Narumu kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 1,888
- 4,489
Hapo hamna kitu kipya hizo teknolojia zipo tangu miaka ya 1980s.Inavyoshuka ni km mwanga wa Radi au imetoka sayar nyingine kupiga duniani
Multiple Independent Reentry Vehicles (MIRVs) zipo kwa makombora mengind ya Urusi, Marekani na nchi chache. Nchi ya kwanza kutengeneza MIRVs ni Marekani ambayo kutokana na mkataba wa silaha za nyuklia START II Marekani ilipanga kuachana na MIRVs 2014, ingawa haizuii kuendelea. Hata Urusi kuna muda waliacha na sasa ndio wakitaka waendelee.
Kuhusu silaha kuzuilika. Urusi yenyewe ina makombora ya tangu 1970s ambayo ukiwaambia wayafyatue kisha wayadungue kwa mifumo yao ya 2020s hawawezi. Missile tech inaenda kwa kasi zaidi kuliko anti-missile tech. Kutengeneza sumu ni rahisi sana kuliko kutengeneza dawa ya sumu. Urusi haina mfumo wa kuzuia ICBM hata liwe la Pakistan.