Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hapana sikuleta viongozi wa kikabila. Nimekutajia jina la Mieszko I aliyeanza kama mtawala wa kieneo akaendelea kuunganisha makabila mbalimbali akaunda ufalme wa Poland ulioendelea kwa karne nyingi.
Tena nilitaja kuimarishwa kwa dola la Poland chini yake na chini ya wafuasi wake.
Hayo yote wakati Moscow na Urusi havikuwepo.
Sasa umejisomea kidogo haraka-haraka unaleta majina ya miji na maeneo yenye historia ndefu ambako yalihamishwa kati ya Poland na madola ya Kijerumani, tangu 1918 au 1945 yako maeneo ya Poland.
HAyo yote haibadilishi ukweli wa kimsingi kwamba Poland ni taifa la zaidi ya miaka 1000.
Haibadilishi ukweli kwamba Poland iligawiwa 1776-1796 baina Urusi na Prussia na maeneo yake kuwa koloni za nchi hizo. Taifa la Poland liliendelea kwa karne moja bila dola hadi kurudishwa kwa Dola la Poland tangu 1918.
Haibadilishi ukweli kwamba Putin anajaribu kukamata tena maeneo yaliyokuwa makoloni ya Urusi zamani. Anaanza Ukraine na hapo sababu Poland inasimama imara sana upande wa ukraine kwa sababu wanaamini akifaulu pale, wenyewe watafuata.

Sasa ulilenga nini kwa maswali yako kuhusu Poland??
Naona unazunguka tu. Nimekueleza huyo mtawala unayemtaja wakati wa karne hiyo ni tawala ndogo ndogo tu mzee kama akina mtemi Mirambo na wengine.

Nimekwambia unieleze Hiyo poland mipaka wake uliishia wapi? Na hii poland ya sasa inaishia wapi?

Tunaongelea Poland kama taifa mdogo wangu.
 
Wewe ni LGBTQ

Na mara nyingi sana nimeshakukataa ku comment kwenye post zangu.

In short i don't like LGBTQ kwenye post zangu.
Hivi hakuna namna ya kublock asikuone kabisa? Moderators inabidi waboreshe hili.

Kuna wengine huwa hatukukariri majina, unabishana na mtu wiki hii, wiki ijayo unareply kwenye post yake kwa bashasha bila kukumbuka hii Id mlishapishana kauli wiki iliyopita.
 
Wachambuzi, tuzijadili siraha mpya kwenye uwanja wa SMO-F 16 planes, je zitakua na impact gani?

Russia watakua damaged how far na meassures za kuzidhibiti ni zipi?
Kuna makala zinaendelea kujadili suala hilo, unaweza kucheki kwenye link hapa kupata machache

20230521_225000.jpg
20230521_224925.jpg
 
Hapana sikuleta viongozi wa kikabila. Nimekutajia jina la Mieszko I aliyeanza kama mtawala wa kieneo akaendelea kuunganisha makabila mbalimbali akaunda ufalme wa Poland ulioendelea kwa karne nyingi.
Tena nilitaja kuimarishwa kwa dola la Poland chini yake na chini ya wafuasi wake.
Hayo yote wakati Moscow na Urusi havikuwepo.
Sasa umejisomea kidogo haraka-haraka unaleta majina ya miji na maeneo yenye historia ndefu ambako yalihamishwa kati ya Poland na madola ya Kijerumani, tangu 1918 au 1945 yako maeneo ya Poland.
HAyo yote haibadilishi ukweli wa kimsingi kwamba Poland ni taifa la zaidi ya miaka 1000.
Haibadilishi ukweli kwamba Poland iligawiwa 1776-1796 baina Urusi na Prussia na maeneo yake kuwa koloni za nchi hizo. Taifa la Poland liliendelea kwa karne moja bila dola hadi kurudishwa kwa Dola la Poland tangu 1918.
Haibadilishi ukweli kwamba Putin anajaribu kukamata tena maeneo yaliyokuwa makoloni ya Urusi zamani. Anaanza Ukraine na hapo sababu Poland inasimama imara sana upande wa ukraine kwa sababu wanaamini akifaulu pale, wenyewe watafuata.

Sasa ulilenga nini kwa maswali yako kuhusu Poland??
Halafu hebu pitia hii hapa kuhusu Urusi kidogo
Unamjua mwamba huyu

Vladimir the Great
Uhusiano kati ya Byzantium na Urusi uliimarishwa sana kupitia uenezi wa Ukristo. Katika karne ya 10, Kievan Rus, ambayo ilijumuisha eneo la sasa la Urusi, Ukraine, na Belarus, ilikuwa na uhusiano wa karibu na Byzantium. Prince Vladimir wa Kiev aliamua kuachana na dini za jadi za Kipagani na kubatizwa kwenye Ukristo wa Kiorthodoksi wa Byzantine mwaka 988. Hii ilisababisha kuenea kwa Ukristo miongoni mwa watu wa Kievan Rus na kuimarisha uhusiano wa kidini kati ya nchi hizo mbili.
 
Naona unazunguka tu. Nimekueleza huyo mtawala unayemtaja wakati wa karne hiyo ni tawala ndogo ndogo tu mzee kama akina mtemi Mirambo na wengine.

Nimekwambia unieleze Hiyo poland mipaka wake uliishia wapi? Na hii poland ya sasa inaishia wapi?

Tunaongelea Poland kama taifa mdogo wangu.
Mkuu unaonyesha tu kwamba ujuzi wake wa historia ni finyu. Hapana Mieszko I hakuwa mtawala mdogo kama Mirambo. Mirambo alianzisha milki iliyoporomoka mara moja baada ya kifo chake. Hakuelewa misingi ya kujenga dola. Wakoloni hawakupaswa kupambana na milki ya Mirambo maana ilikuwa iliporomoka kabla Wajerumani hawakufika Tabora.
Mieszko aliunganisha makabila mbalimbali na kuanzisha taifa. Nasaba yake (=familia ya kifalme) iliendelea kwa karne 3 hivi. Ufalme wa Poland ulikuwa milki iliyoheshimiwa sana wakati ule. Kama ungeelewa kitu ningedokeza mawasiliano na Kaizari wa Dola Takatifu la Kiroma na Papa wa Roma, wafalme wa Hungaria na watemi wa Kyiv.
 
Unaona sasa unakoelekea tena. Unashindwa kutoa maelezo yaliyonyooka. Umesema Rus haikuwepo karne ya 1.
Sasa nimekwambia unamjua Vladimir the Great?
 
Yaani hawa jamaaa ukiwaskiliza utadhani wao ndo miungu hapa wakiona umegundua kitu wanakuponda na kukutoa dhamani ila wakiunda wao kelele mpka maiti anaskia. Ila nnacho amini ni kwamba madhali mpka leo marekani anategema sana engines ya rockets za Urus basi Urusi Anauwezo mkubwa sana maana ni nchi chache sana zenye huo uwezo.
Hata anga za juu USA anamutegemea sana Russia, basi ni ujinga wa USA kujiona yuko juu lakini wapi, baada ya miaka 10-20 Russia na China watakuwa juu sana. Na scientist wengi wa USA Ni foreigners toka Russia, China, India na Africa kidogo, lakini USA anabeba credit zote.
 
Halafu hebu pitia hii hapa kuhusu Urusi kidogo
Unamjua mwamba huyu

Vladimir the Great
Uhusiano kati ya Byzantium na Urusi uliimarishwa sana kupitia uenezi wa Ukristo. Katika karne ya 10, Kievan Rus, ambayo ilijumuisha eneo la sasa la Urusi, Ukraine, na Belarus, ilikuwa na uhusiano wa karibu na Byzantium. Prince Vladimir wa Kiev aliamua kuachana na dini za jadi za Kipagani na kubatizwa kwenye Ukristo wa Kiorthodoksi wa Byzantine mwaka 988. Hii ilisababisha kuenea kwa Ukristo miongoni mwa watu wa Kievan Rus na kuimarisha uhusiano wa kidini kati ya nchi hizo mbili.
Kwa nini nisimjue mtemi Vladimir I wa Kyiv? Jinsi ulivyokopi, Vladimir alikuwa mtemi wa Rus ya Kyiv. Labda jisomee kidogo hapa: Rus - Wikipedia, kamusi elezo huru

Rus ni tofauti na Urusi. Milki ya Rus ilikuwa mzizi mmoja uliozaa baadaye nchi tofauti. Vladimir mwenye alikuwa mtu wa Skandinavia (takriban Uswidi) aliyetawala njia ya biashara kati ya Bahari Baltiki na Mediterenae kupitio mito mikuwa ya maeneo ambayo leo ni Ukraine na Urusi.
Vladimir alibatizwa mnamo mwaka 988 akapokelewa kati ya watawala wa Ulaya ambao walipuuza wapagani. Ila hakutumia cheo cha "tsar" (mfalme).

Baada ya kuporomoka na kugawiwa kwa milki ya Rus, maeneo madogo yaliendelea ; utemi wa Moscow ulitokea baada ya kugawiwa kwa utemi wa Vlodimir. Utemi huo wa Moscow uliendelea baadaye kuwa Urusi.
Unaweza kuanza na Danieli wa Moscow, aliyekuwa mtemi mdogo wa kwanza huko. Watemi wa Moscow walipaswa kutii Wamongolia hadi kuvunjika Umoja wa Wamongolia; mwanzoni walikuwa walikuwa wote machifu wadogo.
Ni kuanzia Ivan III tu kwamba walivunja ukuu wa Wamongolia (1480) na kuongeza maeneo yao. Hata hivyo ilikuwa bado eneo dogo ukiinganisha na Poland wakati ule.
 
Unaona sasa unakoelekea tena. Unashindwa kutoa maelezo yaliyonyooka. Umesema Rus haikuwepo karne ya 1.
Sasa nimekwambia unamjua Vladimir the Great?
Jaribu kusoma yale yaliyoandikwa. Sikujadili "karne ya 1". Rus ilianzishwa mwisho wa karne ya 10. Lakini Rus si Urusi.
(Putin anapenda kuiamini na kukamata sehemu hiyo ya historia, lakini si vile)
 
Hata anga za juu USA anamutegemea sana Russia, basi ni ujinga wa USA kujiona yuko juu lakini wapi, baada ya miaka 10-20 Russia na China watakuwa juu sana. Na scientist wengi wa USA Ni foreigners toka Russia, China, India na Africa kidogo, lakini USA anabeba credit zote.
Mkuu ukitabiri wako China itakuwa juu ya Marekani, uwezekano huu upo. Ila kwa hakika si Urusi.
HAlafu ni kweli kwamba wanasayansi wengi wa Marekani walizaliwa nje ya nchi hiyo na kuhamia Marekani. Ila kwa nini unaangalia hali hiyo kama udhaifu au hitilafu?
Heri ujiulize kwa nini wanasayansi vijana wanapanga foleni kusoma na kufanya kazi MArekani, lakini hawapangi foleni kukaa Urusi - kinyume chake juzi angalau milioni ya wasomi walikimbia?
Hata China hadi sasa hawako wengi wanaotaka kuingia kule...
Unaonaje?
 
emoji298.png
emoji298.png
The U.S. Department of Defense on May 21 announced a new military aid package for Ukraine worth $375 million, aimed to help Ukrainian forces "push back against Russia's unprovoked war of aggression."

The latest package includes additional ammunition for U.S.-provided HIMARS rocket launchers and artillery rounds, as well as Javelin anti-tank missiles and AT-4 anti-armor systems.

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Kituo kinacho fata Odessa
Usicheze na Russia wewe naomba mungu akuweke uje uwahadisie wajukuu zako kuhusu Russia.
 
Kabla ya Patriot kuangamizwa ilikuwa inarusha mabomu hovyo hovyo.

Ilirusha mabomu kama 20 hivi. Hapo hapo Kinzhal missile ika penetrate na kuiangamiza Patriot.

Kuna swali wachambuzi wanauliza je Russia Aerospace Forces wali hack systems za Patriot mpaka ikawa inarusha mabomo hovyo hovyo bila mpangilio?
Inaonyesh patriots zao zilipanic na kupokea erro of signal (signal jam)[emoji16][emoji16]

Then mwanaume akaiadabisha,

Ikija kutoka cover ya Russian war against Ukraine kwa mfumo wa filam/CD sizan kama soko litabakiw na nakala wanawez zalisha mwaka mzma na uhitaji unaendelea
 
Back
Top Bottom