Binafsi sipendi vita, na sipendi kuona mtu au nchi ikichukua uhuru wa nchi nyingine.
LAKINI naweza kusema kwamba Rais Putin yuko sahihi kulinda maslahi ya nchi yake. Kumbuka Ukraine ni zao la USSR, kwa namna moja hii ni sawa na territory au state ndani ya USSR...Ingawa hii haifanyi kazi au sio hoja kwa sasa.
Hoja ni kwamba NATO inatumiwa na US kwa nia ya kutaka kuisambaratisha Russia. Putin kuzuia uwepo silaha za NATO ndani ya Ukraine ni sawa na US ilipopiga Cuba sanctions kwa kuruhusu Russia kuweka silaha zake pale. Russia hakuwa na nguvu tena Cuba, na uchumi wa Cuba ukambaratika. Juzi juzi Russia imetaka kusaidia Venezuela, US kapiga pin kufanya mpango wa kumuondoa kiongozi madaraka. Huwezi temper na US security na interests akuache salama, sasa sijui kwa yeye ni ngumu kukubali wengine kulinda interests zao.
Ni kweli US hajapora ardhi, ila madhila alioyoacha Iraq, Afghanistan, Iran ni makubwa sana...yaan bora angechukua nchi maana wananchi wasingekuwa wanahaha na ugumu wa maisha.
USA ina sifa kubwa ya kutetea demokrasia na haki na kutoa misaada yenye kugusa maisha ya watu maskini na wahitaji (binafsi dola ya mmarekani imenisaidia binafsi), ILA ktk agenda ya democracy kuna linaumiza baadhi ya watu.