Hii vita kwa Mrusi ni ndogo sana. Ikiwa kama tukifanya marejeo utagundua kuwa mambo mengi Russia ya Putin wanayafanya kwa mbinu. Mbinu ni tofauti na sera. Ndiyo maana kwa wamagharibi Putin kwao wanamuona hatabiriki.
Tukubali au tukatae, vyombo vya habari kwa sasa ni silaha kwa nchi husika. Kila mahali kuna propaganda. Vyombo vya magharibi navyo vina malengo yake na vyombo vya kwao vya habari vinasukuma propaganda zao. Tukija kwa Russia, China nako ni vivyo hivyo isipokuwa zinatofautiana uzito kulingana na maslahi ya nchi husika.
Russia na Marekani zimekuwa zikipambana kwenye nyanja za kijeshi na kijasusi kwa muda mrefu. Kwa miaka mingi, tena inawezekana ikazidi miaka yangu na miaka yako. Tujiulize: Pengine sisi tunafikiria hivi je, Russia kwao itakuwaje?
Russia kwake alitangaza kama special military operation. Ni kama sisi Tz kipindi cha JK tulivyokuwa na Operation dhidi ya M23 iliyoitwa Operation Chakaza nchini Kongo. Russia naye ametangaza operation yake kwa Ukraine ikiwa na lengo la denazify na demilitarize jeshi la Ukraine.
Ikiwa hilo ndilo alilolisema inabidi turudi na kufuatilia mwenendo wa mashambulizi anayoyafanya Russia nchini Ukraine. Je, yanaendana na alichokisema? Kama yanaendana yanaendana ni kwa asilimia ngapi amefanikiwa? Na ikiwa ni kinyume chake ni kwa asilimia ngapi amekwama? Haya nayaandika hivi kwasababu ndiyo taarifa aliyoitoa Putin kuhutubia Taifa lake.
Putin alinusurika kufanyiwa assassination mara 5 tangu aliposhika madaraka Russia. Alipokwenda kumtembelea Fidel Castro, Castro akamuuliza kwa nini unajua nipo hai mpaka hivi sasa? Castro akajibu mwenyewe akamwambia ni kwa sababu usalama wangu unaanzia na mimi kwanza. Hivyo Putin licha ya kuwaamini walinzi wake ila usalama wake unaanzia na yeye kwanza ijapokuwa anaiamini sana timu ya ulinzi wa kwake. Alishawahi kuwa director wa FSB ambao ni ya kijasusi pia.
Nikimwangalia Putin naona mission zake anazipeleka mbinu za kijasusi na inakuwa ngumu kutabiri. Tofauti na wamagharibi wanatumia sera katika utekelezaji wa mipango yao hivyo inakuwa ni rahisi kutambua mustakabali wa maamuzi watakayoyafanya.
Kingine: Wachangiaji wengi tunachangia hili suala ilihali hatujui nguvu ya silaha zinazotumika kwenye huu mtifuano. Wachangiaji wengi wanazungumzia kwa kile walichokifahamu kupitia google. Ufahamu wake wa silaha unabaki kinadharia. Ila ukija ulingoni hafahamu. Akitokea atakayewaelewesha wanakuwa bado wabishani. Hivyo kwenye hii idara inabidi tuiache hivyo kwa sababu ya kanuni na nidhamu ya wabongo; tuna ujuaji mwingi.