LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Maamuzi gani magumu unayotaka Russia afanye ?
Putin asimamie kauli zake!

Alionya juu ya hili kutotokea! Na alielezea utaratibu mzima wa jinsi hayo makombora yanavyofanya kazi! Kwa ufupi yatakuwa controlled na Nato.

Na aliweka wazi msimamo wa Russia utakuwa ni nini! Wenzake wamethubutu!

Asimamie kauli yake. Tunamsubiri!
 
Nitarejea baadae nikipata muda nitakushitua.

Napenda mijadala ya utilulivu kama hii.
 
Mimi sichambui kimahaba kama nyie. Tatizo lenu hamtaki mawazo yanayoshusha upande mnaoupenda.
Elewa tu kuwa Russia inaanguka
Wewe nani kakupa kipimo Cha kujua huyu anachambua kimahaba na huyu hachambui kimahaba,?
Kumbuka Kila mtu anachambua kwa uelewa wake.
Wewe unachotakiwa kufanya ni kuheshimu maoni ya watu kisha na wewe leta maoni Yako.
Je na Mimi nikisema na wewe unachambua kimahaba utakataa?
Sasa hebu ona unasema Urusi inaanguka kwa sababu ya mabomu sista TU?
Je Urusi ikijibu kwa mabomu 12 utasemaje?
Urusi inateka miji ya Ukraine Kila siku,inaangukaje?
Kama ni uchumi wote tumeona pamoja na kuwekewa vikwazo vyote lkn Urusi imo kwenye nchi 5 zenye uchumi Bora duniani inaanguka kivipo?
 
Hao Hao wazungu wenzake ndio waliowezesha zilaha za kiatomiki kutoka Ukraine kwenda Urusi.
Kufanya hivyo si kama walipenda!

Bali Marekani aliona slavic nation jengine litakuwa powerful kwa kuwa linamiliki nuclear bombs. Tayari ana Russia akiongezeka Ukraine itakuwa ni hatari kwake. Wakaamua kufanya maamuzi hayo!
Maamuzi ya Ukraine kupatiwa silaha za kiatomiki na taifa lolote litakalo chukua maamuzi hayo labda libahatike kupata kiongozi kichaa na idara nyingine za kitaifa ziwe zimeminywa na nguvu yake.
Tafuta ripoti humu zipo kati kati ya hii SMO nchi ya UK ilitaka iwapatie kwa siri Ukraine TNW (tactical nuclear weapon) na mpango kabambe ulikuwa umeshaandalowa ila makachero wa Russia wakazipata hizo taarifa.
 
Wale jamaa Walitaka Huyu Kenge Auwawe mapema sana Ua wakina budanov wote wale halafu aje mtu mwingine akijua hali ni mbaya...Mbona hao USA walimuua Gadafi hata Sadmu huseni?? HUWEZI kujiita mkubwa huku huna lolote zaidi ya mikwara!! KUMBW WAMEMGUNDUA dhaifu watampiga.
 
Putin ni mtulivu anaweka hesabu zake sawa kama wao wanamdharau hayo ni matatizo yao japo sidhani sana kama wanamdharau Putin.
Hii ndiyo sifa yake kuu,utulivu! Jamaa amemuelezea Putin kwenye ule uasi kama ifuatavyo:

Rosenberg: Putin's military purge echoes Prigozhin's call to act​


Remember Yevgeny Prigozhin? A year ago the leader of the Wagner mercenary group had publicly criticised military chiefs.

And this tells us something about Vladimir Putin. The Russian president is averse to acting under pressure. Order him to sack a minister or an army general, and he’s unlikely to agree to it then and there. He won’t be told what to do.

That doesn’t mean Mr Putin won’t act. At a time of his choosing.


Nb:Huwezi kupata huu utulivu kama hujapata mafunzo maalumu.Mfano utulivu wa marehemu Magufuli ni tofauti na Kikwete, coz mmoja ana mafunzo ya kutulia wakati wa tatizo!
 
Basi maana alisema Ukraine haitumii haya Makombora, haina Uwezo wala Watalamu wa kuyatumia!!! Akasema pia Satellite za kusoma GPS za Location ni zao USA hivyo Kama Ukraine itahusika ni kubonyeza Button tu sasa kama ndio hivyo na bado kapigwa anasubiria nini??? Lakini mm naona Hajasema lolote tangu haya mambo yatokee nasubiria mpaka kesho nione!!! UKWELI ni kwamba hii ni dharau na kama Russia hatachukua maamuzi magumu sana hapa anapotea na atasambaratika!!
 
Ukweli wengi wetu tunaona Putin anatuangusha kwa sababu tulitarajia kuiona kiev ikiwa kama Allepo au gaza. Au kufanywa kama kile wanachofanywa lebanon na mazayuni kule kusini mwa beirut.
Putin kwa kitendo cha ukrain kushambulia kwa makombora ya masafa marefu ndani ya russia ilibidi majibu yake yawe makali na mara 100 zaidi. Kama walirusha makombora 6 kiev ipigwe kwa makombora 100+ hii itawafanya waogope kurudia huu usenge waliofanya.
Ila Putin anatuangusha sana
 
Wachambuzi wengi wa masuala ya kivita walikuwa wanajiuliza Russia hii SMO yake ataimaliza vipi!

Wamagharibi wamevunja agreements zote walizoingia na Russia since 1992 kuhusu kupanuka kwa Nato mpaka Minsk Agreements.

Chancellor wa Ujerumani aliyepita alishasema Minsk agreement lengo lilikuwa ni ku buy time ili Ukraine ijizatiti vya kutosha kupambana na Russia. Hilo ndiyo lengo, wala lengo halikuwa kutii makubaliano ya mkataba.

Wachambuzi wa kivita wanajiuliza na jinsi OP inavyokwenda ni ngumu kwa Russia kumaliza kwa namna anayoiona yeye inafaa ya mkataba. Akitoka Trump ni nini kitafuata.

Mustakabali wao uka base kwenye nukta 2: Imma Russia apige tactical nuclear bomb iwakate kabisa Ukraine maini na waache kufikiria kabisa kunyanyua tena silaha kuendeleza mapigano ambayo mpaka sasa bado yanaendelea.

Au achakaze Ukraine iwe kama Gaza. Athari hiyo itabaki Ukraine kizazi na kizazi kama athari ya Russia dhidi ya Germany ya manazi. Kwa namna hii itamfanya Ukraine aiogope vita na aishi na jirani yake bila ya kukurupuka.

Hizo ndiyo njia pekee Russia itakayoweza kuifanya Ukraine isiendelee kubeba silaha.

Yeye anamsubiria Trump! Haya Trump akitoka na wamagharibi wenyewe hawaheshimu mikataba utafanya nini?

Yeye ametulia kwenye kiti, ijapokuwa wanachukua maeneo ila hasara kama za vifo kwa wanajeshi haziepukiki!
 
Ushabiki ukizidi sana..! Mwishowe hujengeka ujinga kwenye vicha hivyo!

Umeanza kuwa mjinga chief

Umesahau maksudiii kwamba, USA siyo Ukraine na kwamba, USA ni zaidi ya ULAYA au ndio huo ujinga?
 
Muda mwengine ukubwa lazima uwe katili, lazima uwe na maamuzi magumu ambayo yatakuwa faida kwa wengi!

China bhana ni wapole! Ila ukizinguana nao wakiamua kupigana hawajali haki za bindamu.

Sometimes uwe hivyo ili ili uweke nidhamu.
 
Hakuna chochote Russia itakachokifanya zaidi:

1) Atashambulia vyanzo vya nishati ya umeme na maghala ya silaha Ukraine (ambayo haya ni kawaida kwake kufanya hivyo)
2) Putin ata sign doctrine nyengine ya nuclear
3)Putina atatoa onyo
4)Putin atawataka kitengo cha nuclear kufanya mazoezi ya utayari wa kivita.

Baada ya hapo ataonya tena! Na baada ya hapo tavielezea vyombo vya habari kuwa Nato inataka kuharibu amani ya dunia.

Hakuna kingine zaidi atakachokifanya zaidi ya hayo! Amezidiwa hata na Ayatollah bhana!
 
Ngoja
Sana sana tunashangaa kwanini hajaachia Dude????
Tuone ila kama atakaa kimya pasi na kutuma dude japo moja la maana tutakuwa wanyonge hilo lipo wazi kabisa japo wenzetu wa upande huu wanaona kama hatuna subra lakin Dunia inaona kuwa Vladimir Putin anakuwa slow hata kwenye kuhatarisha usalama wa raia wake
 
Hammaz,
Unaweza ukawa sahihi ila kwa Hali niliyoiona ktk mkutano wa E.U ni kama vile Ulaya nzima haijui Trump anakuja na jambo gani kuhusu Ukraine January. NATO top leaders wanasema wanasubiri January kuamua hatmanya Ukraine. Biden anajua anatoka hivyo anarusha mateke yake ya mwisho ya kujimwamba fai kwa Putin kwa kuruhusu mabomu ya masafa marefu kutumika ili baadaye Democrat waseme at least they tried something.
Putin siyo mjinga kuna kitu anasikilizia. Nafkiri hajafanya mazungumzo na Trump kujua mwelekeo wake. Naona ana bet na upepo unavyoelekea. Ngoja tuone atakuja na nini kujibu shambulio hilo la US/Ukraine
 
Tusimlaumu Putin kuwa hachukui maamuzi Mazito. Huenda nguvu na uwezo wa kijeshi tuliokuwa tunaamini kwa Russia, huenda ni tofauti kabisa. Russia inapigika kama Iran tu
Hamjui hii vita inapiganwa sehemu nyingi.Bado kuna asilimia kubwa ya raia wa Ukraine ni pro Russia na kwa usalama endelevu Russia anahitaji kundi hili kuwepo na ikiwezekan kuongoza Post war Ukraine.Hii ni sababu ni ngumu kufanya kwa Ukraine ayafanyayo Netanyahu kwa GAZA na LEBANON.Halafu mambo hayafanywi kwa mihemko,bila kuwa na strategy leo hii uchumi wa EU usingeyumba kiasi hiki ili ni somo ambalo wamepewa EU na NATO kuwa RUSSIA sio Sudan.Kuna response itakuja kuhusu matumizi ya hizi silaha alizojaribu kutumia Ukraine unsuccessfully so far.Kawaida ya PUTIN anajibu kwenye uwanja wa vita na pia atawajibu kwenye maeneo mengine ambayao US na NATO wana interest.Suburini watakavyokuja kulia na kulaani kuwa RUSSIA anahatarisha amani ya dunia.Be patient this is a game of chase.
 
Inauma sana kiukweli sisi ambao tupo upande wake
Tukubali tukatae, Putin ni dhaifu.

Mwaka 1971 India ilikuwa inavamiwa kijeshi na USA akiwa na mixed allied force.

USA alipeleka 10 ship naval task, the US task force 74. US alienda na carrier yake ambayo ilikuwa the largest nuclear powered carrier in the world with 70 fighter Aircraft.

Muda huo huo UK akapeleka aircraft carrier yake naye!

India wakaenda kuomba msaada Russia!

Russia ikatuma nuclear armed ships na atomic submarines zenye uwezo wa kushambulia umbali usiyopungua 300km.

Ili Russia iweze ku counter meli za kijeshi na carrier za UK na USA, Russia ikafanya jambo la hatari la kujitoa kafara. Wakawazunguka wote ili wawaweke kati kati within their target na wakafanikiwa.

UK na USA wanafika wanakutana mbele na melinza kivita na nyambizi ya Russia ipo mbele!

Wakaamua kugeuza na kuacha kuivamia India.

Russia hii iliyojengwa ndiyo ikawafanya wamagharibi wawe wanafikiri kabla ya kutenda pindi Russia awepo!

Putin huyu hii Russia ya namna hii angeiweza? Sidhani! Kinachombeba anatembelea historia ya wenzake ndiyo inayompa umwamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…