Matokeo ya uvamizi wa Russia
1.Uvamizi wa Russia ukifanikwa utachochea baadhi ya mataifa mengine kuvamia jirani zao ambao wanaamini walipaswa kuwa sehemu zao.Tunaweza kuiona China ikivamia Taiwan, Sudan Kaskazini ikiivamia Kusini, Ethiopia ikiivamia Djibouti au Somalia n.k
2.Mataifa yote duniani hasa Marekani na Ulaya yataongeza kiasi cha bajeti kwa ajili ya sekta ya ulinzi, majeshi, silaha na kujiandaa na vita wakati wowote. Sekta nyingine zote na nchi tegemezi kama nyingi za Afrika zitaathiriwa kibajeti kwa njia hasi.
3. Mataifa mengine makubwa ya Ulaya yanayopakana na Russia, Finland na Sweden yanaweza kujiunga na NATO kwa mchakato wa haraka ili yajihakikishie usalama dhidi ya uvamizi wa Russia.
4.Viwanda vya silaha vitashamiri, teknolojia mpya za silaha zitaundwa kwa kasi.
5.Ukali wa maisha utaongezeka kwa mataifa mengine duniani, Russia na Ukraine wanatoa takribani ya theluthi ya ngano inayouzwa duniani, uzalishaji utapungua.
Pia tufahamu
1.Hakuna maslahi yoyote ya Urusi yaliyotishwa na Ukraine hadi kumfanya Putin kuivamia hiyo nchi.Tayari kuna nchi tano zinazopakana na Urusi ambazo ziko NATO hizo ndizo zingekuwa zinatishia zaidi maslahi yake. Ndio maana unaona maandamano ya kuipinga hiyo vita ndani ya Urusi. Sio rai wengi wa Urusi wala jeshi lao wanaolewa kwa nini Putin ameivamia Ukraine.
2.Russia haijaanza kuivamia Ukraine leo, imeanza zamani sana hata kabla haijawa superpower na mara zote Ukraine imekataa kuwa chini ya Himaya ya Russia. Putin anajaribu tena kutengeneza hiyo Himaya.Nchi nyingine zilizowahi kuvamiwa na Putin ni Chechnya 1999 na Georgia 2008.
3.Hakuna Eastern block, Eastern block ilianguka mwaka 1990 na nchi 14 zilijitoa kwenye hiyo block kwa maandamano na mwishowe kura za kuikataa USSR na Russia. Nyingi ya hizo nchi zilipiga hatua kuwa za kidemokrasia na kuungana na Ulaya Magharibi katika EU na NATO. Imebaki Belarus tu ambayo dikteta wake anaharibu uchaguzi kwa usaidizi wa Russia kuendeleza utawala kidikteta uliokataliwa na raia.
4.Hii sio vita Russia kulinda maslahi yake yanayotishiwa na Ukraine, ni vita ya kutanua Himaya kama vita za Empires za kale karne ya 19 kurudi nyuma. Putin ana ndoto Ukraine sio nchi kamili kwamba ni sehemu ya Russia tu. Akiwa na Ukraine na Belarus kwapani kwake anaona kutimia kwa ndoto yake ya kuifanya Russia ya sasa kama aina fulani Umoja wa Kisoviet wa kale.