Wewe member hua ni mgumu sana kuelewa halafu mwepesi wa kusahau.
Nimesema hivi,USA na NATO waache kuirushia mawe Urusi wakiwa nyuma ya Ukraine.
Nikaendelea kusema sio tabia ya USA na NATO kuisaidia nchi kijeshi kwa kuipa misaada bila wao kuingia mazima kama walivyofanya Iraq, Yugoslavia, Afghanistan na Libya.
Hapa nilikua nikilenga wanajifanya kumpa Ukraine silaha lakini wao ndio wanaziopareti.
Nikaongeza kusema wanapigana na Urusi kiujanjaujanja,hii sio tabia Yao na inaonekana udhaifu wao.
Nilimaanisha kua Hali hii inainyima Urusi uhalali wa kujibu mapigo moja kwa moja Kwa nchi yoyote inayorusha jiwe Urusi ikiwa nyuma ya Ukraine,sio nchi tu,hata NATO wote.
Kwa hiyo sio rahisi kwa Urusi kurusha jiwe Kwa NATO.
Ila kama unaona Urusi inaiogopa NATO basi omba Mungu NATO waingize jeshi lao kama walivyoingiza Iraq au Afghanistan au Yugoslavia halafu uone kama Urusi atajibu ama hatajibu.