Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Mkuu ubarikiwe Valimir Vladirmovich Putin the great.
 
Asante, hata hapa angalia miaka mitano, utaona kila mwaka muundo huohuo (sijui kama ni namna ya kutunga takwimu kwao ili wanze Januari chini na kutoa mengi Disemba??). Hata hivyo, pia thamani hii iko ndani ya asilimia tano za exports za Urusi za bidhaa zilizoongezeka thamani sana nilizonyesha huko juu.
 

Nini jipya hapo, huyo rais wa Ukraine siku zote amesema yupo tayari kwa mazungumzo, ameomba tangu mwanzo wafanye usuluhisho bila mauaji, ila huyo Putin wenu mnywa damu amekua king'ang'anizi hataki kuskia chochote, amewatuma wanajeshi Warusi kuuana na ndugu zao, wanajeshi vijana wengi Warusi wamekufa kwenye huu ugomvi na wanaendelea kufa na watakufa wengi tu.
 
Mzee ulikuwa unasema russia exports raw material. Sasa unaanza kuhamisha mada. Hivi umafikiria Russia ni kama kenya siyo!?

Hapo umeona passenger cars unaanza kulalamika tena.

NIMEKUULIZA UNATAKA TUJADILI AU UNALETA UBISHI TU!?
 
Wacha ku exaggerate
 
Asante hii ni kazi zuri ila ina matata. Nikiangalia habari kutoka jirani Uruguay Warusi walifaulu kuwauzia Waargentina treni za umeme kwa njia ambako hakuna umeme. (bado??). Basi hata hivyo - Transmashholding ni kampuni kubwa sina shaka itakuwa treni nzuri (lazima - Urusi kuna kati ya mitandao makubwa zaidi ya reli duniani). Ila tu - hawauzi sana nje. Maana ingawa Transmashholding ni mzalishaji mkubwa wa reli Urusi, hawauzi sana nje. Maana hawako kati ya makampuni wanouza sana nje - hao ni kutoka China, Kanada, Ujerumani, Ufaransa .... ona namba chini.
Pia hawakufikia High tech bado katika reli. Maana hata njia 3 ndani ya Urusi zenye kasi kubwa (zaidi ya 200 kmh) wanatumia injini kutoka Alstom-Ufaransa au Siemens-Ujerumani. Nahisi ni tatizo kama ndege zao,. Ndege za kijeshi - ziko za kisasa (kiasi). Ndege za abiria: hata Wachina waliacha muda mrefu kununua ndege za kirusi wanatumia Airbus na Boeing.


RankCompany2019 Revenue ($ Billion)Country
1​
CRRC Corporation
32.4​
China
2​
Bombardier Transportation
15.8​
Canada
3​
Siemens Mobility
10.1​
Germany
4​
Alstom Transport
9.3​
France
5​
GE Transportation
3.8​
US
6​
Stadler Rail AG
3.4​
Switzerland
7​
The Greenbrier Co
3​
US
8​
Trinity Rail Group
3​
US
9​
Hyundai Rotem
2​
South Korea
10​
Hitachi Rail Systems
1.7​
Japan
 
Mzee ulikuwa unasema russia exports raw material. Sasa unaanza kuhamisha mada. Hivi umafikiria Russia ni kama kenya siyo!?

Hapo umeona passenger cars unaanza kulalamika tena.

NIMEKUULIZA UNATAKA TUJADILI AU UNALETA UBISHI TU!?
Mpendwa, niruhusu nilete nukuu yangu. Pale juu #12,220 niliandika
" Wanauza pia mashine, magari, madawa (bidhaa zilizoongezeka thamani ) lakini hizo ni kama 5% za export yao. Maana hawana vitu vingi vyenye thamani iliyoongezeka ambavyo watu nje wanataka. Linganisha Marekani: kwao bidhaa hizi ni zaidi ya 40%; angalia China kwao ni juu ya 50%. Maana hao wanazalisha vitu vingi ambavyo watu wengi wanatafuta. Ninachukua namba hizi kama dalili ya uwezo ya uchumi."

Mifano yako yote iko ndani ya hizo asilimia 5 (sitaki kubishi ukinionyesha ni 4 au 7) za mauzo yao ya nje nilizotaja ambazo ni bidhaa zilizoongezeka thamani sana. Mengine ni malighafi (~ 50%) na bidhaa sahili kama mabati na feleji nyingine, plastiki, synthetic rubber na kadhalika. Linganisha na China! (wacha Marekani)
Ambayo yote ni maendeleo makubwa nikitazama kwa macho ya Afrika ya Mashariki lakini kwa kweli si top.
Silalamiki chochote. Karibu kunifundisha!
 
Nchi namba 1kwa uzalishaji wa mafuta ni Saud Arabia
Mbili Russia

Nchi zenye akiba kubwa ya mafuta USA namba 1
Mbili Russia


Rekebisha hapo
 
Russia yasema ktk shambulio lake la ngome ya kijeshi Ukraine karibu ya mpaka wa Poland, imeua wapiganaji wa kigeni karibia 180. Pia imeharibu kiasi kikubwa cha silaha zilizotolewa na nchi za nje.

Sasa napata picha, ndio maana Russia ilishambulia kwa makombora zaidi ya 30. Walijua fika kuna wapiganaji wengi na silaha nyingi

 
Wewe ndio unaijuwa vita? Ungekuwa unaelewa japo kidogo wa vita, usingeitaja Afghanistan.

Nikueleweshe tu ili siku nyingine usiandike utumbo; Afghanistan hawaijawahi kushindwa vita yoyoyte na yeyote na haijawahi. Mrusi alipoivamia walipambana nae mpaka akakimbia. Mwaka jana USA na NAYTO wote na wao wameikimbia Afghanistan kwa kichapo walichopewa na Taliban.

Na hao Waarabu uliowaandika ulimaanisha ni kina nani? maana wa Afghanistan sio Waarabu. Duniani Waarabu wengi zaidi kwao ni Afrika, ukisema Waarabu pekee haitoshi, taja nchi uliyomaanisha maana unaonesha hujuwi Mwarabu ni yupi na asiye Mwarabu ni yupi.


Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Msiwe mnajiandikia tu kipumbavu.
 
'ant Majnun
Umejaribu kuandika Kiarabu kwa Kiswahili lakini umekosea sana kwa kua tu hukuielewi Kiarabu wala Kiswahili.

Faidika na darsa la FaizaFoxy, elimu bila khiyana:

Lugha ya Kiarabu kina me na ke katika matamshi na maandiko yake"gender", neno "Ant" uliloweka halipo na halina maana yoyote. Neno "Majnun" lina ) me na ke (gender), "Majnun kwa me na Majnuna kwa ke.

Mzee Abdul Ghafur wa Abraar nilipenda sana usemi wake (aliwahi kuandika humu) "If you have to do something you either do it right or you don't do it at all".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…