Wewe jamaa ni muongo sana, NATO iliundwa kukabiliana na vitisho vya USSR na sio Russia,( Russia ilikuwa miongoni mwa nchi 14 washirika wa USSR) usiipaishe sana Russia hatakama unaihusudu,
2) Russia kuwa na mabomu mengi ya nuclear haimaanishi kuwa USA au nchi za magharibi haziwezi kuongeza huo uzalishaji, nivile sheria za kimataifa zinafuatwa, alafu haiitaji mabomu mengi ya nuclear kumaliza vita, hiyo ni namba tu kiufupi ukipiga bomu Moja la nuclear pale New York madhara yake ni makubwa mnoo.
3, unavyosema NATO wanaiogopa Russia sio kweli, NATO wameshavuka mstari mwekundu uliowekwa na Russia na Putin hajafanya lolote, kama unajua Simba ni mkali yanini uanze kumchokonoa? Kila mara NATO wanaichokoza urusi na hatuoni lolote linalofanywa na Putin, angesambaratisha basi hizo kambi za USA kule ulaya, tusiongee ushabiki muda mwingine
Majibu mheshimiwa speaker.
1. Kila himaya huwa inakuwa na watu na mji unaoibeba roho ya himaya.
Kwa Waturuki enzi hizo ikiitwa Himaya Athuman mji muhimu kwao ni Instanbul.
Je Himaya ya Kirusi na Usoviet mji upi unabeba roho ya Himaya? Ingushetia au Kazan?
Ndio unagundua roho ya Kirusi ipo Moscow na Muscovites kama watu ndio mpaka Sasa wanaitawala Shirikisho la Urusi?
2. Mabomu ya kinyuklia
Nikuweke wazi tu, hii ni moja ya sababu Western world will have to think thrice before any attempt ya kushambulia Urusi.
Kumbuka haya majamaa Yana black hand kama utafanikiwa kuwa wa kwanza kunishambulia na kuwaua wote.
Hawatojaribu hata iweje, nani anataka kubondwa na mionzi isiyo mithilika? Wataishia kubweka.
3.Vinchi 32 vinahanya kushambulia, ujue Kuna namna wanahofia kama angekuwa dhaifu angepigwa.
Kumbuka haka kamuungano kao
German kapigwa
Ufaransa kafumuliwa zaidi ya mara moja.
Poland katandikwa
Finland kazabwa
Uturuki katembezewa
Japan kipo kilichompata mpaka kunyang'anywa Visiwa vya Sakhalin
Lithuania kaingiliwa
Hivyo wanamjua vilivyo kiboko yao, tumaini pekee lililobaki ni Urusi ivunjike yenyewe tu.
NATO hawajaingia sawa, sisi hatukatai maana wale volunteer wanatokea mbagala, swali muhimu Urusi katangaza vita au kaingiza jeshi lake lote kwenye huo mgogoro