Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Huu sasa msala bora wakuje huku Tanzania wasalimishe maisha yao.
 

Vita vya Ukraine: Marekani yatuma kwa siri makombora ya masafa marefu kusaidia Kyiv​


25 Aprili 2024
Na Kathryn Armstrong ,
BBC News

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Ukraine imeanza kutumia makombora ya masafa marefu yaliyotolewa kwa siri na Marekani dhidi ya Urusi, maafisa wa Marekani wamethibitisha.

Silaha hizo zilikuwa sehemu ya msaada wa $300m (£240m) ulioidhinishwa na Rais wa Marekani Joe Biden mwezi Machi na ziliwasili mwezi huu.

Tayari zimetumika angalau mara moja kulenga shabaha za Urusi katika eneo linalokaliwa la Crimea, ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinasema.

Bwana Biden sasa ametia saini kifurushi kipya cha msaada cha $61bn kwa Ukraine.
Hapo awali Marekani iliipatia Ukraine toleo la masafa ya kati la Mifumo ya silaha za Makombora (ATACMS) lakini ilikuwa ikisita kutuma kitu chochote chenye nguvu zaidi, kwa sababu ya wasiwasi wa kuhatarisha utayari wa kijeshi wa Marekani.

Hata hivyo, Bw Biden anasemekana kuidhinisha kwa siri kutuma mfumo wa masafa marefu - ambao unaweza kurusha makombora umbali wa hadi 300km (maili 186) - mnamo Februari.

"Naweza kuthibitisha kwamba Marekani iliipatia Ukraine ATACMS ya masafa marefu kwa maelekezo ya moja kwa moja ya rais," msemaji wa idara ya serikali Vedant Patel alisema.

Marekani "haikutangaza hili mwanzoni ili kudumisha usalama wa oparesheni za vita nchini Ukraine kwa ombi lao", aliongeza.
Haijabainika ni silaha ngapi ambazo tayari zimetumwa, lakini Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan alisema Washington inapanga kutuma zaidi.

"Zitaleta mabadiliko. Lakini kama nilivyosema hapo awali kwenye jukwaa hili... njia rahisi," alisema.

Makombora hayo ya masafa marefu yalitumiwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita kushambulia uwanja wa ndege wa Urusi katika eneo linalokaliwa la Crimea, shirika la habari la Reuters lilimnukuu afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutajwa jina akisema.

Na makombora hayo mapya pia yalitumiwa katika shambulio dhidi ya wanajeshi wa Urusi katika mji wa bandari wa Berdyansk unaokaliwa usiku wa kuamkia Jumanne, kulingana na New York Times.

Miezi ya hivi karibuni imeshuhudia Kyiv ikiongeza wito wake wa kutaka usaidizi wa nchi za Magharibi huku akiba yake ya risasi ikipungua na Urusi ikipata mafanikio ya kutosha.

Kifurushi kipya cha msaada kinafuatia miezi kadhaa ya kukwama huku kukiwa na upinzani wa msaada kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Congress.

"Itafanya Amerika kuwa salama zaidi, itafanya ulimwengu kuwa salama," Bw Biden alisema baada ya kutia saini kuwa sheria.

Akijibu maswali kuhusu kifurushi hicho, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema: "Sasa tutafanya kila kitu kufidia nusu mwaka iliyotumika katika mijadala na mashaka.

"Kile Urusi inachoweza kufanya wakati huu, anachopanga Putin sasa, lazima tumpinge."
Bw Zelensky hivi majuzi alionya kwamba mashambulizi ya Urusi yanatarajiwa katika wiki zijazo baada ya Ukraine kupoteza mji wa Avdiivka wakati wa majira ya baridi.

Vikosi vya Ukraine vimekumbwa na uhaba wa risasi na mifumo ya ulinzi wa anga katika miezi ya hivi karibuni na maafisa wamelaumu kucheleweshwa kwa msaada wa kijeshi kutoka kwa Marekani na washirika wengine wa Magharibi kwa kupoteza maisha na sehemu ya nchi yao.

Bw Sullivan alisema siku ya Jumatano "inawezekana kwa hakika kwamba Urusi inaweza kupata mafanikio zaidi katika wiki zijazo".

Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine tarehe 24 Februari 2022, makumi ya maelfu ya watu, wengi wao wakiwa wanajeshi, wameuawa au kujeruhiwa kwa pande zote mbili na mamilioni ya watu wamekimbia makazi yao.
 
Watazitafutia dawa zake
 
UK imeendelea kuagiza mafuta Russia na Sasa hivi huo uagizaji umeongeza maradufu.


kweli Russia ni kama maji.



View attachment 2973502
Hawa wazungu wa siku hizi,inawezekana ni tofauti na WA zamani.
Ama walikua ni wajinga namna hii toka zamani ila sema sisi tulichelewa kuwajua.
Ama ni wazungu wachache TU ndio waliokua Wana akili zamani, basi sisi tukaona Kila mzungu ana akili.
Mambo na matendo wanayoyafanya ama wanayoyapigania ni ya ajabu sana.
Wewe mtu huwezi kulazimisha haki za binadamu kwa watu wanaoingiliana kinyume na maumbile,Mungu mwenyewe alowanyima haki hiyo na kuamua kuwateteza wao na vizazi vyao.
Ama mfano,vita hii eti mtu analazimisha kujiunga na NATO.sasa unajiuliza NATO Ina faida Gani kiuchumi au kimaendeleo?
Au nchi moja inazilaghai nchi nyingine zijiunge na NATO.ana malengo Gani huyo?
Yaani mtu anaiwekea nchi nyingine vikwazo Hadi vikwazo hivyovinaiathiri nchi mweka vikwazo pia vinaziathiri nyingine,nazo zinaona sawa TU.
Mtu anazunguka Dunia nzima kuomba silaha,lkn sio kutafuta suluhu.
Watu wanakufa nchini kwake yeye kang'ang'ania TU kuomba silaha kwenda kupigana na li nchi ambalo hata hao NATO wenyewe orijino wanaogopa kuingia vitani nalo moja Kwa moja.
Ameona kilichofanyika kwa Israel na Iran,hao hao NATO wanaomsaidia waliweza kumsaidia Israel kudungua silaha za Iran kwa vitendo,lkn hawataki kufanya hivyo kwa Urusi,hapa alitakiwa kujiuliza na kushituka,lkn alivyo kiazi anawalaumu kwa kutomsaidia kama walivyomsaidia israel.
Anashindwa kujua tofauti kati ya Iran na Urusi.
Maangamizi ya Urusi ni makubwa kuliko mfano.
Kwa kifupi ukiangalia kwa undani utaona wazungu ni wajinga mno kuliko tulivyokua tunafikiria.
Wana ushindani wa kijinga mno.
Hebu fikiria,Kuna nchi hawazipendi na sio washirika wao,mfano Korea kaskazini,Iran,Urusi,china,Cuba, Venezuela, Syria n.k
Wao Wana umoja na urafiki wao,lkn hawataki Hawa wasiowapenda wawe na umoja wao.au wasipendane wao Kwa wao.
Utasikia Kila siku USA inaoambia Urusi kua isizichagulie marafiki nchi zilizojitenga na Umoja wa kisovieti,lakini hiyohiyo USA inazunguka Dunia nzima kuziambia nchi marafiki wa damu wa Urusi wasiwe upande wa urusi.cha kichekesho zaid wanazionya hata zile nchi walizoziwekea vikwazo,mfano Iran, Korea kaskazini, Venezuela n.k kwamab zisiisaidie urusi.ajabu sana hii.
 
Duh, mmarekani kweli anajua kufanya biashara! Hapa kaamua kulinda biashara yake a.k.a brand! Ila ametumia njia ya kitoto!

Ukraine moves US tanks away from frontlines after 'hunter-killer drone' attacks​


Ukraine has sidelined US Abrams M1A1 tanks - partly because Russian drones can detect them and launch attacks, two US military officials have said.


Moscow has begun to use more surveillance drones and hunter-killer drones, making it more difficult for Ukraine to protect the tanks.

Five of the 31 Abrams have already been lost to Russian attacks.



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…