Akizungumza kwenye kikao/mkutano chama Cha conservative huko Blackpool Waziri Boris Jonson alisema,
" Ni wazi kwamba Putin amefanya kosa kubwa (catastrophic mistake) na unatakiwa kujiuliza KWANINI kafanya hivyo??
Kwanini aliamua kuivamia nchi hii isiyonahatia kabisa,
Siyo kweli kwamba aliamini Ukraine itajiunga na NATO kwasasa, alijua wazi hakukuwa na mpango wowote wa matarajio za nchi za Magharibi kuweka makombora kwenye ardhi ya UKRAINE.
Waziri Boris alisema,
Putin aliogopeshwa na UKRAINE kwa sababu tofauti, amekuwa na hofu kwasababu UKRAINE wana Uhuru wa habari, na uchaguzi huru,
Ni kwasababu Urusi na Ukraine wamekuwa karibu Sana hivyo mfumo wao unaweza kuwa na athari kwake na Urusi,
Na kwamba Putin anahofu ya kile kinachosemekana kuwa ni MAPINDUZI (Moscow color revolution ) na hivyo kwaukatili anataka kufutilia mbali mshumaa wa Uhuru UKRAINE Jambo ambalo nimuhimu Sana ameshindwa/amefeli.
Waziri pia ameonya Putin mshindi hataishia UKRAINE ataendelea Georgia, Moldova etc hivyo kuanzisha Zama mpya ya Vitisho Ulaya mashariki yote kuanzia eneo la Baltic (baltic region) mbaka bahari nyeusi(black Sea).
View attachment 2157884View attachment 2157885