Bro una nondo kuntu sema una tuna mahaba bado [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]... Nakufatilia vizuri 75% unazungumza fact 25% unaongeza mahaba...
Anyway so mbaya lakin ni mtizamo wako pia...
Ngoja nikutolee mfano kuna picha zilikuwa zinasambaa wakidai wanajesh wa Russia wanaiba kuku... Ingawa kuna Tani kibao za Humanitarian Aid zinaingia kila kukicha Ukraine kwe majimbo ambayo teari yashachukuliwa....
Hv kama wanalishwa Raia... Au kwamba Russia wana njaa wangepeleka msosi uko?
Sasa ndo kama ww rafiki angu unaitazama Russia kama Zimbabwe. Una nondo konki kichwani ila una mahaba...
Nikuhoji tena... Unaeza kunielezea apo nyuma aliwezaje kushika nafasi ya 11 duniani kwa GDP akiwa na sunction zaidi ya 2700 mgongoni??? Ambapo sa hv ndo vimeongezeka mpk zaidi ya 5400...
Ko utaona au ka huoni bas uku nje me ndo navyokuona... Unachambua vizuri ila unachambua kwa mahaba... Teari akilin mwako una "adui" ambae kwe kila analysis zako unatafuta weakness....
Huezi kuupata uhalisia kwa namna hyo...
Asante kwa hoja. Haya, nikiri: habari za soksi na chupi si kweli. Tukiona picha za wanajeshi Warusi wanaiba chakula (kuku sijaona, lakini video kadhaa jinsi walivyovunja maduka na kuchukua chakula) hapa si maana yake kuna njaa Urusi. Ni dalili kwamba kwenye siku za kwanza jeshi la Kirusi lilipanga vibaya. Ni dhahiri walitegemea kumaliza katika siku chache. Hivyo vikosi kadhaa vilikosa chakula na vifaru viliachwa barabarani kwa sababu dizeli ilikwisha.
Sidhani inatokea leo hii. Yalikuwa makosa ya siku za kwanza. Hii inalingana na habri kwamba Putin alipumzisha majenerali kadhaa na kuwabadilisha.
Kuhusu nafasi ya GDP na sanctions: si vigumu. Ukiwa na akiba kubwa ya gesi na mafuta unayouza unapata namba za GDP. Upande wa tasnia nchi ni dhaifu zaidi. Wana msingi pana, lakini sekta nyingi ni dhaifu sana. Maana tasnia wakati wa ukomunisti ilikuwa kubwa lakini tekinolojia ya nyuma, isipokuwa tekinolojia ya kijeshi kwa sehemu kadhaa.
Kwa nini kuna makampuni mengi ya Ulaya na Marekani ambayo yanaondoka sasa? Je Urusi isingekuwa na makapuni yake yenyewe? - Ukweli ni: kutokana na udhhaifu wa uchumi walikaribisha hao wa nje kuwekeza na kuleta tekinolojia.
Sasa sanctions: Zilianza baada ya uvamizi wa kwanza wa 2014. Lakini hazikuwa kali. Hii takwimu inayotaja namba za sanctions inapotosha kidogo.
Maana nchi yenye vikwazo vikali kwelikweli ni Korea Kaskazini, lakini idadi ya sanctions kwenye takwimu ni ndogo kuliko Urusi. Ambao inaleta picha isiyo halisi.
Idadi ni kubwa ukimjumlisha kila mwanasiasa na kiongozi wa kijeshi anayehesabiwa kama "sanction 1". Pia nchi za Ulaya walitaka kuendelea kufanya biashara na Urusi. Hivyi hapakuwa na santion 1 kwa tasnia ya ndege (jinsi ilivyo Korea kwa ujumla), bali orodha ndefu ya kuzuia hiki (lakini kuacha nafasi kwa biashara ya kitu kingine) na yale, kwa kulenga hapa na pale, si kwa jumla.
Maana makampuni yalitaka kuendelea na biashara.
Hii imebadilika sasa. Ila bado hakuna kikwazo dhidi ya gesi na mafuta kwa Ulaya, kwa sababu huko hawana mbadala hadi sasa.
Kama Putin angetaka kuwapiga Waulaya, angezima SASA gesi na mafuta. Ila tu hii hafanyi KWA SABABU ANAHITAJI KILA SENTI.