LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
IMG_20220306_130609_471.jpg
 
put

Aisee alafq wanaelewana lugha kabisa ,Putin anapigana na ndg zake kabisa huyu jamaa ni dictator wa kwelikweli.Aisee watasema na hii ni propaganda
Hapo Kuna mtu ame load bunduki yake huyo jamaa wa Urusi akaanza kulia kama mtoto... Aisee vita zingekuwa zinapiganwa na Wanasiasa
 
Asubuhi hii Kuna msafara mrefu sana wa Jeshi la Russia umeshambulia na uharibifu na Maisha mengi yamepotea nikipata video nitashare
 
Hahahahhahah huyo Veteran si yule wa Marekani?😅 Yule mwamba amekuwa muwazi tu kuwa sio marekani wala Nato ambao wanaweza simamisha battle na mrusi maana watapotea.

Yeye ni mstaafu na amekiri hilo, sasa humu wapuuzi wanavyoona Russia sijua anapondwa mara jeshi lake limefurumushwa wakati wameshakamata vinu vya Nyuklia viwili hapo Ukraine bado kimoja sijui story za mrusi kuzidiwa wanazito wapi!
Sio yule Colonel huyu alikuwa Surgent tu.. Ngoja nione namna na kuweka screenshot zake hapa..
Screenshot_20220306-130850_Twitter.jpg
screenshot_20220306-130939_twitter-jpg.2140949
Screenshot_20220306-131041_Twitter.jpg
Screenshot_20220306-131137_Twitter.jpg
Screenshot_20220306-131159_Twitter.jpg
Screenshot_20220306-131241_Twitter.jpg
Screenshot_20220306-131314_Twitter.jpg
Screenshot_20220306-131338_Twitter.jpg
Screenshot_20220306-131429_Twitter.jpg


Screenshot_20220306-130939_Twitter.jpg
 
Kuna majamaa wanadai urusi anaenjoy show , but in reality ni disaster , tatzo ni kuwa urusi ni Taifa maskini tuu tofaut na tunavyoaminishwa humu ....!!! Ukraine ni underdog Sana , but resistance Yao dhidi ya taifa linalodai ni la Kwanza in term of millitary , ni surprise
Mkuu urusi hajaamua kumpiga Ukraine, anachofanya anamlazimisha rais wa ukrane akubali, ndo maana hujaona modern weapons zikifanya kazi.
 
Tukiachana na nuclear weapons, siwezi panga majeshi bora ya conventional weapons Urusi ikawepo kwenye top 4. Huwezi kuwa na jeshi la ovyo la ardhini na angani linaposhindwa kupigana na vijeshi vidogo kama Ukraine alafu unataka tukuite superpower kwenye majeshi. Ujerumani kwenye WW2 ilipigana na Poland, Ufaransa, Urusi, Marekani na Uingereza ikiwa pamoja na Commonwealth zake zenye nchi imara kama New Zealand, Australia na Canada, et. Hata South Africa ilishiriki dhidi ya Mjerumani, hao ndio walikuwa na jeshi la kupigana na maadui wengi sio hii Russia.

Huu uzi nimeutelekeza kwa siku tatu hizi baada ya kuona kile ninachokijua kimezidi kupwaya. Jeshi la anga la Urusi ndio la kufanya mashambulizi usiku ili lisidondoshewe ndege zake kweli? Juzi ndege 6 ziko confirmed kuangushwa, source zipo nyingi za kudhitibisha hilo na ndege ambazo hakuna uhakika hazijahesabika. Wiki ya pili sasa bado Ukraine imesimamisha S-300 zinafanya kazi. Ingekuwa Israel siku ya kwanza tu, trust me siku ya kwanza tu hakuna air defence system ungeona iko kazini!

Urusi inashindwa kulinda convoy zake, inapaki magari kibao mpakani kule Belarus ila inaogopa kuingia nayo mengi ziko Bayraktar TB2 zinayasubiri, hawana air cover wanaenda as if tuko 1980s. Urusi wana systems zao kama S-300 (S-400 si rahisi ikaletwa kufanya kazi ndogo hizi) ziko mbali uko kwao ambavyo wala Ukraine hana mpango wa kuishambulia Urusi hivyo zinatoa air cover mpaka pembeni mwa Ukraine ila nao wanaendesha ndege level za chini kukwepa radar.

Russia haina coordination nzuri ya airstrikes, artillery na troops. Hata airforce yao haina uzoefu na combat missions, Urusi wako busy na kuendesha ndege kwenye maonesho na kwenye mazingira rafiki wakati NATO wanakuwa na mazoezi magumu yanayofanyika kwenye maeneo tofauti duniani kama Mediterranean sea, Marekani na maeneo ya Ulaya. Marubani wa UK na US hukutana kufanya mazoezi magumu kila mwaka yanaitwa 'Red flags', hutumia makombora ya kisasa, ndege za kisasa na hutumia hali ya hewa mbovu kwenye mvua kubwa, fog na upepo. Last year mwishoni hapo kuna F-35 mpya ya Uingereza ilidondokea kwenye maji wakiwa kwenye mazoezi makali na Marekani. Marubani wa NATO wana simulation rooms za kisasa zinazofanana na mazingira halisi ya vitani, rubani anapewa simulator inayofanana kila kitu na ndege yenye hata VR anazoea mazingira, buttons, emergencies, maamuzi ya haraka. Hata movements za ndege, acrobatics na mitikisiko anapewa anachokosa ni ile hofu inayotofautisha mazoezi na reality. Russia hana kampuni ya kutengeneza modern simulators marubani wake wana disadvantage hapa. Marubani wa Russia wakifanikiwa sana wanatimiza masaa 100 ya kurusha ndege kwa mwaka wakati Marekani na members wakubwa wa NATO wa kwao wanazidi masaa 200 kwa mwaka.

Ndege za Urusi zingekuwa mbovu India isingekuwa inazitumia vizuri na kushinda angani, tena India iliwahi fanya mazoezi na members wa NATO wakakubali sana uwezo wake. India ndio airforce inayoongoza kupata ajari, wale jamaa hawakai miezi miwili bila ndege ya jeshi kuanguka, kamanda wa jeshi la anga alidai bora wafanye mazoezi kwenye mazingira magumu wafe kwenye wakati wa amani ila vita ikija wawe strong wafanye mission kwenye mazingira yote.

Hapa tatizo ni training mbovu isiyokidhi, na washirika wa Urusi hawafanyi mazoezi pamoja. Russia inafanya mazoezi na India, China kidogo sana na watu wa kawaida kama Belarus. NATO wanaunganisha mbinu za wageni kama South Korea, Japan na Israel which I think ndio airforce inayojua sana air warfare kuliko hapa duniani. Israel imeanza operations Syria miaka zaidi ya 10 na sijawahi sikia imepoteza ndege hata moja. Leo hii Urusi ndani ya wiki mbili ana hasara kibao angani.
 
Back
Top Bottom