Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kwa nini hao 15 walijipiga risasi mkuu? Na ni lini? Samahani lakini kwa kukuuliza
Bila samahani mkuu humu tunaelimishana. Mwaka 1944 Field Marshall Erwin Rommel alitakiwa anyongwe. Kutokana na kuwa maarufu kuliko majenerali wote jeshi la Ujerumani ilimuwia vigumu Adolf Hitler kumuua kwa execution squad maana ingepunguza morali ya jeshi na wananchi.

Akashawishiwa ajiue mwenyewe familia yake itapewa mafao yote ambayo wangekosa endapo angehukumiwa kufa. Akajipiga risasi na kutangazwa amekufa kwa majeraha ya vita, akazikwa kwa heshima za kijeshi na uzuni kubwa.

General George S. Patton Mmarekani aliyekuwa mtukutu mno na mwenye tabia kama majivuno, ubishi, upinzani na jeuri alionekana atakuwa threat. Kabla vita haijaisha walikuwa wanatafuta namna ya kumdispose wanashindwa.

Mara tu baada ya vita alifia Ujerumani kulekule kwenye mission ya denazification (hii ambayo Putin ndio anaita sasa). Alifia kwenye ajari ambayo gari lake liligongwa na gari la jeshi na aliyelazwa ni yeye pekee kati ya wote. Alifia hospitali

Ofisa wa usalama wa taifa au ofisa wa jeshi kujipiga risasi au kupata ajari kwenye private car kunakuwa na namna. Personnel wa kawaida kujiua utasema stress za pesa au mapenzi, mabosi hawana stress za kimaisha kujiua na wanatembea kwa convoy chance za ajari ni ndogo. Hao 15 wa Russia walijiua kwa nyakati tofauti tangu 1991 mpaka 2016. Ni miongoni mwa vifo vya maofisa wa jeshi kwa interval hiyo
 
Malighafi wanauza wengine pia. Kama Urusi wangekuwa nchi ya pekee - hii ingewapa mamlaka kubwa. Jinsi ilivyo sasa kuhusu gesi ya nchi kadhaa za Ulaya. (wanajitahidi kupata mbadala; Ujerumani wameanza sasa kujenga bandari kwa gesi inayofika kwa meli . hadi sasa walitegemea gesi ya Urusi kwa njia ya bomba).
Mambo yote bado yapo duniani. Hakuna haja kwenye sayari.
Mafuta: Venezuela na Iran watafurahi wakipata tena wateja kwa mafuta yao. Pamoja na hayo Ulaya inaelekea kupunguza mahitaji yake kwa kurukia nishati mbadala kama sola na upepo, na hidrojeni.

Kumbuka (ulipendelea kutojibu): Putin angeweza sasa kulazimisha Waulaya kama angezima gesi yake. Kwa sasa hivi hawana mbadala (bado). Lakini hazimi. Anahitaji kila senti.
Jomba jomba... Mbona unaonekana mfuatiliaji ila unafaitilia kimahaba...

IMG_20220313_090326_133.jpg


Unaeza kuniletea nchi yenye capability chini ya jua ya kufill hlo Gap?

Unaeza kuniletea nchi yenye uwezo wa ku'compesate 11.3Mil Barrel per Day anazozalisha mrusi?

Hivi hesab kwako iko vizuri kweli?

They told you more than 30% of world natural resource imelala kwenye ardhi ya mrusi ilhal just as little as 1.4% of World population ndo iko pale... At kuchekecha tu akili apo kuwaza mara mbil hutaki?

IMG-20220313-WA0002.jpg


Unaelewa ata maana ya 1 kwa 10... Kwasabab meanza kupata mashaka na hesab zako... 1 ya 10 ukiipeleka kwenye asilimia ni sawa 10%... Apo wastani kwa dunia nzima.... Katka nchi zaidi ya 200 hujiulizi kwanini aslmia 10 zote n yeye?

Et Venezuela so unataka kunambia Venezuela ndo anaenda fil gap la Mrusi sio? Em nenda kwenye raman kisha itizame venezuela kisha litizame bara la Ulaya...

Kama kweli we n mchumi angalia Transportation cost y huo umbali kufanya importatiom...

Na nikuulizs tena swali kutoka kwa Venezuela uliyekmbilia kumtolea mfano. Anao uwezo wa kusupply kias alichokua anakisambaza mrusi?

Jibu ni Hapana ata OPEC countries ambao ndo wazalishaji hasa wenyewe wanakwambia hyo Gap haijaziki af we nani wakusema huo upupi unaozungumza apo...

Sorry ka ntakua metumia kauli kali... Ila kwa navyokutizama hauko teari kunisikiliza unless mekubali unachojarib kunishawishi... Af bahat mbaya sitakubaliana na ww ko itakuwa kama mabishano kitu ambacho sipendi na sihitaji kufanya.

Ko ili tusichoshane endelea kuamini hivo hivo kwa akili zako za kizungu kwamba vikwazo vinaenda kumpoteza Russia kwenye Ramani.

Tena kwa hivo vikwazo vya kuambiwa bia imepanda uku kule gas imepanda af mwana uchumi unajua hesab na una akili zako timamu unajisifu kuna mtu kakomolewa....

Kiasi unasifia anasa kupanda bei flam amekomolewa kwa vikwazo uku kikwazo kile kile kinakutafuna kwenye uzalishaji...

Hunielezi kwanini bei imetoka 1.78USD kwa Gallon mpk 4.35USD kwa mtu unaedai anajitosheleza... Hv "Demand and Supply Rule" unaijua.... Ukifinya supply what ilhal demand n kubwa unategemea nn kwenye price?

Na kama supply iko balanced inajazwa can you try alittle ata kuelezea why price inakuwa ka Demand na supply vuko correlated.

Mwanzo likuwa naona unaeza ila sa hivi naona ndo unazidi kwenda chaka... But no sio chaka [emoji847][emoji847][emoji847][emoji847] ndo fikra zako ziliko.

Ukiendelea kua na mawazo ya kumkomoa af ukaanza kutafta data za kuchambua hil swala hautakuwa na tofauti na Daktar anayemfanyia upasuaji ndugu yake wa karibu anaemuathiri kihisia...

Taaluma inakuponyoka unapelekwa na hisia matokea unafanya kitu ambacho si sahihi...
Una data kibao ila unachagua ya kutumiia na zaidi unajifumba uelewa... Yani unashindwa kuzi'analyze...

So nipumzishe kidogo mzee... Endlea kuamini hvo hvo unavoamini so dhambi ndo uwezo wako wa kufikri ulipoishia...

Narudia tena kukupa neno kua RUSSIANS are not ZIMBABWEANS.
 
Malighafi wanauza wengine pia. Kama Urusi wangekuwa nchi ya pekee - hii ingewapa mamlaka kubwa. Jinsi ilivyo sasa kuhusu gesi ya nchi kadhaa za Ulaya. (wanajitahidi kupata mbadala; Ujerumani wameanza sasa kujenga bandari kwa gesi inayofika kwa meli . hadi sasa walitegemea gesi ya Urusi kwa njia ya bomba).
Mambo yote bado yapo duniani. Hakuna haja kwenye sayari.
Mafuta: Venezuela na Iran watafurahi wakipata tena wateja kwa mafuta yao. Pamoja na hayo Ulaya inaelekea kupunguza mahitaji yake kwa kurukia nishati mbadala kama sola na upepo, na hidrojeni.

Kumbuka (ulipendelea kutojibu): Putin angeweza sasa kulazimisha Waulaya kama angezima gesi yake. Kwa sasa hivi hawana mbadala (bado). Lakini hazimi. Anahitaji kila senti.
Na apo mwisho sikukujibu kwasabab hufikirii kwa utashi wako unafikiria kwa mhemko...

Na ka ungekuwa na fikra huru ungemsif Putin sio kwa kuivamia Ukraine bali kutokukurupuka ka wanavokurupuka wenzie na vikwazo vyao...

Narudia tena kukuonesha hii picha...

IMG_20220313_090326_133.jpg


Af nambje who care for humanity... Who care consequences za Civilians kati ya hao western unaowaabudu na huyu Putin unaemchukia...

Akisema azime kama unavohitaji anawaumiza viongozi wanaoshinda ofisin kunywa kahawa na kalam mkonononi au Raia wa nchi hizo?

Mnyonge mnyongeni ila usipuuze kizuri afanyacho... Akisema afunge ghafla hapo ulaya patakalika? Mbona una fikira za kushikiwa sana jamaa angu.

Western wana attack raia wa kirusi moja kwa moja kumkomoa Putin na huo ni Upuuzi je unataka naye afanye hivo kukomoa Raia wa Ulaya....?

Walioshiriki maamuzi sio hao zaidi yya Mil.700 watu waliopo ulaya bali their Corrupt Politicians who siku zote they don't care about Raia wao...

Usimwage sumu baharin kisa samaki mmoja tu ilhal unaenda kuangamiza samaki na viumbe wengine baharini... Na binafs naona hicho Putin hana...

Angekuwa na roho mbaya ka hao ndugu zako wanaojinasibu wamestaarabika wangekuwa washamfungia kitambo mno...

Ka una akili kweli unaeza acha kununua kiberiti cha sh 100 kenya kwenda kufata cha 500 Nigeria kisa tu unataka kumfundisha adab mkenya? Hizo ni akili au upuuzi?

Nakukumbusha tena wenye roho ya kikatili kias hcho ni western tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ambao wanajilipulia tu ka wanavofanya sehem zingine.

Hii nazan ndo last text kukujib zaidi ya apa ntakupuuza kama mwanzo uendelee kukamata hicho hicho ulichonacho ili uendelee kujifrahisha zaidi...
 
Malighafi wanauza wengine pia. Kama Urusi wangekuwa nchi ya pekee - hii ingewapa mamlaka kubwa. Jinsi ilivyo sasa kuhusu gesi ya nchi kadhaa za Ulaya. (wanajitahidi kupata mbadala; Ujerumani wameanza...
Wew tuishie kwenye vita tuu usiingilie fani za watu ungekuwa mwanauchumi si tungekuwa kama South now unajiona unatumia akili kuuubwa kwa hiyo hiyo gesi inayosafirishwa itakuwa itakuwa ya bei cheep kuliko inayokuja na Bomba you think your too intelligent bt your an empty head
 
Samahani, hivi unaichukulia Russia kama nchi za kiafrika siyo.
Wewe ulisema russia wanauza raw material. Unajua kuhusu international space station!?
Unajua china ananunua silaha za kivita kutoka Russia!?
Bila samahani. Ni vema kujadiliana kwa ustaarabu hata tusipokubaliana. Hapana Urusi si kama nchi ya Kiafrika. Lakini nimeangalia uchumi wa nje. Tazama Urusi, linganisha na China na Marekani. Warusi wanaweza kuuza hasa malighafi na bidhaa zisizoongezeka thamani sana - mfano feleji na mabati ya feleji (ukitazama orodha ya wikipedia kwa haraka, ukisikia dharau bado, nenda kwenye chanzo hapa (unaweza kubadilisha country pale juu). Wanauza pia mashine, magari, madawa (bidhaa zilizoongezeka thamani ) lakini hizo ni kama 5% za export yao. Maana hawana vitu vingi vyenye thamani iliyoongezeka ambavyo watu nje wanataka. Linganisha Marekani: kwao bidhaa hizi ni zaidi ya 40%; angalia China kwao ni juu ya 50%. Maana hao wanazalisha vitu vingi ambavyo watu wengi wanatafuta.
Ninachukua namba hizi kama dalili ya uwezo ya uchumi.

Silaha ni sehemu ambako Urusi imekazia, tangu siku za ukomunisti. China imenunua sana kutoka Urusi, lakini China imepunguza manunuzi kutoka huko, wanapendelea kutengeza silaha zao wenyewe na hapa wanasogea mbele. Katika mengi yanayohitajika katika silaha za kisasa kuna hasa elektroniki - na hapo kuna mapengo. Tulipata habari nyingi jinsi gani vikosi vya Urusi katika Ukraini vilisikilizwa kwa sababu walikosa vifaa vya kisasa ambavyo haviwezi kusikilizwa. (au vifaa ambavyo viligoma)

ISS: Warusi wana vifaa vizuri vya usafiri vya anga lakini kiteknolojia ni vya juzi. Marekani NASA walishindwa miaka 10 iliyyopita walihitaji Soyuz za Urusi kufikisha wanaanga juu na kuwarudisha. Sasa makampuni ya binafsi zimepita kila kitu kilichowahi kutengenezwa na NASA au pia na ROSKOSMOS ya Urusi. Makombora ya Elon Musk (mtu wa Afrika Kusini mwenye uraia wa Marekani) yanapita uwezo wote wa vifaa vya Urusi pia vya serikali ya Marekani. Warusi walitishia kidogo wangeondoa vipande vyao kwenye ISS. Musk alicheka tu alisema waende tu. Ataendelea na vifaa vyake. Hadi sasa inaonekana anaweza.
 
Wewe jamaa ni very naive.

First of all vikwazo alivowekewa Russia sio vya kuleta matokeo kesho asubuhi ila vikwazo ambavyo vitamzoofisha in short and long term.

Russia uchumi wake kwa zaidi ya 20% unategemea mafuta, na kwa taarifa na wengi hawaijui ni kuwa USA na Canada ni wazalishaji wakuwa wa mafuta USA ni wa kwanza Duniani, Bei ya Mafuta haipangwi na taifa moja ndio maana Bei inapanda hata kwa mataifa ya yanayozalisha sana, ili kupunguza makali ya bei, Marekani huwa wanaakiba ya Mafuta, wenyewe wanaita Strategic oil reserve huitumia kipindi ambacho kuna emergency hasa kipindi hiki, Kwa taarifa yako USA wangekuwa wanatoa tu hii reserve wanaweza kuireplace Russia ndani ya mwezi kama muuzaji mkuu wa Mafuta.

Saudi Arabia ndio silaha kubwa ya marekani linapokuja suala la Nishati duniani, ni suala la muda tu Saudi Arabia ataongeza uzalishaji, Pia Marekani tayari amepata unlikely Ally kwenye hili naye Ni Venezuela, Venezuela ndio taifa lenye kiwango kikubwa cha mafuta kilichogundulika ila bahati mbaya hanufaiki nayo kwa sababu ya vikwazo (China na Russia hawajuzia kuathiriwa na vikwazo vy Magharibi)

Kuna watu wanasema Russia itaitumia China kukwepa vikwazo (at least watajaribu) wote wanaosema hivi hawajawahi kuwe kwenye Biashara za kimataifa ambazo zinahusiana na kuhamisha mitaji kati ya nchi na nchi, Kila mtu anayefanya Biashara na taifa fulani anaangalia kitu kinaitwa "Financial Risk of Doing Business", ahadi na ndoto hazishibishi hapa Pro Russia muelewe, Wiki Iliyopita Xiaomi kampuni ya China ilipunguza 50% ya Biashara zake inazofanya na Russia, na si Xiaomi pekee na hata Mabenki ya China yanakwepa kufanya miamala ya Benki za Urusi.

Unasema ticket za Ndege za Mataifa ya Ulaya zimepanda Bei, Hivi kupanda Bei na Shirika lako kufa Bora nini?
Kama hujui au kwa faida ya wengine Shirika la ndege la Russia ndege zake zote ni Airbus na Boeing isipokuwa 10 au 20 ndio zinaundwa Russia, hapo Boeing na Airbus wamejitoa kufanya biashara na Russia, this means they will not be able to get Spare parts and therefore lazima wapunguze Safari za nje au za ndege hizo, this means hadi Airline industry irudi kama kawaida sio zaidi ya miezi 12.
China mshirika wa Karibu wa Russia ndege zake karibu zote ni Airbus na Boeing, ameshindwa kumuungisha mshikaji wake (Hebu jiulize Kwa nini), au kama unajua maifa yanatumia Ndege za Russia hapa Africa yataje, now imagine kampuni inayoziunda ndege itakuwa na hali gani baada ya miezi 12?

Russia ana provide Rare Earth, Nickel na raw materials nyingi sana kwa Ulaya, na yeye hawezi kuuacha kuwauzia kwa sababu ndio msingi wa Uchumi wake, Kama hujui na kwa faida ya wengine Tanzania ina Deposit ya Nickel ambayo dunia nzima wakiacha kuchimba tutaweza kumuuzia kila mtu kwa miaka 30, na kambuni ya Kabambaga Nickel ni Kampuni ya Uingereza (Kwa usajili) so tutarajie speed ya ujenzi kuongezeka.

Umeitaja BRICS, hii sio formal wala informal alliance, kwanza wana tofauti za kimipaka, kisera, lengo lao lilikuwa ni kujaribu kuzichallenge IMF na WB ila hadi leo Nchi karibu zote za Africa na zinazoendelea zinakimbilia IMF na WB (Mfano Tanzania), hii ina imply Western financial Frameworks and Institutions are very strong kwa sasa labda itokee vita kubwa sana, that will destroy our civilazion.

Vita ni gharama na hii gharama ndio Silaha ya watu wa Magharibi
Angalau mtu mmoja anayejua kusoma takwimu na tarakimu kati ya majenerali wa kitandani
 
Bila samahani. Ni vema kujadiliana kwa uataarabu hata tusipokubaliana. Hapana Urusi si kama nchi ya Kiafrika. Lakini nimeangalia uchumi wa nje. Tazama Urusi, linganisha na China na Marekani. Warusi wanaweza kuuza hasa malighafi na bidhaa zisizoongezeka thamani sana...
Nakuuliza. Unataka tujadiliane au tubishane!?

Nakusihi jifunze uchumi kwanza ndio uje tujadili.
 
Kwa sasa zitakuwa kama porojo tu kwe huu huzi... Unachokiona mbele nahisi ni tofauti na nachokiona kwa upande wangu kulingana na analysis zangu mwenyewe.

So whether uko sawa au hauko sawa sizan ka na haja ya kuk'prove wrong o right ilihal mda upo na mda utaongea....

But bnafs kwa analysis zangu mwenyewe na bet kwa mrusi kwenye hivi vikwazo vyote anatoboa tena kwa 98% efficiently kbs.

Nikukumbushe tu Mrusi anafanya biashara ya Rasilimali sana sana na sio Technology Health care au vitu vinginevyo kiivo... Na rasilmali alizo nazo ni "Basic needs" so "Additional" ambazo kila nchi inazihitaji na ni nchi zilzokua au tayari ambazo zimekwisha kua...

Waswahil wanasema kuoga hiari kula lazima.

Nikurejeshe nyuma Europe + USA + Canada na nchi zingine kama Australia Japan na Korea Kusini Plus Singapore zote kwa pamoja zina Account about 1.3Billion kwenye Population ilo na watu zaidi ya 7.8Billion dunian.

Biashara hufanyi na kuku unafanya na watu so rejea hio Population ilobaki inahtaji malighafi za mrusi achilia mbali sector zingine...

Geuka nyuma angalia huu muungano wa BRICS yani Brazil, Russia mwenyewe, India, China na South Africa aliyejiungha juzi... Hyo ni Primary back up ya Mrusi inayo accounts for more than 40% of the world Population. Apo hujataja marejeo kama nchi zingine Africa ukaenda mbali zaidi apo Middle East ambao hawajajihusisha na hivo vikwazo vilivowekwa....

Ukitaka kupata usahih wa unachokizungumza zama deep kuangalia kila nchi iliyojihusisha na Vikwazo kwa Mrusi namna wanavyoingiliana kibiashara na tizama kwa jicho huru utaona nani atakayeumia na hivi vikwazo zaidi...

Kisha ingia ndani zaidi angalia kwa umakini kinachoondoka Urusi na kinachozuiliwa na wazuiaji kipi kina maana...

Huezi ukanambia unazuia wafanya biashara wako wasipeleke "Gongo" kenya kisha unazuia uingizwaji wa mafuta nchini kwako kutoka kenya et unamkomoa ilhal unawaumiza nduguzo ulonao kwa inflation ya bei...

Nikuulize tena swali... Toka hvo vikwazo vimeanza umesikia kuna mfumuko wa bei Urusi... Italy kawekewa vikwazo kwani mpka afunge viwanda uzalishaji kisa gharama za umeme kupanda? Au italy ndo Russia?

Either wajua au umesahau nikukumbushe... Nini kinafata baada ya nishati gharama kupanda? Ni mfumuko wa bei mpk kwa mahtaji ya kawaida ya mwananchi mdogo chini...

Sasa nikuulize tena hyo jump ya gharama za umeme kutoka $100 mpaka $175 zimetokea Russia au Europe? Hizo gharama za usafiri zinawaathiri warusi au wenyewe?

Kingine umezungumzia kuhusu makampuni ya nje... Em nenda apo UK achana na biashara za ndani nambie Club kubwa ulaya inayomilikiwa na mzawa...

Nenda tena kaorodheshe katka Club 20 zinazoshiriki league kuu ni ngapi zinamilikwa na wazawa na zipi zinamilikiwa na wenyeji... Apo nakutolea mfano kwenye michezo tu hujaingia kwe biashara halisi...

Nikukumbushe tena hakuna kampuni kubwa duniani ambalo liko whole owned na wazawa... Apple the most valued company iko registered in USA ila share holder wamezagaa dunian kote. The same to Alphabet Inc. na mengineyo so nakupa notice ya ziada kua Investors popote dunian huwa wanaangalia "Opportunities"...

Na ndo maana ukawaona warusi hao hao wakivuka mipaka ya nchi yao kuwekeza kwenye mataifa mengine...

Nazidi kukudokeza kua Russia ina Over 110 Billionaires kati ya 2700 tuwajuao... That's is over 4.22% ya Billionaires wote duniani... na ni number 5 baada ya USA kisha CHINA kisha INDIA, kisha Germany Kisha yeye... Apo number of Millionairea iko zaidi ya zaidi ya malaki ya watu..

Na hao sio mabilionea na mamilionea wa Tsh bali USD... Idadi ya mabilionea walioko Russia ukilinganisha na UK ni takriban mara mbili ake... UK wapo ka 54 hv...

Je hao wafikir hawawezi kwenda kwenye rest of population kuwekeza???? Kama waliekeza Europe wanashinda kuekeza sehem nyingine? Fedha wanazo.

Ko nirudie tu kukwambia una Idea nzuri za uchumi sema una "mahaba" yanakutoa kwenye Reli... Fanya deep analysis kwe hil jambo bila ushabik utaona "utumbo" mwingi unaofanywa na siasa za kimagharibi hasa hasa kwe huu mzozo...

Ningeandka mengi ila nachoka... But kwa hayo machache niishie apo.
Huu mwaka 2022 kabla haujaisha utashangaa msimamo wako.

1. Russian aviation will collapse soon. Hakuna spare parts wala maintenance kutoka kwa Boeing wala Airbus, tegemea ajari za ndege kuwa nyingi na kuwa unreliable. Russian made Sukhoi Superjet-100 zipo chache sana na zilinunuliwa kisiasa, wengine walionunua kina Mexico walizirudisha baada ya ajari na maintenance problems.

2. Marekani anao uwezo mkubwa wa kuzalisha mafuta, ni kitendo cha yeye kuwa na uhakika hana source ya mafuta utaona kama atazima viwanda. Ana oil rigs ziko under utilized na ana fracking technology akiwa nayo yeye tu duniani. Marekani alinunua 'dirty oil' ya Russia hili kutoacha mitambo yake dormant isiharibike, kaweka sanctions na gharama za uzalishaji kwa njia nyingine kwake ni kubwa ila sio kwamba hawezi.

3. Russia WILL NEVER survive without oil money. Hii Russia haina jeuri ya kuzima gesi kwenda Ulaya maana zaidi ya nusu ya mauzo itapotea na provided that wana vikwazo sekta nyingine.

4. Muungano wa BRICS ni irrelevant kwa Russia kwa sasa. Kina EU wana sarafu moja, sheria zinazofanana za mlaji na vitu vingi vinaendana. Ndani ya BRICS hakuna nchi itasideline na Russia na iache dunia nzima. Hakuna nchi humo kwenye BRICS eti iache kutumia SWIFT ikatumie ule mfumo wa Urusi alioanzisha February ambao hautumiki popote zaidi duniani. Hakuna nchi itaachana na VISA au MasterCard itumie UnionPay kisa Urusi.

5. Immediately mdororo wa uchumi utakuwa kwa Western. Miezi michache ijayo kama vita itaendelea au iishe ila vikwazo viendelee maumivu ya vikwazo kwa Russia yataonekana waziwazi. Hii dunia haitaki uishi mwenyewe kuna global economy nchi zinategemeana
 
Russia has said it is banking on China’s help to withstand the crippling economic sanctions placed by Western nations over the war in Ukraine as the United States warned Beijing not to provide that lifeline.

Russian Finance Minister Anton Siluanov said sanctions had deprived Moscow of access to $300bn of its $640bn in gold and foreign exchange reserves, and added that there was pressure on Beijing to shut off more.

“We have part of our gold and foreign exchange reserves in the Chinese currency, in yuan. And we see what pressure is being exerted by Western countries on China in order to limit mutual trade with China. Of course, there is pressure to limit access to those reserves,” he said on Sunday.

“But I think that our partnership with China will still allow us to maintain the cooperation that we have achieved, and not only maintain, but also increase it in an environment where Western markets are closing.”

Mtu anakaa Mbagala au Yombo anaanza kusema vikwazo haviumizi, sijui China atamsaidia Urusi, kukwepa Maumivu, 50% mabenki yanaogopa kutrade
Haya we kenge wa Mbezi, Masaki, Upanga, Oyster bay vikwazo vinawaumiza?
 
Urusi ilijipanga kufanya hiki anaachokifanya muda mrefu, Putin anajua kabisa hawawezi kutia pua zao pale wataishia kwenye sanctions tu.

Wangekuwa smart enough wange mshaauri Rais wa Ukraine kuondoka nchini mapema kabla ya uharibifu mkubwa.

Shida nyingine huyu Comedian hatumii akili yake vizuri, Anakua wazi kabisa hii vita hata shinda hata Yesu arudi na nchi itaharibika, huko mbele tunakuja kuiona Ukraine ikiwa nchi iliyopoteza mvuto kwasababu ya ujinga wa mtu mmoja asiye na akili nzuri ya kufikiri.
Hakiona haibu kuwa hawezi kuishi bila majivuno, ajifunge baruti halafu ajilipue
 
Back
Top Bottom