Ila mie nadhani wewe ndio unaetakiwa kwenda kujifunza "Politics" kwanza kabla ata ya kuijua hiyo "Geopolitics" yenyewe.
Hakuna adui wala rafiki wa kudumu kwenye ulimwengu wa kisiasa. "Ni nini napata kutoka kwa nani na yeye anapata nini kutoka kwangu"... Kutoka apo ndio utapata "Urafiki wa kisiasa na Uadui wa kisiasa" kwani hivo viwili havipatikani isipokuwa kwenye masilahi tu.
Yawezekana upo nyuma kidogo katika taarifa. Una habari kama Saudia na UAE walizichunia sim za Biden? Una habari kama Saudia katangaza kuanza kuuza Gas yake China kwa Yuan? Una habari kama Assad kakutana na Waziri mkuu wa UAE?
Unaeza kuunganisha hizo dot kugundua kitu?
Kwa hali iliyopo Ukraine, Aliyekuwa anapewa full backup na USA kabla "hajaingiliwa" na Russia, kisha kutoswa baada ya tukio na kuishia kupelekewa silaha tu wakauane vizuri... Hii inatoa alert ipi kwa nchi zilizo mlengwa wa USA kwe issue za kiusalama???
Je ka we waijua Geopolitics unafikiri nini Saudia angefanya kama USA anaenda shikana mikono na "Adui" wa Saudia ambae ni Iran kuhusu kuufufua mpango wa nuclear?
Je ushajiuliza kama USA hataki pigana na Russia "akidai ni WWIII" Je atafanya nini Iran ikiingia saudia kwa backup ya Russia? Naye atasema kwasab hayupo NATO ko hataenda msaidia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Unafiki wa USA na washirika wake ushaanza kujidhihirisha wazi na soon baada ya hii vita binafs naona kutakuwa na shift ya World Order kutoka kule tulikokua tumezoea kwenda upande mwingine.
India si huyo apo kanunua zaidi ya mapipa Mil 3 kutoka Russia juzi tu apa. Na kasema Nishati yake isihusishwe na siasa itaharibu uchumi wake [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]....