SPEEDAF Carrier na uhuni wenu wa kitoto mnaotufanyia

Kuna mwamba yoyote aliewai kufanya ivi, iyo kutoka Aliexpress, inaitwa china to china
 
Wadau wa manunuzi online aliexpress ...ivi nikinunua hii bidhaa [emoji116][emoji116] makadirio ya kodi ya VAT ita vhargiwa kama bei gan ivi.
Bei yake ni kama 122090 Tsh ktk mtandao ..je hesabu za kodi ya VAT yanapigwa vipi hapo
Sio kila mzigobunalipia kodi, ila ukitakiwa kulipa kodi haitakua chini ya 43%. Chukua gharama ya bidhaa bila usafiri alafu zidisha kwa 0.43 utapata kodi ya kulipia.
 
Mkuu, hivi naweza kuwatumia speedaf kwenye alibaba?
Na wanacharge vipi shipping fees, wanatumia uzito au CBM?
 
Tatizo watu wote wanalalamika kuhusu kupotea mizigo yao ila hakuna aliewahi shtaki mahakamani ili upate hela ndefu, tatizo Nini haswa?
 
Mimi miaka mitano na ushee kidogo, tokea nianze hizi mishe naishia kupokea tu kupitia posta.. Na nachagua shipping method zaidi ya moja, sometimes free cainiao, standard shipping lakini chaa ajabu ndio hivyo sina maajabu.

Sijawahi kuletewa na spidaf hata siku moja... Siku moja nikaja kulizua nikaona labda kwenye address lile box la posta linaniponza, nikaamua kulitoa/kulifuta ili nije kutarajia niletewe na spidafuu.. Kilichonikuta mzigo niliufatia makao makuu posta pale kuna kitengo cha TRA nikakandamizwa na kodi. Sasa nimeona nitulie tu niangalie chochoro zengine.
 

Mzigo toka tarehe 4 upo ofisini kwao mpaka tarehe 11 ndio umetoka, na hio Tarehe 11 jamaa katulia sehemu hajaleta mzigo, ukimpigia hapokei, then kaurudisha na sababu imeandikwa mpokeaji ameomba uletwe siku nyengine. Hawa jamaa wanawaharibia wenzao biashara.

Mzigo toka China hadi Tanzania unatumia muda mchache kuliko toka Ofisi zao hadi kwa mteja, hivi hakuna pa kuwaripoti?
 
Speedaf wana official website unaweza pia kuripoti huko kuhusu huyu wakala wao wa Tanzania.
 
Sasa hapo mbona simple?

Aliye confirm as received by me huyo ndiye atajua hajui maana for now inakuletea mpaka namba ya muhusika aliye confirm sasa hapo tunaachanaje kwa mfano?

Kuwa na amani ndugu, hakuna kupoteza kitu hata kama ni cha buku.
 
Refund unapewa depending na fault ipo wapi hata kama ulishapokea mzigo

Nimepata Refund Juzi kati Hapo..nilipokea mzigo lakini product haifanyi kazi nikadai refund na evidence nikawapa wakarudisha pesa yangu kiroho safi
Naomba kufahamu....Hivi hapo kwenye refund manake unapiga picha bidhaa kuwa ni fake(Tafsiri kama haifanyi kazi vizuri) kwa huyo muuzaji atakurudishia hela au product mpya
 
Samahani naomba kufahamu mambo haya mawili
1.Mzigo posta mda maximum wakukaa ni muda ganii????
2.Waweza mtuma mtu akuchukulie mzigo posta
 
Wazee mpaka hapo kuna ulazima wa kusubiri tena nipigiwe simu au niwafate huko huko mwenyewe nikajichukulie changu mapema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…