Ecowas wamekubaliana kuingia NIGER kijeshi kulinda maslai ya Marekani na NATO. Poor Africa
Hizo ni Beat tu japo kuna presha kubwa sana kutoka kwa West ila hawana huo ubavu, kwanza jamaa wanakwambia watamuua Bazoum kama ECOWAS wataendelea na kimbelembele.
Kupeleka Jeshi ni ngumu sababu Niger wana support ya Wananchi hapa ndo ugumu unapoanzia, wananchi wan hasira sana. Angalia support ya maelfu ya Nigereans ambao walikuwa uwanjani kutoa support .
Hakuna kitu kinachoweza kupambana na Nguvu ya Wananchi. Niger wamesaini na Wagner kwenye masuala ya Ulinzi, sasa sioni Jeshi la ECOWAS ambalo litaweza pambana na hawa watu asee.
West wanataka kuwatumia ECOWAS kwenye kukamilisha misheni yao hawataki kwenda wao direct unafikir kwanini?. Nyuma ya mzozo wa Niger kuna Russia na Niger ndo kete muhimu kwa Russia kwa sasa kama ilivyokuwa kule Syria.
Russia anapambania Maslahi yake pale hakuna Bomba la gas litakalopita Niger wala hakuna jeshi litakaloingia pale.
Walitoa deadline ya week ikapita, afu leo hii waingie thubutu hawana hio jeuri ECOWAS zaidi wanawafurahisha WEST tu.
Huu ni mpango wa Russia uliosukwa kwa muda mrefu usishangae kuona yale mapinduzi yalotokea kwa muda mfupi ukanda ule.
Russia anawabana west kwa njia za kijasusi, kila wanakotaka kwenda kuna Russia wako kwenye PANIC MODE kwa sasa, walichezea sharabu za dubu.
Ingekua Niger haina backup ya Russia sahivi tungekuwa tunaongea mengine hapa. Angalia jinsi Niger wanavojiamini na wanavyo mjibu Nuland kwa kejeli na dharau, angali jinsi wanavyowakatalia ECOWAS nje nje, mwenye akili ameshajua nyuma kuna nani.
Kama mliambiwaga Russia ni dhaifu nadhani mshaanza kupata picha Russia ni nchi gani. Kama intelligence yao imeweza kufanya hayo mambo yote tena kwa muda mfupi na West hawana habari, wanakuja kushtuka kumekucha.
Hata hiyo vita ya Ukraine ilikuwa ni kiini macho tu, West walitegewa mtego wakaingia kichwakichwa. Hata huyo Zelenksyy inawezekana kuna mchezo wanacheza na Putin, maana ukiangalia jinsi ambavyo Russia anaipiga Ukraine kwa huruma sana huwezi fananisha na kule Syria.
Sio kwamba Russia hana huo uwezo naamini kuna agenda ya siri sana ni vita ya kiuchumi. Toka vita ianze mambo mengi yamebadilika sana na Russia walisema formation ya Multipolar world dunia haiwezi kubaki kama Zamani.
Ukiangalia jinsi mambo yanavyokwenda kwa sasa watu wako siriazi na malengo yao ni suala la muda tutaimba wimbo mmoja.