LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Raia wengi wa urusi wangekuwa wanakubaliana na alichofanya Putin, wasingefungiwa mitandao kma facebook nk

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Kwani kuna RAIA wa USA walikuwa wanataka USA avamie Iraq,ukweli ni kuwa western ndio wanamiliki vyombo vya habari na wanatumia kila aina ya propaganda kumchafua Russia.
Na kweli lazima watumie hizo propaganda maana wanajua uwezo wa Urusi na wasipofanya hivyo Ukraine itakuwa majivu.
 
Mkuu hapa hatuko kwenye mipasho bali tuko kwenye uhalisia.
Kwenye hivi vita Urusi hautumii nguvu nyingi na ndio maana unaona mauaji ya raia ni kidogo na uharibifu wa miundo mbinu sio mkubwa sana.

Hivi unaya kumbuka mashambulizi yaliyo fanywa na Urusi kwenye mji wa Allepo nchini Syria?

Hivi unadhani Urusi ingekuwa inatumia nguvu kubwa hayo majengo unayo ona kwenye miji ya Ukraine yange kuwepo ?

Hata Idadi ya walio uawa sasa hivi ingekuwa maelfu tofauti na sasa.


Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Wanaona mtandaoni na kwenye tv tu hawajui mazingila ya battle field
 
Wazungu akili hawana kwahiyo wanataka vita iendelee mana sio kwakutuma silaha hatar
Wanachotaka kiwe ni Ukraine iwe uwanja wa vita kwaajili ya kumdhoofisha Urusi... Sasa Ukraine yenyewe wanakaza fuvu wakijua wanasaidiwa kwa nia njema
 
Boss ni sawa. Issue yangu ni kwamba katika mataifa mawili yenye nguvu mataifa madogo yanachagua kuwa na ushirika na mwenye nguvu zaidi. Russia hawezi kuweka vikwazo kwa NATO na USA wakifanya uvamizi. Kwanini Ukraine awe na ushirika na nchi isiyo na ushawishi?
Wakati wa dola ya Ottoman ya Kiislamu na dola nyengine kubwa ya Kikristo ilifika pahala pakuwa na mtafaruku mkubwa baina ya pande hizi mbili. Kuna jamii moja ya wazungu inaitwa Khazarian. Mfalme wao alichagua kama Taifa wawe na dini ipi itakayowaongoza katika Taifa. Dini iliyochaguliwa baada ya kukaa na baraza lake la Mawaziri ni dini ya kiyahudi.

Sababu ni kuwa ni kuepukana na athari ya aina yoyote kutoka kwa dola kubwa mbili, ya Ottoman ya waislamu na dola ya kikristu. Hivyo ana gain kotekote. Na athari itakayotokea baina ya dola hizo 2 hazitoweza kuathiri Taifa moja kwa moja.

Ukraine ilibidi iwe neutral ambapo kwake ni mahali salama. Mahusiano yake na west angeyaimarisha kwenye uchumi zaidi kuliko mahusiano ya kijeshi. Wakati mwengine hata kama ukiona ni sahihi ila ukiacha ndiyo njia salama itakayokuepusha na maafa basi ni vizuri kuicha hususani ikiwa unadhamana ya mustakabali kwa wengi.
 
Back
Top Bottom