Mkuu mbona unaniangusha ?
Kwa uwelewa wako kwenye masuala ya kijeshi na kimataifa sikutegemea kama ungekuwa una toa hoja dhaifu namna hii.
Hivi mkuu linchi likubwa kama Ukraine kutekwa ndani ya siku mbili ww unaiona nika kazi ndogo?
Marekani na washirika wake walitumia miezi kuingusha Iraq lakini Urusi ni ndani ya masaa 48 wamesha ufikia mji mkuu wa Ukraine, bado tu mkuu hujaona nguvu ya Urusi.
Alafu kingine nilicho gundua kwenye vita hivi Urusi hautumii nguvu kubwa kivile hata makombora anayo tumia ni ya kiwango cha kati na ndio maana hata vifo vya raia sio vingi
Urusi ngekuwa inatumia nguvu zake kisawasawa sasa hivi tungekuwa tunaongelea vifo vya maelfu kwa maelfu ya watu.