Mkuu!kumbe Putin alipanga kumaliza vita mapema (hakutarajia au hakutaka asaidiwe siraha) ila mambo yakaenda tofauti,basi nimekuelewa but kuna wenzako humu jukwaani wanasema oprn inaenda kadili inavyotakiwa na siraha kutoka magharibi haziathiri chechote.pia wanakanusha kuwa Putin hakuweka muda wa kumaliza oprn(wanakanusha pia hakupanga kuimaliza mapema kama unavyosema)
Vita sio ndoni kuwa baada ya round 12 inaisha...hayo mambo itaishalini.kwa sasa hayana maana yoyote....issue ni kwa muda husika unafanya nini..US kakaa Afghanstan 20 yrs, Libya tangu 2011 mpaka leo mwendo mdundo hakueleweki (12 yrs), Syria tangu 2011 mpaka leo hakujakaa sawa..(12 yrs), Chechnya operation (10 yrs), Soviet-Afghanistan ( 10 yrs)...sasa mnata mfanye vita kama mechi ya mpira aisee...tuwaache watwangane tu..
Ukraine anajichelewesha tu kusurrender....hawezi toboa hii vita....na hapo Urusi huko ni kama hakuna vita, watu wanaendelea na life kama kawa...only 3% ya GDP ndo inaendesha hilo songombingo lote, hivi ikitangazwa vita-full mobilization ikafanyika, war economy ikaanzaa kazi Ukraine atasimama kweli.. na kaishachoshwa na Wagner etc..
Ukraine atapoteza kwa maumivu sana....hivi UKRAINE hao Georgia walivyoamua kutulia tu na maisha yanasonga, Moldova yenyewe wanabweka tu.lkn.hawajafanya ujinga kama wa Ukraine..wakujaribu kutunishiana misuli..
US wapo CUBA pale-guantanamo bay..kibabe (Umesikia CUBA wameanzisha operation ya kijeshi kukomboa??)...wanajua kina-chake sio mchezo..
British wanakalia visiwa vya Argentina kusini huko-umesikoa Argentina wamepeleka jeshi kukomboa kwa miaka ya karibuni...Hapana..why?wanajua kitakachowakuta....
CHINA na India wameweka mpaka sheria kwenye sehemu wanayoigombania huko mpakani- hakuna silaha za moto.
mkipigana ni ngumi na fimbo tu...
Viongozi wa UKRAINE hawakua na hawana busara..ilibidi wajifunze nna ya kudeal na jirani yake ambaye ni mbavu zaidi yake..diplomasia...etc lkn kujifanya et wanataka kuzipanga ni upumbavu tu...
Hii dunia vitu vingi watu wanatumia akili tu, sio hisia ..ukiweka hisia unaumia..kama Ukraine