's dead. Jiulize nani mwenye sauti Afrika kati ya viongozi wake na mataifa ya Ulaya na Marekani?

Kutokana na matagazo yake ni dhahiroi kwamba anaona mwisho wa ubeberu wa Kirusi kama kosa kubwa anajaribu hatua ya kulisahihisha.
Hapa ni wazi hujui maana ya ubeberu. Actually, Marekani ndiye beberu dhidi ya Ukraine kwa sababu bila yeye kujipenyeza na kuivuruga Ukraine, amani ingekuwa inatawala hadi sasa.
 
Wamenunua. Ni azimio la kisiasa kama unataka kuwekeza katika dhahabu.
Kuorodhesha Ufaransa pamoja na Mali haina maana kwa sababu dhahabu ya Ufaransa haitokei Mali, wananunua sokoni.
Angalia nchi nyingine. Italia , Uswisi, Japani, Uholanzi au Ujerumani hawana dhahabu kwao, wamenunua.
Tena uzalishaji wa Mali ni mdogo mno ukiinganisha na akiba ya Ufaransa.
Umejibu hoja moja kati ya mbili za muuliza-swali. Vipi kwa upande wa nchi ya Mali yenyewe? Kwa nini ina a lot of mines lakini haina hizo reserves?

Sikushangai sana kwa sababu hata majambazi na waporaji huwa wana mawakili wa kuwatetea mahakamani. Go! Go! Go!
 
Frankly speaking, ni almost dunia nzima versus Russia. Huku Afrika nadhani Saudhafrika na You-gun-Dar ya M7 ndizo pekee zilizo upande wa Putin.

^Wengine wooooooote ni punda^ ~ in Francis Atwoli's voice.
Unajua nchi ngapi za Africa zilikausha pale UN manyakng'au walipopeleka hoja ya kupiga kura kuinyanyapaa Urusi??

Hao uliowataja ni wale walioamua kujionyesha waziwazi
 
Back
Top Bottom