Propaganda, propaganda, propaganda.
Humu jukwaani na nje ya jukwaa hili kumejaa propaganda nyingi sana Sasa hivi hususan kutoka kwa Pro UkraiNATO.
Sijui ni aina ya kujifariji ama kutokukubali Hali Hali ya uwanja wa mapambano au ni kuishiwa uwezo wa kupambana mambo.
Propaganda zao utawasikia wakisema hivi,
"Masikini Putin",
"Urusi imeshalegea",
"Urusi ilifanya kosa kivamia Ukraine",
"Urusi vita hii imekwama",
N.k.
Sasa kwa sisi ambao tunafatilia kwa kuangalia uhalisia "facts" tunabaki tunashangaa!
Hivi kama Hali ni mbaya namna hiyo kwa Urusi mbona Sasa hivi inasemekana Warusi ndio wanasonga mbele kwa Kasi ya upepo?
Zaidi tunasikia kua Ukraine wanapoteza maeneo kwa Kasi mno?
Najiuliza hivi kama Urusi Ina Hali ngumu,mbona hatusikii Urusi kunyang'anywa hata wilaya moja iliyokua imeishikiria?
Acheni Propaganda jamani Hali ya Ukraine ni mbaya kuliko mwaka 2022.
wataalamu wanasema bado kidogo TU jeshi la Ukraine lita collapse,
Wataalamu wanasema bado kidogo TU Donbas inaenda kuanguka yote kwenye mikono ya jeshi imara kabisa hapa duniani la Urusi.
Fatilieni vianzo vya habari huru,na Sasa hivi hata vyombo vya west vimeanza kusema haya na kusema ukweli.
Jamani eeeh hii ni SMO kwa upande wa Urusi lkn ni vita ya ku survive kwa upande wa Ukraine.
Ukraine imezidiwa,imekweisha Haina hata wanajeshi imeishiwa wanajeshi,imeandikisha watu wazima,wakaisha,ikaandikisha wavulana kuanzia miaka 18 wakaisha,Sasa inafikiria kuandikisha watoto kuanzia miaka 14.
Huu si uuaji huu?
Haya ninayoyasema ni Hali halisi.
Jamani eeeh Ukraine Kwa kusaidiwa na NATO inarusha makombora ndani ya Urusi mengi yanadunguliwa machache sana Tena sana yanapenya,hata hivyo Hali hii haioneshi udhaifu wa Urusi na kibaya zaidi hayabadilishi kabisa mafanikio ya vita anayoyapata Urusi huko uwanja wa vita,tofauti kabisa na makombora anayorusha Urusi ndani ya Ukraine,makombora ya Urusi yanaidhoofisha kabisa Ukraine Kwa kikindi hiki ambacho vita inaendelea,yanalipunguzia nguvu kwa kiwango kikubwa sana jeshi la Ukraine kuweza kujitetea.
Kuua kamanda au makamanda wa jeshi la Urusi Tena wasio katika uwanja wa mapambano haibadilishi mafanikio ya vita aliyoyapata Urusi.
Kwana kuua kwa njia za kigaidi ni dalili za kua ndani ya uwanja wa vita mmezidiwa.
Kulenga na kuua wakuu wa kijeshi au wa kisiasa Kila upande unaweza,kama mnakumbuka Putin aliwahi kusema msitulazimishe tukapiga kwenye Decision making Centers za Viongozi wa Ukraine,na kama mnakumbuka Kuna siku kulikua Kuna mkutano wa kuwapa nishani wanajeshi wa Ukraine,alikuwepo Zelensky na kiongozi mmoja wa nchi ya west nimemsahau,Urusi walipiga kombora umbali mdogo TU kutokea sehemu palipokua na sherehe hiyo,Hiyo ilikua ni onyo kwamba tukitaka kumuua zelensky hatushindwi.
Lkn pia kama mtakumbuka Waziri Mkuu Msataafu wa Israel bwana Bennett Naftali alipokua akiongea na Putin alimsihi na kumuomba Putin asimuue Zelensky,Putin akakubali ombi hilo, Naftali akamwambi nihakikishie hutamuua.
Poa nakumbuka kauli ya Putin aliwahi kusema tunajua anapolala Zelensky na anapoamkia,hatutaki kumuua lkn tukitaka tuanaweza kumuua,ila hatutamuua ili aje aweke sahihi makubaliano baada ya kushindwa vita.
Ndugu zangu wapo mnaoona Urusi inachukua mda mrefu kumaliza vita,ila nyie Pro Russia na hata Pro UkraiNATO nadhani mnajua Ukraine peke yake asingefika Leo hii,Bali kwa msaada ya NATO amefika lakini akiwa amechoka balaa.
Sasa hivi ninavyoandika hapa zile silaha zote alizokua nazo Ukraine kabla ya hii SMO Hana Tena,zote zimeteketezwa,
Wanamletea Kila siku masilaha na masilaha lkn yanateketezwa.
Jamani eeeh sote tunakubaliana hapa kua NATO ndio umoja pekee wa kijeshi hapa duniani wenye nguvu kubwa kuliko umoja wowote na kuliko nchi yoyote.
Ni Hali ya kweli kabisa ndani ya NATO Kuna nchi Inaitwa Marekani,nchi hii siku zote tunasema Ina bajeati kubwa ya ulinzi kuliko nchi yoyote hapa duniani,tunasema kua ndio nchi yenye jeshi kubwa,uchumi namba moja,ujasusi namba moja na tunasema Ina teknolojia kuliko nchi zote Dunia,hii nchi inaweza ikakuvalisha jina la kuwa wewe ni gaidi Na Ina uwezo wa kukuvua.
Tunakuabali kua Marekani ndio nchi tajiri namba moja duniani.kwa kifupi tunasema Marekani yeye peke yake ndio superpower.
Haya lkn ndani ya NATO Kuna nchi zenye teknolojia kubwa sana Kwa Kila kitu,kuanzia teknolojia za silaha,ujasusi na vitu vingine nchi mfano UK,German,France, Italy,Canada, Denmark, Norway,Spain,Poland, Belgium, Sweden, Finland etc.
Ndani ya NATO Kuna nchi tajiri zaidi duniani yaani G7.
Sasa ndugu zangu mnashangaa Nini kwa Urusi kuchukua muda wa miaka miwili kukabiliana na nchi inayopewa misaada ya "Hali na Mali" na nchi hizo nilizozitaja hapo juu?
Jamani eeeh naomba tuone kwa macho yetu ukuu,maajabu na uwezo wa Urusi.
Urusi peke yake inaweza kupigana dhidi ya nchi ya Ukraine inayopewa Kila aina ya msaada inaoutaka wa silaha ,ushauri, ujasusi,mafunzo,vikwazo, satellite,mbinu,askari na propaganda nk.
NATO walichofanikiwa ni kupunguza ty spidi ya Urusi kupata ushindi lakini wameshindwa kufanya Urusi ishindwe vita hii ambayo Kwa kuisaidia Ukraine Kwa Kila kitu lengo lao ishindwe.
Ndugu zangu,kwa kuangalia hasara nadhani hamutaki Tena kuangalia UkraiNATO wamepata hasara kiasi Gani Bali mnnangalia Urusi TU kimsingi UkraiNATO wamepata hasara kubwa mno.
Jamani eeeh Kila siku tumekuab tunasikia Urusi imelipuq treni iliyokua Ina shehenq za silaha,Urusi imelipuq meli iliyokua Ina shehenq za silaha,Urusi imelipua makambi yaliyokua na shehena za silaha,Urusi imelipua majengo ya chini ya ardhi ya kuongoza vita ndani yake kulikua Kuna wakuu ama wa USA Poland,UK , Ukraine n.kama wakuu wengine wa NATO.
Ndugu zangu haya yote hayajafanyika siku moja yamekua yakifanyiaka toka vita ianze.
Baadhi ya Maafisa wakuu wa NATO na hasa USA waliuliwa huko na baada ya kuuliwa utasikia huko USA wakisema Afisa huyu alikufa kwa jali alikua akifanya mazoezi ya kupanda milima,ama ajali ya helkopta,ama ajali ya gari,kumbe vijana wa Putin walifanya Yao
Suala la askari wa Korea kaskazini kufika vitani,jamani eeeh nimeshasema hapo juu NATO nao wengi TU wamekufia vitani,hivi mmesahau hapa juzi kati Wataalamu,wakufunzi na waalimu wa wasuala ya kijeshi ya mawasiliano na wanafunzi wao wa chuo Cha
kijeshi waliteketezwa chuoni hapo Ukraine?wataalamu kutoka USA,Finland Sweden n.k.
Ndugu zangu Mimi Lee nitakua mtu wa mwisho kuiona Urusi kama ni nchi dhaifu kwa sababu Urusi peke yake ikiwa imewekewa vikwazo kuliko nchi yoyote hapa duniani imeweza kukabilania na nchi zote hizo,nchi zenye nguvu kabisa hapa duniani.
Urusi ingekua dhaifu Leo hii tungekua hatuandikib hivi.
Kwa kifupi Urusi imeweza kuteketeza silaha nyingi sana za UkraiNATO kuliko silaha za urusi zilizoteketezwa,ndio maana unaona Leo majeshi ya Ukraine ndio yanayorudishwa nyuma na ardhi yake kuchukuliwa licha ya masilaha yote hayo kusaidiwa kutoka west.Kama silaha za urusi zingekua zimetekekezwa kwa wingi Leo hii majeshi ya UkraiNATO yangekua Yako mpakani mwa Ukraine na Urusi na hakuna hata centimeter moja ya ardhi ya Ukraine ingekua imekaliwa na Urusi.
Watu wanapiga propaganda eti Ukraine inashindwa,labda inashinda kwa kurusdi nyuma.
Kuna watu watakwambia hata Urusi inasaidiwa.
Eti inasaidiwa na Korea kaskazini'.
Hivi wakorea wamekuja lini Urusi?
Maana smo ilianza 2022.
Watasema Urusi inasaidiwa na china na ran .
Hivi ni lini marafiki wa Urusi wanakaaga vikao kama vile NATO wakaavyo na kuchangishana fedha ,wanajeshi na silaha?
NATO wanakaa vikao Kila mara kwa ajili ya Ukraine ambae sio mwanachama wa NATO.
Jamani eeeh vitani Kuna kupiga na kupigwa ,hata USA alipoivamia Iraq licha ya udhaifu na udogo wa Iraq kijeshi na kiuchumi dhidi ya Marekani na washirika wake lakini wanajeshi wengi TU wa Marekani walikufa.
Kubalini kataeni Urusi imeonesha maajabu makubwa sana hapa duniani,Urusi inastahili heshima.
NATO wameogopa kuweka No fly zone,wameogopa kudungua makombora ya Urusi kama walivyodungua ya Iran,wameogopa kuingia waziwazi wanaingia kama mamluki (mercenaries).
Walisema Urusi haiwezi kupigana mda mrefu,kumbe wao ndio hawawezi,
Urusi imeishiwa silaha,kumbe wao ndio zimekwisha,maana imejulikana kua Urusi inazalisha silaha mara Tatu kuliko NATO wote.
Silaha za urusi duni,kumbe zao ndio dhaifu.
Jeshi la Urusi dhaifu kumbe ndio jeshi imara.
Propaganda hazisaidii Sasa hivi.