LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Ndugu zangu Pro Russia na Pro Hali,naona mmepanik mno kwa sababu mmezoea ushindi Kila siku.
Kama Kila siku tunavyoongea humu Kila siku kua vita hii sio baina ya Ukraine na Urusi,Bali ni kati ya Urusi na NATO.
Mpaka hapa Urusi ipewe heshima
yake.
Unajua nchi moja kupigana na nchi zote hizo sio jambo Dogo,Tena nchi zenyewe ni nchi za west,ambazo ni tajiri na ze tech ya Hali ya juu sana.

Amin nawaambieni kwa wale ambao mnamuona Putin kama mpole mtakuja kumuona kama mtu muuzaji na katili mno.
Vita ni piga nikupige,wakati wa Urusi wa kutumia nguvu kubwa na kupiga pigo kubwa kwa adui ilikua bado haujafika,nadhani Sasa umefika na tutegemee kuona kile watu mnachotaka.
Watu tunatofautiana kwa busara,Putin anaonesha busara ya Hali ya juu mno,na busara yake inaepusha vita vya Tatu vya Dunia na vita vya kinyukilia.
Nadhani wote mnakubali kua Urusi Ina silaha za maangamizi lkn mmashangaa ni Kwa Nini hataki kuzitumia.
Kila kitu kinaenda kwa hatua,kama angetumia hizo nguvu mnazozitaka mwanzo Kuna wengine mgesema Urusi imezidiwa na Ukraine Hadi imetumia silaha kubwa.
Naamini Urusi itatoa jibu ambalo wote mtabadili hasira zenu.
Hata hivyo hicho walichofanya Ukraine hakita rudisha majimbo yaliyochukuliwa Bali ni kulazimisha Urusi ipige moja kwa moja kwenye nchi za NATO ili Sasa iwe (rasmi) vita baina ya NATO na Urusi,RASMI.
Na Hali hii ikitokea Ukraine wanadhani ndio itakua nafuu kwao ingawa kiukweli Ukraine inaweza ikapotea kabisa.
Ndugu zangu naunga mkono busara za Putin ambazo Kuna baadhi ya Viongozi wa USA wako na busara kama zake,mfano ni Trump.
Vita ya nyukilia sio nzuri jamani.
 
Putin akiajribu nuclear atakuwa mtu alieua watu wengi zaidi duniani.

Marekani juzi ametoa ruhusa
Baada ya saa 24 makombora yametumika.
Na baada ya saa 24 wametoa tahadhari kqa raia wao.
Na ubalozi unatarajia kufungwa Kyiv
 
Tusimlaumu Putin kuwa hachukui maamuzi Mazito. Huenda nguvu na uwezo wa kijeshi tuliokuwa tunaamini kwa Russia, huenda ni tofauti kabisa. Russia inapigika kama Iran tu
Kwa maelezo Yako haya halafu ndio unajiona mchambuzi mwenye akili kuliko wotehumu jukwaani.
Aisee kweli wabongo noma.
Kwamba Urusi inapigika kama Iran.
Sasa Urusi inapigika na nani?
Inapigwa na Ukraine?
Inapigwa na USA?
Inapigwa na NATO?
Ama all collective west?
 
Ni mapema mno kumuona Afande Putin kama mtu dhaifu
Subirini majibu ya hicho kilichotokea.
 
Sijawahi comment humu.

Hii ndio comment yangu ya kwanza nasema Putin ni mtulivu na mvumilivu juu ya maamuzi yake ukizingatia uhatari wa silaha wanazo miliki Russia na ukubwa wa Taifa lao.

Ni sawa na kusema Xi ni dhaifu kwa sababu hakupeka jeshi 2019 Hong-Kong au apeleki majeshi Taiwan.

Kuwa viongozi katika haya mataifa utulivu ni wa muhimu pasipo kujali maamuzi yako uliyochukua awali yalikuwa sahihi au si sahihi Russia ipo vitani na vita bila utulivu ni hasara pia.

Putin ni mtulivu anaweka hesabu zake sawa kama wao wanamdharau hayo ni matatizo yao japo sidhani sana kama wanamdharau Putin.

Kitu anachofanya Israel ya Netanyahu Russia ya Putin wanaweza kifanya hata mara kumi yake lakini je, ipo tayari kupokea matokeo ya maamuzi yake kwa marafiki zake,majirani zake na dunia kwa ujumla ?
 
Asante kaka, hawajui hii ni vita, sio mashindano ya unenguaji kiuno ndio useme utashinda wakati ujao. Mastermind putin anajua anachokifanya, Ila ataeleweka. Kwangu mm ni shujaa, living god among men. Kupigana vita inayohusisha the most advanced weapons in terms of tech sio kitu kidogo. All after all, ninaweza kusema mpaka sasa putin n jeshi lake wameonyesha exemplary ability in the fields of war. Kwann nasema hivi, Ukraine anarudishwa nyuma Kila kukicha, maeneo yake na wananchi wake wanabinafsishwa n gov ya Russia. So sio silaha tu, bali hata wanajeshi wa nato wanaoipigania Ukraine wote wameonyesha incompetence kwa kushindwa kumzuia putin kuchukua ardhi ya Ukraine Kila kukicha. Pia wametuonyesha the real power ya Russia, imagine bado hajaanza kutumia hata ballistic missiles with nuclear war heads, potezea strategic nuclear bombs like black Satan 2. Hii vita bado haijaanza, Ila mrusi akisema iishe, hata muamerica hatokuwa na ubavu wa kumtusi putin. Kwann, mrusi akimaliza vita na Ukraine kwa kumpa a historical kipigo, kama nchi yeyote ya itatokea kumshambulia Russia, basi sio Russia tu, Ila nchi zote za nato au ulaya kwa ujumla zitakuwa reduced into ashes. Russia ikifa, hakuna taifa la nato litabaki stamding
 
Ila pia Kuna mwamba alikuwa anaitwa Joseph Stalin.....

Huyu rais wa Russia alikuwa ni hatari
 
Maamuzi gani magumu unayotaka Russia afanye ?
 
Putin kama hataonyesha msimamo wa maneno yake kwenye hili RUSSIA itapoteza ushawishi wake ulimwenguni,
Dunia ilitarajia Russia kubalance mzani wa ubabe.
Kauli zimekua nyingi kuliko vitendo.
Mkishakuwa kwenye vita hamna busara,,,
Hakunaga urafiki kwa adui

Dunia nzima inaifatilia hii vita
Kama kutakuwa kimya na maneno mengi Putin atathibitisha HE IS NOT A SOVIET MATERIAL
 
Ulitaka Putin afanye nini toa option ?
 
Nakubaliana na wewe.
 
Inauma sana kiukweli sisi ambao tupo upande wake
 
Uko sahihi kabisa Mkuu
Watu wanataka Urusi ifanye maamuzi kwa mihemko.
Hata hapo ilipofikia imeonesha uwezo mkubwa sana.
Wao wanataka waone Urusi inapigana TU lkn hawataki kuona Urusi inapigwa wakati nchi moja inapigana na nchi zenye majeshi yenye nguvu zaidi duniani.
 
Inauma sana kiukweli sisi ambao tupo upande wake
Ndugu yangu ungekua unajua huko USA watu wametaharuki kiasi Gani na kuchukizwa na uamuzi wa Biden usingeumia kiasi hiki.
Watu huko USA wanahofu na vita vya nyukilia,angalia TikTok watu wanjipost
na kumlaumu Biden kwamba anataka kuwaachia janga au vyombo vingine vya habari,nimeona Kuna seneta mmoja pia anamlaumu Biden.
Kwa kifupi ni kwamba Urusi anaweza kupiga Kambi za NATO,je ni Nini litafuata?
Kama Biden Hana busara sio Putin Hana busara.
 
Hizo silaha hawawezi kumpatia hakuna taifa linaloweza kufanya ujinga huo.

Hayo maamuzi yanahitaji kiongozi kichaa asiyejali hata watu wake nyumbani
Tafuta taarifa za nyuma za kwenye hii SMO uone kwa nini Russia ilizindua kombora la nuclear aina ya samart. Linafikia UK kwa dakika 2 kwa lengo la kukitishia hiko kisiwa.

Marekani na wenzake kipindi cha cold War waliandaa atomic bombs takribani 200 kuishambulia Russia.

Russia iliwawahi kufanya jaribio la bomu lao wakaona mwenzetu analo lenye uwezo kuliko la kwetu ndipo wakarudisha nyuma mipango yao.

Miaka ya 90 Russia ilikuwa dhaifu sana kiuchumi. Ripoti za FSB zinaonyesha Marekani alifadhili wanamgambo ya Chechnia kudai uhuru wa kuwa nchi kamili inayojitegemea ili kujimega kutoka Russia.

Lengo lilikuwa ni kuimega Russia mdogo mdogo ili iwe nchi ndogo watakayoweza kuidhibiti kiurahisi.

Hao watu wapo serious kwa wanayoyafanya.
 
Mimi sichambui kimahaba kama nyie. Tatizo lenu hamtaki mawazo yanayoshusha upande mnaoupenda.
Elewa tu kuwa Russia inaanguka
 
Hao Hao wazungu wenzake ndio waliowezesha zilaha za kiatomiki kutoka Ukraine kwenda Urusi.

Maamuzi ya Ukraine kupatiwa silaha za kiatomiki na taifa lolote litakalo chukua maamuzi hayo labda libahatike kupata kiongozi kichaa na idara nyingine za kitaifa ziwe zimeminywa na nguvu yake.

Sio rahisi maamuzi hayo kuchukuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…