LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Hao sio wanataka Kuua warusi wanajilinda kutokana na mrusi kuwavamia

Mrusi akirudi nchini kwake wao hawana shida naye sasa mtu akuvamie kwako nikibeba panga useme nakuonea

Kwa hiyo nikae nyumbani kwamgu bila silaha nikuache tu unitwange nyumbani kwangu
Waache wauwawe tu usilalamike.

Russia is a peacemaker

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
 
Unabisha ujinga kweli ndugu, ufahamu na uelewa wako wa mambo no mdogo sana. Russia amewaona Ukraine kama ndugu kabisa wa damu ambao wame-share historia muhimu sana hivyo wamepeleka silaha zile hafifu sana na mpaka sasa haijatumika silaha vimetumika vijisilaha vya enzi za soviet. Ungetaka kujua Russia ni nini NATO angepeleka jeshi.

Mwanzoni eti NATO wakiongozwa na Ujerumani walikuwa wanatoa kauli za vitisho Putin aliposema tu usalama wa Russia upo shakani na kuviagiza vikosi vyote vikae tayari umeona kuna harakati zozote Poland ,umeona kuna kauli imetolewa tena.
Warusi wa Itilima mna maneno
 
  • Thanks
Reactions: F9T
Kwani ukraine ni sehemu ya umoja wa NATO hadi NATO apeleke jeshi?
Libya, Iraq na Syria zilikuwa sehemu ya NATO walipopeleka jeshi kujifanya wanasaidia raia? Una hoja mufilisi sana. Russia kavamia Ukraine na kuwaonea raia kama mnavyosema basi NATO wamepeke jeshi kusaidia uone kama mpaka mpaka wa ulaya haujasogezwa.

NATO wanajua fikra wakiingia pale itabidi Poland waitoe sadaka ya kuteketezwa maana yanayoendelea pale Kapustin Yar yatajulikana Poland
 
Mkuu wewe darasani ulikuwa sio timu ya ubuyu na visheti!yaani unachambua mambo vizuri unaeleweka,Kuna wajinga wanachukulia hili suala Kama movie za Rambo,yaani hawaangalii impact za baada ya hii Vita itayoikumba dunia,wapo busy kuchekelea eti Putin mbabe,Wanamsifia mtu anaharibu atmosphere ya dunia kweli..Tanzania sisi na serikali yetu tunafanana akili zetu,dunia nzima imelaani hili suala sisi serikali inasema haina msimamo ,huku Wananchi wako wanampraise Putin akalie nchi ya mwenzie kimabavu,yaani hata sielewi akili zetu huwa Zina nini!
Halafu sasa kichekesho kikubwa ni hawa hawa wanaomshangilia Putin enzi za Serikali ya awamu ya Tano na hata kule Jukwaa la Siasa walikuwa wanatokwa mapovu ya kulaani Udicteta wakiongozwa na kina Yericko Nyerere , unabaki unajiuliza hawa ndiyo wanaolilia Demokrasia hapa Nchini kweli,tukiwapa madaraka si watageuka kuwa kina Putin wa Bongo.
 
Breaking news:urusi yakinyakua kinu kikubwa cha nyuklia balani ulaya muda mfupu uliopita hichi kinu kipo ukraine. Putin anaendelea kugawa dozi
img_1_1646378764027.jpg
 
Pamoja na kuwa ni mdogo lakini anatumia akili zaidi na kaonyesha upinzani mkubwa tu kuliko adui anaepambana nae,Ukraine inazidiwa kwa kila kitu na Russia ndiyo maana wengi waliamini kabisa hii vita wenyewe humu wanaiita special operatiosn ingekwisha ndani ya msaa 24 tu,Lakini kinachoendelea tumeona hadi Mkubwa alipanic akataka atumie hadi Mabomu ya Nyuklia utadhani yeye angebakia salama kama angeyatumia.
Hivi ni Putin ndiye aliyesema kuwa operation hiyo ingechukua saa 24????!!! Watu naona mmeshiba mno propaganda za USA na magharibi kwa ujumla....game plan ya Russia kuhusu Ukraine ni tofauti kabisa...subirini muone
 
Kuichuku nchi nzima sio kitu rahisi kwa Strategy Anayoitumia Putin ya kubembeleza, Na ndio inampa hasara sana.

Uwepo wa watu katika battlefield Imekuwa advantage kubwa Sana kwa Ukraine, kutumia kama kinga kwao, Na kuwapa ugumu Russia kutupa mabovu kwa kunyatanyata.

Nazani wangesema raia wote wametoka, Nchi ingebaki tambalale.

Map of the progress of the special operation for March 3

View attachment 2138152
Unadhani kwanini basi watu hawatoki pamoja na kunyeshewa mnvua ya mabomu kila siku?
 
Usidharau Marekani. Wale watu wana personel ya watu wenye akili. Kama una exposure jaribu kujipenyeza kwenye taasisi za kati za USA au nchi washirika utanielewa.
Anadharau Marekani wakati leo akipewa Green Card ya kwenda kuishi huko anaweza hata kuukana uraia ili akaishi "American Dream"
 
Mkuu wewe darasani ulikuwa sio timu ya ubuyu na visheti!yaani unachambua mambo vizuri unaeleweka,Kuna wajinga wanachukulia hili suala Kama movie za Rambo,yaani hawaangalii impact za baada ya hii Vita itayoikumba dunia,wapo busy kuchekelea eti Putin mbabe,Wanamsifia mtu anaharibu atmosphere ya dunia kweli..Tanzania sisi na serikali yetu tunafanana akili zetu,dunia nzima imelaani hili suala sisi serikali inasema haina msimamo ,huku Wananchi wako wanampraise Putin akalie nchi ya mwenzie kimabavu,yaani hata sielewi akili zetu huwa Zina nini!
Taifa lina bahati mbaya sana ya kuwa na watu wengi wa hovyo, vilaza wenye akili kiduchu na mawazo finyu.
Poor us.
 
Anadharau Marekani wakati leo akipewa Grren Card ya kwenda kuishi huko anaweza hata kuukana uraia ili akaishi "American Dream"
😀😀😀. Nafikiri Ndo nchi inayoongoza kwa watu kutaka kuwa raia wake.
 
Back
Top Bottom