Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Dunia ndio inalalamika maana Putin alijinadi anafanya special operation, sasa amekua frustrated anafyatua makombora popote kama kichaa, ila kwa yote bado vifaru vyake vinaliwa shaba, amepoteza mamia ya vifaru na maelfu ya wanajeshi, amechanganyikiwa hajui pakutokea.
Hahaaa haa hii coment ya layman sanaa ambaye hana uhakika wa kula kesho
 
Ndio tatizo lako,unataka yale yanayokufurahisha wewe tuu
Huyu jamaa huwa anachekesha sana,sijui wakati anajiunga JF hakujua kuwa atakutana na mawazo kinzani? Unakuja kwa forum na unataka udictate kile unachokitaka,JF imekuwepo way back 2006 ina utamaduni wake sote tunaujua ni kuwa na mawazo kinzani,huwezi vumilia rudi kwa Tiktok Mazee 🙂😀
 
Kama unaweza kuweka kwenye PDF hoja na majibu ya member Warusi wazalendo humu JF ukaanza zipitia upya moja baada ya nyingine utagundua kuwa tangu day 1, wana expectation kubwa mno. Wanatamani lishuke bomu moja limalize kila kitu wamtukuze Mrusi ila Puttin anawaangusha.

Mmoja alisifia maamuzi ya Puttin kushambulia maeneo yenye makazi Sasa hivi huyo huyo ameshasahau anasema warusi wana utu sana hahawezi piga sehemu yenye watu hii ni operation sio vita.
Wenyewe wanasema Red Army lipo limetulia tu linawasubiri NATO utadhani Putin alisema anakwenda vitani na NATO😅
 
Kama unaweza kuweka kwenye PDF hoja na majibu ya member Warusi wazalendo humu JF ukaanza zipitia upya moja baada ya nyingine utagundua kuwa tangu day 1, wana expectation kubwa mno. Wanatamani lishuke bomu moja limalize kila kitu wamtukuze Mrusi ila Puttin anawaangusha.

Mmoja alisifia maamuzi ya Puttin kushambulia maeneo yenye makazi Sasa hivi huyo huyo ameshasahau anasema warusi wana utu sana hahawezi piga sehemu yenye watu hii ni operation sio vita.
Nyinyi ndio mnataka Ukraine iangamie maana mnasema Urusi ni dhaifu kwa kushindwa kuiteka Ukraine.
Kwa maana hiyo nyinyi mnataka Urusi ianze kutumia silaha kali za kuuwa maelfu ili ashinde vita haraka.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Nilijisahau rafiki nenda telegram
Intel Slava Z utazikuta...

Vile vile Ukitaka zingine ingia apa

Ukitaka Free Uncensored info nenda apa

View attachment 2153974

Zipo nyingi tu ila hyo ya kwanza na ya pili ndio zenye video nyingi za matukio...
Shukran mkuu.
 
Wapi Ukraine wameihangaisha Urusi!? Kwa vigezo vipi!? Kuchukuliwa miji yao, mji mkuu wao kuzingirwa na kushambuliwa na mabomu, kuharibiwa miundombinu yao ya kijeshi na kiraia, kutekwa viongozi wao na kuvuliwa madaraka (i.e. mayor), kukamatwa kwa masilaha yao na yale waliyopewa kama msaada, Raia wao kuuliwa na mamilioni kukimbia nchi yao, kuzimika matarjio yao ya kujiunga na NATO, etc. Huko ndio kuihangaisha Urusi!? Mind you Ukraine ndio anapigana vita wenzao wapo kwenye Operation tu[emoji1787] Na hao west wanasema app. 90% ya silaha zilizokuwa deployed Ukr bado zipo. Sasa km 10% tu ndio zimearibika na matokeo ndio hayo sijui huko kuhangaishwa mnakokusemea ni kuhangaishwa kupi na hapo bado inaamikika bado sophisticated weapons hazijatumika!!

Vita ilitakiwa iwe imeisha na nani!? Wewe ndio ulitaka vita iwe imeisha!? Kama mpaka hapa hamtaki kuappreciate achievements za Rf kwenye hii operation sijui mnataka mpaka nini kitokee ndio mkubali? Au Unataka mpk ukraine wafe wote raia na wanajeshi na nchi iwe majivu!? Watu wanatengeneza corido za kibinaadamu kuruhusu raia watoke huku majadiliano bado yanaendelea kukiwa na possibility ya 'ceasefire' hayo yote yanachangia kuchelewesha na kupunguza mapigano nyie hamlioni hilo!? And no sir Ukraine sio poorest in europe. gdp nominal 22th, gdp ppp 16th unamdogosha hivyo ili uoneshe udhaifu wa Russia au!? Chambua mambo ya silaha unavyotaka taja kila aina ya kifaa pitia kila mtandao na iwe itavyokuwa mwishowe Russia ni world's military Superpower. He took crimea nobody said nothing. Now he's going to take the entire ukraine and again nobody will say a thang! Na Russia's military mighty utaiona pale Poland na USA wanarushiana mpira wa kupeleka ndegevita ukraine. Wangekuwa washapeleka ila wakifikiria Putin is unpredictable and right now he is all gas no brakes wanaishia kumbwela tu

"Russia is the only country on planet that makes the US think twice before doing something"

That is the pain in the axx kwa nyie Pro-west




Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Shida huyu jamaa anajiona anajua kila kitu kumbe bure kabisa
 
Mkuu ni kweli Urusi inaweza kuwa imeonesha udhaifu ila mm kinacho nikera ni kurazimisha Urusi ifanye kitu ambacho hata hao nato wenye nguvu unao wasema hawajawahi kufanya na hawatakaa waweze kufanya.
Ukraine ni linchi likumbwa mno na lenye miji mingi huwezi kuliteka kirahisi ndani ya muda mnao taka Urusi afanye labda utume jeshi la watu milioni moja

Mkuu na ww acha kuikuza sana Israel tofauti na uharisia.
Sasa hivi upo unainanga Urusi kwa kushindwa kuiteka Ukraine ndani ya wiki tatu za vita.
Lakini mbona hauongelei kushindwa kwa Operation ya Israel ya kuliangamiza kundi la hamas na kuidhibiti gaza mwaka 2014?

Tena Operation hiyo ilidumu zaidi ya mwezi lakini hakuna walicho kiambulia zaidi ya kupoteza wanajeshi wake, kupoteza baadhi ya vifaa vyake na kuuwa watu wasio na hatia, ina maana hamasi ingekuwa na silaha za kisasa kama alizo nazo Ukraine Israel ingekumbana na maafa makubwa sana kuliko hata haya anayo kumbana nayo Russia.

Mkuu kuhusu udhaifu wa silaha za Urusi dhidi ya zile za kimagharibi, mbona huongelei silaha za kimagharibi ambazo mpaka sasa zimeshindwa mbele ya silaha za kirusi na kiirani nchini Yemen na Syria?

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Huyo jamaa yupo kishabiki zaidi, si unaona hapo anasema Putin ni dikteta. Hilo neno dikteta lipo kwa ajili ya justification ta west kumchukia mtu.
Nato wapo zaidi ya nchi 30, USA, Canada, Uk, Germany na France bila kusahau Poland wamepeleka vifaa vya kijeshi na mercenaries wa kutosha. Hili la urusi kuendelea na operation kwao ni mshangao. Hawataki ku admit tu, lakini nguvu waliyompa Ukraine na kipigo anachopata inabidi kuheshimu urusi.

Leo kuna taarifa urusi anapekeka meli za kivita kule Ukraine, ina maana waneona threat ni kubwa, mda si mrefu tutaanza kushuhudia vita kamili, na sio operation maalumu tena.
 
Nyinyi ndio mnataka Ukraine iangamie maana mnasema Urusi ni dhaifu kwa kushindwa kuiteka Ukraine.
Kwa maana hiyo nyinyi mnataka Urusi ianze kutumia silaha kali za kuuwa maelfu ili ashinde vita haraka.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Mkuu anayetaka Ukraine iangamie ni Marekani na NATO.

Kama wasingepeleka silaha na mamluki operation ingeshaishaga.

Sasa Putin ataiangamiza kama bado Mmarekani anaxidi kuleta silaha.

Hii ni mbinu ya kummaliza Russia nguvu za kiuchumi ili wamwigilie kisawa.sawa.
Mi naona Russia atumie silaha nzito ili hili nalo liishe maana laweza leta WW3 ikiwa litaendelea
 
Aweke military base wakati yeye ndio analolipa silaha zote Taiwan huku China akipiga kelele tuu. Kambi zake za South Korea, Japan na Philippines zinatosha.
Sasa ndicho ambacho Russia amezuia Kwa US kuweka Kambi Ukraine!Ndivyo pia US alivyozuia Russia kutoweka Kambi Cuba!
 
Urusi ya kale

Mababu wa Urusi na Ukraine walikuwa sehemu ya nchi ya slavic iliyoitwa Kieven Russia. Ilianzishwa na Viking Oleg katika karne ya tisa.

Faith Hillis, Profesa wa historia ya Urusi kutoka Chuo Kikuu cha Chicago, anasema kwamba eneo la bahari ya baltic na bahari nyeusi, ilipo sasa Ukraine, iliishi jamii ndogo karibu miaka elfu iliyopita.

"jamii hizi ziliamua kuungana na kuunda nchi mpya chini ya uongozi wa wafanyabiashara wa Scandinavia wanaosafiri kutoka Scandinavia kwenda Byzantium kupitia mto Nipro. Nchi hii mpya iliitwa Kieven Uussia na mji mkuu wake ulikuwa unaitwa Kiev ambao ni mji mkuu wa Ukraine sasa. Watu hawa wa Slavic hawakuwa raia wa Ukraine wala Urusi. Pia ilijumuisha jamii zisizo za Kislavoni kama vile jamii za makabila, Mongolis, Waislamu na wayahudi."

Jamii tofauti za eneo hili ziliunganishwa na imani ya kidini ya orthodox, wakiunganishwa na himaya ya mashariki ya waroma. Wengi hapa walibadilika kuwa Wakristo wa orthodox, ingawa pia kulikuwa na jamii tofauti za rangi.

Katika karne ya 13, jamii ya Mongols walivamia Kieven Russia. Idadi kubwa ya watu wa 'Slavic' hapa iligawanywa katika sehemu tatu kubwa. Baadae mgawanyo huu ulizaa Urusi, Ukraine na Blarus ya sasa.

Katika karne ya 14, wakati Mongols inaanguka, kulikuwa na tishio jingine uvamizi wa Kiev. Poland ilikuwa inajiandaa kupanua mipaka yake na uongozi wake ulikuwa mikononi mwa wakoloni wa kirumi.

Faith Hillis anasema, "Poland na Lithuania waliungana mikono, na katika karne ya 16 walianza kuelekea eneo la kusini. Kiev ikawa chini ya utawala wa Poland-Lithuania.

Historia ya Urusi na Ukraine iliingia katika sura mpya katika karne ya 17. Jamii ya Kiev, chini ya Poland, na jamii ya warusi wakiongozwa na tsar (kama mfalme) wa kirusi wakaunda kitu kinaitwa muungano wa Kikristo wa Orthodox.

Faith Hillis anaelezea, "hii ilikuwa hatua kubwa ya mambo kuanza kugeuka ambapo majadiliano juu ya masuala ya utaifa yalianza na yanaendelea mpaka katika zama za sasa.

Katika karne ya 18, ulikuwa wakati Urusi ilipounda himaya ya warusi ikijumuisha sehemu ya mashariki ya Ukraine. Ikawa na utamaduni wake, utawala wake wa uhuru na viongozi wake.

Jina la Ukraine ya mashariki sasa ilikuwa Novorasia yaani Urusi mpya. Wakati huo huo, sehemu ya upande wa magharibi ilibaki kwanza kuwa chini ya Austria na kisha baadaye chini ya utawala wa nasaba wa himaya ya Austro-Hungarian.

Mvutano huu himaya barani Ulaya ulisababisha vita vya dunia mwaka 1914. Miaka minne baadaye, wakati vita vilipomalizika, hakuna aliyebaki salama, si Austro-hungary wala himaya ya Warusi iliyonusurika.

Muungano wa Soviet
Sarhi Ploughti, Profesa wa historia kutoka Chuo Kikuu cha Harvard na Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa wa-Ukraine, anasema kwamba machafuko yaliyoibuka baada ya vita vya kwanza vya dunia na mapinduzi ya urusi yalibadilisha ramani ya bara la Ulaya. Wa-Ukraine wakaunda kuunda nchi yao huru. Mwaka 1917 Ukraine ikawa Jamhuri ya ujamaa ya soviet. Lakini haikuchukua muda mrefu.

Mwaka 1921, mkataba wa 'riga' ulisainiwa ili kumaliza vita vya Poland-Soviet, ambapo baadhi ya maeneo ya Ukraine yakawa sehemu ya Poland, Czechslovakia na Romania, wakati baadhi ya Jamhuri za Ujamaa za Soviet zilikuja kwenye umoja wa Soviet ulioongozwa na Vladimir Lenin na Bolshevik.

Rais wa sasa wa Urusi Vladimir Putin analichukulia hilo lilikuwa kosa la kihistoria. Kwa mujibu wake, Jamhuri ya Soviet yaani Ukraine ya Mashariki, Donetsk na Luhansk zilikuwa sehemu ya Urusi.

"Mwaka 1939, Hitler (kiongozi wa Ujerumani aliivamia Poland, iliyokuwa na kundi kubwa la wachache wa wenye asili ya Ukraine. Raia wa Ukraine walishirikiana na wanjeshi wa nazi. Aliona Poland kama ya ya ukandamizaji na ujerumani kama mshirika. Harakati za kizalendo za raia wa Ukraine wakaweka ushirika na wanazi. Lakini ushirika huo haukudumu.

"Wakati Jeshi la Ujerumani lilipoingia Ukraine, wazalendo walitangaza uhuru wa Ukraine. Wakakamatwa na Ujerumani. Mwishoni mwa 1941, mashirika yote ya wazalendo wa kiukreni yalikuwa ya kupambana na nazi, na wakati wanazi walipohamia sehemu nyingine za ukraine, mamilioni ya ukraini walijiunga na vita hivyo."

Uhuru wa Ukraine
Disemba 1991, viongozi waaandamizi wa Urusi, Belarus na Ukraine walikutana huko Belarus. Pande zote tatu zilikubali kuondoka katika Umoja wa Sovieti. Zama za Soviet zikafika mwisho. Ukraine ilikuwa tayari kuwa taifa huru.

Margarita Bameseda, Profesa katika Chuo kikuu cha Seaton nchini Marekani, anasema Ukraine ikawa huru, lakini maisha hapa yalikuwa magumu kwa watu wa kawaida.

Margarita anaelezea, "wakati huo, ilisemwa kwamba siasa za Ukraine zinatoka Kiev lakini pesa zinatoka Donetsk. Hii ina maana kwamba Donetsk ilikuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi, waheshimiwa hapa walikuwa wameacha mambo ya siasa kabisa kwa kiev."

Mwaka 2004 Ukraine iliingia tena katika mzozo. Kulikuwa na mapigano kati ya Viktor Yanukovych inayoungwa mkono na Urusi na Viktor Yuschenko, anayeungwa mkono na nchi za magharibi, katika uchaguzi wa rais.

Yanukovych alitangazwa mshindi, lakini alishutumiwa kwa wizi wa kura na maandamano dhidi yake yalianza. Maandamano hayo yalijulikana kama mapinduzi ya machungwa. Rangi ya chungwa ilikuwa rangi ya kampeni ya uchaguzi wa Yuschenko.

Margarita anasema, "watu kwa mara nyingine tena walitaka uchaguzi ufanyike upya na Yuschenko akashinda na kuwa rais. Ilikuwa hatua kubwa ya mabadiliko makubwa ya kidemokrasia. Baada ya hapo uchumi wa Ukraine ukaanza kupaa.

Mwaka 2010, Viktor Yanukovych alipata uungwaji mkono kutoka sehemu za mashariki na kushinda uchaguzi. Hapa mapinduzi mengine Ukraine yalikuwa yanaanza.

Harakati za viunga vya Midan
Mambo yalizidi kuwa magumu mwaka 2013. Yanukovych alipaswa kuchagua kati ya Ulaya au Urusi. Kabla ya kuingia makubaliano na umoja wa ulaya, akasitisha uamuzi huo na kuishutumu Urusi kwa shinikizo lake la kutaka Ukraine isijiunge na Umoja wa Ulaya

Kwa upande wa magharibi mwa nchi hiyo, watu walihisi kwamba uamuzi wa Yanukovych ulikuwa umevunja ndoto zao za kuwa na maisha bora ya baadaye. Karibu watu 100 waliuawa katika maandamano katika uwanja wa Midan mjini Kiev. Yanukovych ikabidi akimbilie kujificha Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akaingilia hali ya mambo Ukraine, akatangaza Crimea kuwa sehemu ya Urusi na kuanza kudhibiti maeneo ya Luhansk na Donetsk.

Tangu mwaka 2014, mgogoro katika maeneo ya mpaka wa Urusi na Ukraine haujawahi kwKabla ya Urusi, iliyokuwa ikiongeza idadi zaidi ya wanajeshi kwenye mpaka wake na Ukraine kwa miezi kadhaa, ikaivamia Ukraine mnamo 24 february 2022.
 
🇸🇰The only Slovak S-300 can be handed over to Ukraine only when it has a replacement.

Defense Minister Yaroslav Nagy said that the republic should first of all think about its own security.

On Wednesday, the media reported that Slovakia had allegedly already previously agreed to transfer the S-300 air defense system to Ukraine on the condition of its immediate replacement with appropriate equipment for its army.

“We are all striving to help Ukraine as much as we can, but I am the Minister of Defense of Slovakia. I must think first of all that the defense interests of the republic are fulfilled,” Nagy said.

Today head of the Pentagon Austin will visit Bratislava. It is assumed that the transfer of S-300 to Kiev may become one of the topics of negotiations.
 
Back
Top Bottom