Mkuu vita ya Ukraine imetufunulia mengi tulivyokua tunadanganywa.
Urusi peke yake inapigana na silaha dhidi ya jeshi linalopewa silaha Bora kabisa kutoka nchi tulizoambiwa ni nchi zenye tech ya Hali ya juu sana ya silaha,yaani nchi zote za west.
Achilia mbali silaha pia Ukraine imekua ikipewa mafunzo Bora kabisa kutoka nchi tulizokua tuliambiwa ni nchi Bora kijeshi hapa duniani,yaani nchi ya USA na NATO yake.
Sio TU silaha Bora na mafunzo Bora,Bali Ukraine imekua ikipata ushauri kutoka Kwa makammanda Bora kabisa wa USA,UK,FR, German NATO wengine.
Lakini muhimu zaidi ambacho Ukraine amekua akipata ni huduma za satellite za kijeshi na za kiraia kutoka nchi zote za west kwa ajili ya kuonesha mienendo ya jeshi la Urusi.
Na zaidi kuliko yote ni huduma za kiintelijensia.
Ukraine imepata faida kubwa sana ya misaada ya intelijensia kutoka mashirika ya kijasusi ya kijeshi na kiraia kutoka nchi zinazosifika katika tasnia hiyo ambazo ni USA,UK, German,fr, na NATO wengine.
Lakini Cha ajabu Urusi peke yake imeweza kuwadhibiti kabisa licha ya misaada yote hiyo.
Dunia inashihudia Yale iliyokua haiyajui.