LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mkuu silaha za Czech Republic sidhani kama zimefika wala kutumika. Hata za Poland zimetolewa jana zitakuwa zimeanza kutumika leo, Urusi wakitoa taarifa hawatoi evidence. At least Ukrainians wanaonesha video clips na picha sometimes.

Ikitokea any International community kama Red Cross ndio tutapata angalau picha ya nani ana casualties nyingi. Russia anaonesha weakness moja kubwa ni supplies na logistics. Akienda frontline harudi nyuma kwahiyo maiti na majeruhi wako uko uko. Hata resupply ya ammunition na chakula hana, wala hatengenezi corridors au pockets kwamba atakuwa anazileta hapo. Hajasecure supply lines maroli ya jeshi yakipita mitaani yanapigwa ambush na raia. Russia vita wameingia juzi ila washaanza kuwa exhausted na walijipanga miezi kibao. Nasema hivi kwa kuwa nalinganisha advancement ya juzi, jana na leo naona washachoka wakati Ukraine ndio wanazidi kupata nguvu. Sijui kama niko sahihi

NB: Wale wanaosema kuhusu Ghost of Kyiv na kills zake dhidi ya Russian Airforce sijathibitisha popote kwahiyo mpaka sasa nauita ni uzushi. Jikinge dhidi ya fake news na propaganda
 
USA alifanya nini Japan? alitumia silaha ya mwisho kubwa kuliko zote.
 
Media zote ni fake wana agenda zao hakuna Media yoyote ina balace kidogo nimeenda Fox news kwa mara ya kwanza wanajitahidi ku report kinachotokea au wanachokiona ila hawa wengine hasa CNN wamekuwa kama TBC tu ndio maana Trump aliwaita fake news
 
Hivi pesa inamchango mkubwa katika stage vita iliyofikia?
Ngoja nikueleweshe Kidogo hapa.

Makampuni ya Kutengeneza Siraha nchini Marekani Kama Reython,Northgrop,Boeing na Mengine yanamilikiwa na watu binafsi Chini ya Sheria ya kudhibiti Siraha ya Marekani.

Kwahiyo,Biden anaposema Anatoa $ 600m kwa ajili ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine anamaanisha hivi;

Akipata Hizo pesa atanunua Siraha kutoka kwenye Makampuni ya Marekani,Siraha hizo ndizo hutumwa nchini Ukraine.

Usione Makampuni ya Siraha ya Marekani yanatumia Pesa Nyingi Sana kuwafadhili wagombea Urais na Ubunge nchini Marekani,Kwasababu wanatafuta Influence ya kuuza Siraha. Vita ni faida kwao. Pia,hawawezi kuuza Siraha Popote pale Duniani bila idhini ya Bunge.

Kwahiyo Usifikili Biden ana ghala la Siraha pale Marekani,laa hasha,yeye anatoa fedha za Serikali kununua Siraha kutoka kwenye Makampuni ya Marekani.
 
Shukran
 
Media zote ni fake wana agenda zao hakuna Media yoyote ina balace kidogo nimeenda Fox news kwa mara ya kwanza wanajitahidi ku report kinachotokea au wanachokiona ila hawa wengine hasa CNN wamekuwa kama TBC tu ndio maana Trump aliwaita fake news
Habari ni pesa....
 
Jamani hii ni kweli? Asee kama ni kweli russia hapana adhibiitiwe mapema hii ni htrView attachment 2131976
Hilo la Chini sio ICBM Tena,Hilo ni Gofu la Injini ya Rocket na Lipo nchini Ukraine. Baada ya Mkataba wa kumaliza Vita vya Dunia,Marekani na USSR walikubaliana kuharibu baadhi ya Siraha za Nyuklia. Moja ni Hilo la Chini lililolala Chini,Liko Makumbusho pale Kiev ambayo ndio ilikuwa Kambi ya Majeshi mengi ya USSR.
 
Kwa mtu yeyote anaeweza kunisaidia nn chanzo cha vita inayoendelea kati ya Ukraine na Russia, chimbuko lake hasa limeanzia wap
Chanzo ni pale jirani yako anawakaribisha watesi wako kwake, wanakuchimba chimba. Sasa dawa kuanza kisago kwa huyo anayewapokea
 
We jamaa [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Kumbe huyu former boxer Vitali Klitschko ndio Meya wa Kiev!?nimemsikia atoa tangazo kwamba atakayetoka usiku baada ya muda wa zuio atachukuliwa kama ni adui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…