Russia wanaposema hii vita ni hybrid wanamaanisha nin???
Wakisema hivyo wamaanisha kwamba kila aina ya mbinu za kivita zatumiwa na NATO na US hivyo na wao ni lazima wajibu na kuwa sambamba navyo.
Vita vya Hybrid hujumisha matumizi ya mambo yafuatayo:
1. Vifaa vya zamani na vipya vya kivita na ndo maana silaha nyingi kwa upande wa NATO na US zimepungua maghalani kutokana na matumizi mabaya ya majeshi ya Ukraine. Russia watumia silaha zao kwa mpangilio ingawa Prigozhin alikuja kuwa mkali kwa kuona abaniwa lakini ukweli nikwamba Russia atumia silaha zake kwa mahesabu.
2. Information War -yaani vita ya habari yaani nani kasema nini na nani kasema visivyo hivyo kuweka mashindano ya nani habari zake au taarifa zake ndizo zenye uzito.
3. Matumizi ya vikosi vya kukodi ambapo Russia wana Wagner, Ghukas na vikosi vya Chechen wakati NATO na US nao waitumia Ukraine kupigana na Russia kwa niaba yao na pia kutumia vikosi vya kukodi kutoka katika sehemu ya wanajeshi wa zamani na wale wenye ujuzi mbalimbali.
4. Uchumi kwa maana ya kuwekeana vikwazo ambapo NATO na EU na US wameweka vikwazo vya kiuchumi kwa Russia lakini Russia watumia mbinu zingine kuhakikisha uchumi hautetereki kabisa na kusababisha matatizo kwenye nchi.
5. Vita vya mitandaoni (cyber attacks) na adversaries ambapo hivi sasa mitandaoni kuna vita watu washambuliana kwenye mifumo ya computers jambo ambalo halitangazwi ila vita hiyo ipo yaendelea.
6. Matumizi ya mbinu kama mabomu ya kutega kushambulia miundombinu ambapo Ukraine ndie hufanya sana hivi na pia kuua watu muhimu kutoka upande wa adui (assassinations) na kadhalika.
7. Matumizi ya vifaa vya hali ya juu vya kiteknolojia kama UAVs, AI katika kutambua targets na magari ya ardhini ambayo huchimba kuficha mabomu (huitwa VBIED au Vehicle Borne Improvised Device) bila kujulikana na maadui.
Na njia zingine nyingi za kisiasa, kidiplomasia kama vile kumtangaza Putin kuwa ni mhalifu wa kivita ambayo inamfanya mtu kuwa ametengwa au "isolated".
Hivyo NATO na US pamoja na washirika wote walijiandaa kwa aina hii ya vita na pia Russia na washirika wake pia walijiandaa vilivyo kwa miaka 8 tangu 2014.
Haya ni kwa ufupi tu.