Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 7,091
- 15,519
Niwe mkweli! Kwa sasa hata sielewi Russia anafanya nini?Russia imeshindwa kuyachukuwa kwa 100% yale majimbo ma4 yaliyofanya referrundum kuwa upande wa russia.
Kila siku tunaletewa story za kukomboa vijiji na vitongoji.
MAisha yakoje kwenye hayo majimbo?
Lavrov kwenye interview yake na Tucker Carlson naona naye alikuwa anajitetea tu! Mara ooh watu wanasema mistari mekundu yote Russia aliyoiweka Nato wameivuka, anajinasua anasema tumetuma ujumbe, na ujumbe wetu mpaka sasa umeeleweka.
Ujumbe wenyewe ni ile missile mpya waliyoitumia dhidi ya Ukraine.
Tuwe wa kweli, maamuzi ya Putin yanawàweka Russia kwenye wakati mgumu sana wa kiusalama duniani. Tena sana!
Wamagharibi wapo serious na wanachokipambania, Putin anajifanya ana hekima.
Kwa sasa wapo wakati mgumu sana kiusalama. Wamagharibi wamemwanzishia vuguvugu jengine mlangoni kwake Georgia. Sijui kama ataweza kupigana vita mbili kwa wakati mmoja.
Na Georgia pakinuka ni lazima apeleke idadi si chini ya laki jeshi lake huko kwa sababu kipindi cha Bush alipeleka wanajeshi takribani elfu 60 naaa!
Putin anajifanya master mind, wenzake wanatanua wigo wa kulishughulisha jeshi lake.
Putin kuna mahali anafeli sana! Ijapokuwa watu humu watakataa kwa mapenzi waliyonayo kwa Russia, lakini tufike mahali tùkubali ukweli; Usalama wa Russia kwa hali anayokwenda nayo Putin atautia hatiani.
Itazame movie ya 13 days uone wamarekani walivyo haha baada ya Russia kupeleka nukes zake Cuba baada ya yeye kupeleka zake Turkey.