LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Hata kwa upande wangu naona kwenye Historia iliyopo wazi kuna uongo mwingi sana. Yes katika wengi nikiwa mmoja wapo sikuepo enzi hizo lakini kile kilicho andikwa na kinachoendelea sasa kinatia mashaka.

Mfano ukiingia wikipedia, kuna hiki kitu kuhusu WWII,


Upande wa allies kuna USSR, USA, UK na CHINA ya enzi hizo. Upande wa axis kuna Germany, Japan na Italy. Imeandikwa kwamba "Allies" ndio walikua washindi baada ya miaka hiyo 6 ya vita.

Sasa ilikuaje allies kama UK, US kuungana na "axis" kama Germany na Italy kutengeneza umoja wa kujihami (NATO) against "allies" mwenzao kwa wakati huo ambae ni USSR?

Hapo hapo tena unajiuliza if really allies kama UK na US walikua wanapigana na Unazi, ikawaje sasa makamanda wa kinazi kukimbilia kwe nchi hizo kujificha baada ya vita?

Nachelea kusema history iliyopo na inayosomwa sana sio halisi tena imejaa pumba sana sio kidogo 🤣🤣🤣.
 
Haya maswali yako yote jibu ni moja tu.

Marekani haitokaa kamwe iruhusu Urusi ajitwalie ushindi na heshima dhidi yake. Urusi nayo vilevile.

Umoja wa NATO uko tayari kuwatoa kafara watu wote ulimwenguni, ikiwezekana, ilimradi ijaribu kujisitiri aibu.

Kauli za Putin nazo haziko mbali na ukweli huo mchungu.

Maana yake ni nini? Tunaelekea kushuhudia mtukuso wa kijeshi (military showdown) wa namna yake ambao haujawahi kutokea kamwe katika historia ya ulimwengu.

Matokeo? Muda wenyewe utazungumza. Lakini ukweli tuujuao yakini ni kwamba kamwe katu hatakuwepo mshindi--si Marekani wala Urusi!
 
inatafakarisha sana.
 
Hakuna kitakacho tokea!
Mzigo wote ataangushiwa Zelensky. Au ili kuficha aibu yao wanweza wakaruhusu Trump apite aokoe jahazi la aibu kwao. Kisha historia itabaki kumlaumu Trump.
 
Adui wa Adui yako??
 
Kutoka Javelin,Himars…..Abrams,Leopold mpaka Atacms..

Hahahahahaa
 
Lina movie inaitwa spy city, inaonesha wote wamepiga kambi berlin wakijasusiana. Je Russia alifikaje kutokea East??
 
Sasa NATO si wafungue hiyo Anga
 
Mkuu mbona Chasiv Yar na Kyiv ni mbali sana?! Una uhakika na ulichoandika?
 
Mkuu mbona Chasiv Yar na Kyiv ni mbali sana?! Una uhakika na ulichoandika?
Hapa bila shaka ameenda chaka.
Kuanguka kwa Chasiv Yar kunafungua njia kwa kumshambulia majiji manne yaliyopo upande wa magharibi wa Chasiv Yar.

Ambayo ni Konstanivka, Dughanivka, Kramatorsk na Slovyansk ambayo iwapo yatakombolewa basi vita ya Donbas itakuwa imefikia mwisho.

Kuanguka kwa Chasiv Yar kutaipa pia Urusi nafasi(access) ya kuweza kuona na kumshambulia chochote kwenye huo upande, kwa sababu Chasiv Yar ipo kwenye muinuko.

Ila sio mbaya Tupo nae pamoja.
Uraaa Uraa Uraaaaaa Uraaa
 
Mkuu mbona Chasiv Yar na Kyiv ni mbali sana?! Una uhakika na ulichoandika?
Ndivyo mkuu wa intelligence katika jeshi la Ukraine anasema hivyo.
Ni mji ambao utampa urahisi Russia kuingia Kyiv, ni ngome iliyokubalika sana hadi Zelensky kuiita haipenyezeki.

Nadhani mahesabu yao hio ngome ikichukuliwa basi hakutakuwa na upinzani mkubwa mbeleni, kumbuka Russia wanachotaka ni kuingia Kyiv.

Kumbuka pia Russia ilishafika hadi km 31 karibu kuingia Kyiv 27 february, siku chache tu vita ilipoanza 2022 Feb 24 hapo ni siku kama 3 tu. Bila NATO Ukraine ai chochote.

Chasiv Yar kuwa chini ya Russia ni kurahisisha Russia kuifikia Kyiv kwa urahisi. Usiangalie umbali kwenye ramani bali ni ngome ngumu kupenyezeka. Kumbuka jeshi la Russia kwa kutoa kichapo na kusonga mbele wapo faster, hawana kuremba. Huo umbali wa kawaida tu, kama walitoka Russia hadi karibu na Kyiv kwa siku 3 hapo ni mbali?

Kama walimpiga mjerumani peke yao kutoka mashariki wakafika wa kwanza Berlin unafikiri ni mchezo.
 
Hakuna kitakacho tokea!
Mzigo wote ataangushiwa Zelensky. Au ili kuficha aibu yao wanweza wakaruhusu Trump apite aokoe jahazi la aibu kwao. Kisha historia itabaki kumlaumu Trump.
Watu wanaofanya maamuzi juu ya vita vya Ukreni vs Urusi ni walewale wa majanda ya juu (people from high places).

Wengi watashangaa kujua kwamba malengo yao, ingawa watu hao wako pande mbili zinazohasimiana, ni yaleyale.

Dunia inaelekea katika mfumo wa siasa, jeshi, uchumi na jamii ambao utaamua mapinduzi mapya na tofauti kabisa katika maisha ya mwanadamu.

Ni kana kwamba wakuu hao kutoka pande hasimu wako kwenye kiapo cha kufikia lengo lilelile moja licha ya njia, mbinu na mwonekano unaoweza kukinzana baina yao.

Ni vigumu kuamini kwamba hao ^wachezeshaji^ wakuu wa harakati hizi za siasa za kimataifa hawako katika namna fulani ya masikilizano ambayo yumkini hayafahamiki kwa kundi kubwa la daraja la chini.
 
DEMOKRASIA NI NINI?
JE DEMOKRASIA NDIO MFUMO SAHIHI KULIKO MIFUMO MINGINE?
NINI FAIDA NA HASARA ZA DEMOKRASIA?
DEMOKRASIA ILIANZIA WAPI? (Ugiriki)
JE MAENDELEO NI NINI?
JE KUNA UHUSIANO CHANYA AMA HASI WA DEMOKRASIA NA MAENDELEO? (TOA MIFANO 5 KWA HASI NA 5 KWA CHANYA)
TAJA NCHI 5 ZIFATAZO DEMOKRASIA NA ZINA MAENDELEO
TAJA NCHI 5 ZISIZOFATA DEMOKRASIA NA ZINA MAENDELEO
TAJA NCHI 5 ZIFATAZO DEMOKRASIA NA HAZINA MAENDELEO
TAJA NCHI 5 ZISIZOFATA DEMOKRASIA NA HAZINA MAENDELEO
TAJA MIFUMO MINGINE TOFAUTI NA DEMOKRASIA


View: https://x.com/FunnyWorld1313/status/1786718147644649851
 
Sahizi wameamua kuingiza wagonjwa kabisa 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…