Alexander Lukashenko
JF-Expert Member
- Sep 9, 2017
- 4,323
- 10,199
Mkuu hypersonic missiles sio tu kwamba Ukraine hawezi stahimili, ni kwamba hakuna nchi yeyote inaweza stamihili hypersonic weapons. Hata Israel yenye strongest na most active air defence system 24/7 haiwezi zuia hypersonic weapons ambazo Russia na China ndio wanazo tu, Marekani testing zake hazijawa successful. Unajua mwaka juzi nilipokuwa naona hizo Kinzhal zinafanyiwa testing na wakasema ziko tiyari sikuamini sana maana development period ilikukuwa ndogo na ambavyo Russia wana ugonjwa mkubwa wa delay kwenye development. Kwa sasa nasubiria kusikia Poseidon yao iko tiyari kwa matumizi ya underwater, mojawapo ya silaha game changer ila sio ya level za Ukraine.
Russia huwa wana uhaba wa precision guided munitions na hawapendi kuzitumia sana wanakwepa gharama. Wanategemea wanyanyue Tu-22 ibebe dumb bombs kibao idondoshe ila sasa bado hawana air dominance Ukraine na of course ni kweli wanakwepa kuua raia wengi kelele zisizidi. Strategically naamini watatumia hizo very high speed missiles kuharibu kama hizo shipments za NATO ila si lazima sana kuzitumia kwingine. Wakitumia na Kalibr pia.
Tatizo la Russia hajawa na attack drones za uhakika, hizo Orion alizotengeneza kwa msaada wa Israel hazijaonesha maajabu sana ila nina imani Sukhoi Su-79 Okhotnik ikikamilika miaka ijayo itakuwa on par na American drones. Kutumia missiles zinazosafiri umbali mrefu, zenye circular error probability (CEP) ya mita kadhaa za mraba, za gharama kubwa haiwezi zidi matumizi ya drones za size ya kati, zenye low radar cross section na secure communications, zinazokaa angani masaa 20 zikizurula strategic area kusubiria any possible target kisha zinadondosha smart bomb ambayo haina gharama sana na iko very accurate.
Nasubiria hizo silaha za Marekani alizotoa ikitokea akaleta kamikaze drones zinaitwa Switchblade hapo kazi ipo sana kwa Russia
Ngoja tuone....
Kombora linalofumua mpaka mahandaki, sio la level ya vita hii.