Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Spika Anne Makinda ambapo kuukwaa uspika ilibidi "awezeshwe" na JK kupitia rafu kibao sasa ameonyesha hana sifa wala uzoefu wa kuliongoza Bunge hili ndani ya utamaduni wa vyama vingi.
Tatizo alilonalo ni kuwa yumo kwenye kundi dogo ndani ya CCM ambalo linaona nchi haifai kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi na hivyo kufanya jitihada za siri na wazi kuuvuruga na kuleta shari ambazo siyo za lazima.
Baadhi ya mapungufu yake ni pamoja na:-
1) kukemea wabunge wa upinzani kama vile ni watoto wadogo na kuwakalisha chini nyakati ambapo hutoa michango yao. Yeye anasahau jinsi Sitta alivyokuwa "akimkwida sketi" yake hata alifikia hatua ya kulalamika kuwa ananyanyaswa sasa sijui haya ndiyo malipizi yake?
2) Kuzuia wapigakura kuwatathmini utendaji wa wabunge wao kupitia luninga. Huu nao ni upungufu wa kudhani demokrasia ni kuwachagua viongozi lakini siyo kuwapima utendaji wao. Hivi baada ya miaka mitano mpigakura atajuaje anavyowakilishwa kama mijadala ya bungeni ni siri yao wenyewe?
3) Upigaji wa kura ndani ya Bunge na kamati zake ni siri kubwa sasa mpigakura anapotakiwa kushiriki uchaguzi na amenyimwa taarifa za kuwapima wabunge atafanyaje maamuzi ya busara?
4) Kuvunja kamati kinyume na maelekezo ya kanuni na hili pekee linatosha kwa wabunge kumpigia kura ya kukosa imani naye na kumng'oa maana sasa hata kanuni haziheshimu ambazo ndiyo msingi wake wa kulisimamia Bunge.
5) Kukataza picha za wabunge wanapouchapa usingizi Bungeni zisipigwe na kuwaelimisha wapigakura juu ya udhaifu wa uwakilishi tajwa. Spika Makinda anafanya hivyo kuwalinda wabunge wa chama chake ambao kwa kuuchapa ndio maarufu kabisa.
6) Kupitisha miswaada kwa kutumia sauti na hata yeye mwenyewe hufikia mahali na kusema;-......" nafikiri waliosema ndiyo wameshinda....."..................ikimaanisha hata yeye hana uhakika kama maamuzi yake ni sahihi ili mradi kulinda masilahi ya serikali ya chama chake.
7) Kufutilia mbali khoja binafsi na hivyo kulinyima Bunge uwezo wake wa kuisimamia serikali. Inawezekana khoja binafsi baadhi yake hazina mashiko lakini ni vyema kwenye kamati husika ndipo kura zipigwe na kuamua hivyo badala ya yeye kuwa hakimu kwenye kesi yake mwenyewe.
8) Kuzidhalilisha kamati za Bunge kwa kuziingilia kwenye maeneo yao. Mfano pale ambapo huunda kamati kufanya kazi ambazo kamati zipo kulingana na mujibu wa kanuni. Mara nyingi hufanya hivyo kulinda serikali kwenye mapungufu yake na hivyo kumfanya Spika kuwa kioja kwenye taswira nzima ya maana halisi ya kikatiba ya Bunge kulisimamia Serikali.
9) Uteuzi wa watendaji ndani ya Bunge akiwemo Katibu wa Bunge hauzingatii taratibu za ajira ya watumishi wa umma kwa maana ya kushirikisha wananchi na vyombo husika na matokeo yake watendaji ndani ya Bunge nao wameingiwa na hulka ya ushabiki wa chama tawala.
10) Kuunganishwa kwa kofia za Uspika na Ujumbe wa kamati kuu ya CCM pia kunampunguzia Spika uhuru wa kufanyakazi yake bila upendeleo kwa chama chake kilichompa ugali kupitia "mbeleko" tata. Ni vyema katiba mpya ikatamka wazi ya kuwa wabunge na watendaji wote Bungeni akiwemo Spika na wasaidizi wake hawapaswi kushika nyadhifa zozote ndani ya vyama vya siasa ili kuleta mazingira ya kutenda haki.
Kwa mtazamo wangu hatua zichukuliwe za kumwondoa Spika Anne Makinda kwenye kiti chake ili kutoa funzo ya kuwa cheo ni dhamana tu na wala siyo mtaji wa kujijenga kisiasa ndani ya chama chake cha siasa.................