Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,465
- 5,672
Makubaliano na nani? Na Biden? Na Putin?Mkuu, mazungumzo na mashauriano yalishafanyika kitambo sana tangu mwaka jana Trump aliposhinda uchaguzi (na hata kabla ya uchaguzi maandalizi ya msingi yalikuwa yameshafanyika).
Kwa sasa utawala wa Trump unatekeleza tu makubaliano hayo. Usidhani jamaa anakurupuka au unabahatisha.
Ajenda kubwa kuhusu vita vya Ukreni ni kumaliza mzozo huo lakini katika namna ambayo dunia ya Magharibi na NATO itashawishiwa kudhani wao ndio wameshinda, ingawa kila mtu anajua Urusi ndiye mshindi hadi sasa. Putin ameshajinyakulia pointi 3 muhimu!
Marekani anaogopa aibu kuliko hasara. Yuko tayari kutumia mabilioni ya dola ili kufidia ombwe analodhani litamletea kadhia kwenye macho ya washirika wake.
Si ajabu tunaona kuna ubwekaji mwingi na kauli zinazoonekana kupingana na NATO, na wakati mwingine wanapingana Wamarekani wao kwa wao.
Marekani ya sasa iko kwenye survival mode. Vita vya Ukreni vimewajeruhi sana kiuchumi, kisiasa na kiushawishi duniani kote.
Marekani ione aibu? Tangu lini? Are you joking? Endelea kusikiliza vimbwanga vya Trump kama kuna mtu wa kuona aibu hapo.