Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hapo kwenye nuclear napingana na wewe nadhani wanaweza wakazitengeneza kwa siri bila kujua
 
Russia anachukuwa ardhi lakini wanajeshi wake wanachinjwa kila siku.
 
Upo sahihi, Ukraine angepewa 'offensive weapons' kwa kiasi alichohitaji Urusi ingepata tabu mno.

Alafu Ukraine imepewa silaha chache tu tena kwa kuchelewa sana na kwa masharti mengi yanayodhibiti matumizi yake.
Kwa Nini Ukraine apewe silaha na nchi nyingine wakati anapigana na nchi nyingine?
Ukiona nchi moja inapigana na nchi nyingine lakini Haina silaha zake Bali inategemea kupewa na nchi nyingine ili ipigane na adui yake basi ukae ukijua ni zile nchi zinazotoa silaha ndio zinapigana na hiyo nchi moja.
Kwa kifupi ni kwamba nchi za west zimeunganisha nguvu kwa ajili ya kupigana na Russia peke yake kwa kujifanya zinamsaidia Ukraine.

Hii ni tofauti na mfano huu,
Tanzania na Malawi zinapoingia vitani,Tanzania ama inanunua silaha ama inakopa silaha kutoka china na Malawi ama inanunua ama inakopa silaha kutoka UK,kwa mfano huu hapa ni kweli Tanzania na Malawi zitakua zinapigana zenyewe.
Lakini vita kati ya Ukraine na Urusi pale Urusi inapopigana peke yake na Ukraine inategemea silaha zote kutoka west,wataalamu,wanajeshi, intelligence,huduma za satellite,mafunzo, vikwazo n.k hivi vyote vikiwa vinafanyika kwa wakati mmoja hii tunaita ushirika wa kivita kama vile USA na washirika wale walipoivamia Iraq, Afghanistan na Libya.
Na hii ndio tunaiona katika vita vya Ukraine.
 
Upo sahihi, Ukraine angepewa 'offensive weapons' kwa kiasi alichohitaji Urusi ingepata tabu mno.

Alafu Ukraine imepewa silaha chache tu tena kwa kuchelewa sana na kwa masharti mengi yanayodhibiti matumizi yake.
Hahaha 😆 na bado mtasema
 
Ingekuwa ni Ukweli, Urusi ingekuwa na wakati mgumu mno kuliko Sasa.

Urusi ndio imeshatumia Kila silaha waliyonayo isipokuwa nuclear.

T14 Armata
Huenda mwenzetu utakuwa unalipwa, haiwezekani kila unapopewa hoja za ukweli juu ya maandalizi ya kutosha ya kijeshi, silaha na intelijensia aliopewa UKRAINE siku inayofuata unarudi tena msimamo ule ule.
Msikilize hapa BIDEN anachoongea.
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Ukraine alisema usalama wa viongozi watakaoenda May 9, ni at their own risk na atashambulia red square
Tunasubiri tuone
 
Kwa kifupi ni kwamba nchi za west zimeunganisha nguvu kwa ajili ya kupigana na Russia peke yake kwa kujifanya zinamsaidia Ukraine.
Hakuna nchi inajitosheleza na kupigana peke yake.
-Russia juzi wamekiri kuwa na askari toka korea baada ya report ya askari 600 wa korea kuuliwa.
  • Kuna raia wa china walikamatwa wakipigana upande wa Russia
  • Russia anatumia drones toka iran.

Ushirika kwenye vita ni jambo la lazima.
 
Ukraine alisema usalama wa viongozi watakaoenda May 9, ni at their own risk na atashambulia red square
Tunasubiri tuone
Hii umeitoa wapi boss?
Hata kwa fikra na hesabu za kawaida Ukraine wako tayari kumuua Rais wa Uchina?
Wako tayari kumuua Putin?
Halafu wakishafanya hivyo kifuate nini juu yao?
Nb. Sheria za kimataifa zinakataza hili waziwazi ndo maana muda wote huu wa vita huko Ukraine Putin hajawahi kuthubutu kupiga ikulu au kumuua kiongozi yeyote wa kiraia.
 
Fuatilia mkuu, hiyo statement ya Zelensky
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…