Spika Anne Makinda sasa analiendesha Bunge KIIMLA!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Spika Anne Makinda ambapo kuukwaa uspika ilibidi "awezeshwe" na JK kupitia rafu kibao sasa ameonyesha hana sifa wala uzoefu wa kuliongoza Bunge hili ndani ya utamaduni wa vyama vingi.

Tatizo alilonalo ni kuwa yumo kwenye kundi dogo ndani ya CCM ambalo linaona nchi haifai kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi na hivyo kufanya jitihada za siri na wazi kuuvuruga na kuleta shari ambazo siyo za lazima.

Baadhi ya mapungufu yake ni pamoja na:-

1) kukemea wabunge wa upinzani kama vile ni watoto wadogo na kuwakalisha chini nyakati ambapo hutoa michango yao. Yeye anasahau jinsi Sitta alivyokuwa "akimkwida sketi" yake hata alifikia hatua ya kulalamika kuwa ananyanyaswa sasa sijui haya ndiyo malipizi yake?

2) Kuzuia wapigakura kuwatathmini utendaji wa wabunge wao kupitia luninga. Huu nao ni upungufu wa kudhani demokrasia ni kuwachagua viongozi lakini siyo kuwapima utendaji wao. Hivi baada ya miaka mitano mpigakura atajuaje anavyowakilishwa kama mijadala ya bungeni ni siri yao wenyewe?

3) Upigaji wa kura ndani ya Bunge na kamati zake ni siri kubwa sasa mpigakura anapotakiwa kushiriki uchaguzi na amenyimwa taarifa za kuwapima wabunge atafanyaje maamuzi ya busara?

4) Kuvunja kamati kinyume na maelekezo ya kanuni na hili pekee linatosha kwa wabunge kumpigia kura ya kukosa imani naye na kumng'oa maana sasa hata kanuni haziheshimu ambazo ndiyo msingi wake wa kulisimamia Bunge.

5) Kukataza picha za wabunge wanapouchapa usingizi Bungeni zisipigwe na kuwaelimisha wapigakura juu ya udhaifu wa uwakilishi tajwa. Spika Makinda anafanya hivyo kuwalinda wabunge wa chama chake ambao kwa kuuchapa ndio maarufu kabisa.

6) Kupitisha miswaada kwa kutumia sauti na hata yeye mwenyewe hufikia mahali na kusema;-......
" nafikiri waliosema ndiyo wameshinda....."..................ikimaanisha hata yeye hana uhakika kama maamuzi yake ni sahihi ili mradi kulinda masilahi ya serikali ya chama chake.

7) Kufutilia mbali khoja binafsi na hivyo kulinyima Bunge uwezo wake wa kuisimamia serikali. Inawezekana khoja binafsi baadhi yake hazina mashiko lakini ni vyema kwenye kamati husika ndipo kura zipigwe na kuamua hivyo badala ya yeye kuwa hakimu kwenye kesi yake mwenyewe.

8) Kuzidhalilisha kamati za Bunge kwa kuziingilia kwenye maeneo yao. Mfano pale ambapo huunda kamati kufanya kazi ambazo kamati zipo kulingana na mujibu wa kanuni. Mara nyingi hufanya hivyo kulinda serikali kwenye mapungufu yake na hivyo kumfanya Spika kuwa kioja kwenye taswira nzima ya maana halisi ya kikatiba ya Bunge kulisimamia Serikali.

9) Uteuzi wa watendaji ndani ya Bunge akiwemo Katibu wa Bunge hauzingatii taratibu za ajira ya watumishi wa umma kwa maana ya kushirikisha wananchi na vyombo husika na matokeo yake watendaji ndani ya Bunge nao wameingiwa na hulka ya ushabiki wa chama tawala.

10) Kuunganishwa kwa kofia za Uspika na Ujumbe wa kamati kuu ya CCM pia kunampunguzia Spika uhuru wa kufanyakazi yake bila upendeleo kwa chama chake kilichompa ugali kupitia
"mbeleko" tata. Ni vyema katiba mpya ikatamka wazi ya kuwa wabunge na watendaji wote Bungeni akiwemo Spika na wasaidizi wake hawapaswi kushika nyadhifa zozote ndani ya vyama vya siasa ili kuleta mazingira ya kutenda haki.

Kwa mtazamo wangu hatua zichukuliwe za kumwondoa Spika Anne Makinda kwenye kiti chake ili kutoa funzo ya kuwa cheo ni dhamana tu na wala siyo mtaji wa kujijenga kisiasa ndani ya chama chake cha siasa.................

Makinda ni mchapa kazi na anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na sheria za bunge. Mengine yote ni tisa.

zomba kama una khoja ya kumbeba basi fafanua khoja zako vinginevyo unaleta ushabiki wa kisiasa..................Huyu mama kazi imemshinda kabisa......
 
Makinda ni mchapa kazi na anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na sheria za bunge. Mengine yote ni tisa.
Rutashubanyuma kaweka vielelezo kibao vya kuonyesha kwamba Makinda hana uwezo, wewe unakuja na sentensi moja tu ya kusema anaweza bila ya kufafanua hoja zilizoletwa na mtoa mada. Huu nao ni mfano wa uwezo mdogo wa wanaCCM kuchambua mambo. Matatizo makubwa kama ya ukosefu wa democrasia bungeni mnayasolve kwa kufuta kuonyesha bunge live. Huo ni wehu. Kama ni hivyo bora na sisi wananchi tugome kuwapigia kura wabunge.
 
Last edited by a moderator:

Lukolo tatizo la zomba ni ushabiki ambao unapofua hata ukweli na kushikilia jambo ambalo linaiathiri nchi...............nchi ni kubwa kuliko chama cha siasa ndilo ambalo hawafahamu.
 
Akufukuzaye hakwambii toka, ile mvua ya sms iliyomnyeshea ni dalili tosha kuwa hatakiwi na akisubiri kutolewa mengi yatamuandama

Halafu anaishia kulalamika tu anatukanwa bila kufikiria kwanini anatendewa hivyo.
Infact,mimi nakubaliana na wazo kuwa:
1/Spika wa bunge asitokane na vyama vya siasa,bali awe ni proffesional aliye bobea katika masuala ya sheria.
Hii itaondoa maamuzi ya kibabe ya kutofuata sheria na kanuni za kuongoza bunge just because of ignorancy.
2/Jina la spika lipatikane baada ya nafasi hiyo kutangazwa,na watu kufanya application na kuwa approved na senate itakayo undwa na jopo la wataalamu wa sheria na masuala ya bunge.
 
Hivi kwenye hili suala kiini cha tatizo ni Makinda?

Unadhani Makinda akitolewa na hiyo nafasi kuchukuliwa na mbunge wa Temeke au Korogwe basi mambo yatakuwa fresh?

Ninawashangaa sana watu wanaotaka Makinda ajiuzulu as if akifanya hivyo basi bunge iltakuwa safi.
 
Well said
 
Mkuu EMT,
Kila kiongozi anawajibika kwa matendo yake anapo kuwa kiongozi.
Mtoa mada ametoa details jinsi Makinda anavyo boronga.
The fact kwamba ameboronga,inatosha kumwajibisha,au kumsababisha awajibike,bila kujali spika ajaye atakuwaje,kwani kuna potentials wengi tu miongoni mwa wabunge wanao weza kufanya vyema kazi ya spika vizuri kuliko Anne Makinda.
 
Mpenda Yesu yote naafiki isipokuwa kumtusi mama wa watu!
 
Hivi kwenye hili suala kiini cha tatizo ni Makinda?

Unadhani Makinda akitolewa na hiyo nafasi kuchukuliwa na mbunge wa Temeke au Korogwe basi mambo yatakuwa fresh?

Ninawashangaa sana watu wanaotaka Makinda ajiuzulu as if akifanya hivyo basi bunge iltakuwa safi.

EMT mwizi ukimkamata itabidi umwachie kwa sababu hawezi kuzuia wengine wasiibe eti kwa sababu umemfunga.............sijaona reasoning ambayo is cockeyed than this.....................impunity must be punished and provide an act of deterrence
 
Mkuu EMT,
Kila kiongozi anawajibika kwa matendo yake anapo kuwa kiongozi.
Mtoa mada ametoa details jinsi Makinda anavyo boronga.
The fact kwamba ameboronga,inatosha kumwajibisha,au kumsababisha awajibike,bila kujali spika ajaye atakuwaje,kwani kuna potentials wengi tu miongoni mwa wabunge wanao weza kufanya vyema kazi ya spika vizuri kuliko Anne Makinda.

Mpenda Yesu kwenye hili tuko sote.................aluta continua
 
Akufukuzaye hakwambii toka, ile mvua ya sms iliyomnyeshea ni dalili tosha kuwa hatakiwi na akisubiri kutolewa mengi yatamuandama

Inkoskaz hii sasa ni aibu ya JK kuchakachua mambo ambayo hayafai kuchakachua.................labda wangelimwacha Mzee Sitta amalizie kipindi chak mambo yangelikuwa ahueni maana yeye alikuwa ni mtu wa viwango .....huyu mama yeye ni bora liende tu
 
Mkuu EMT,
Kila kiongozi anawajibika kwa matendo yake anapo kuwa kiongozi.
Mtoa mada ametoa details jinsi Makinda anavyo boronga.
The fact kwamba ameboronga,inatosha kumwajibisha,au kumsababisha awajibike,bila kujali spika ajaye atakuwaje,kwani kuna potentials wengi tu miongoni mwa wabunge wanao weza kufanya vyema kazi ya spika vizuri kuliko Anne Makinda.

Kwa hiyo kiini cha tatizo ni Makinda?
 
EMT mwizi ukimkamata itabidi umwachie kwa sababu hawezi kuzuia wengine wasiibe eti kwa sababu umemfunga.............sijaona reasoning ambayo is cockeyed than this.....................impunity must be punished and provide an act of deterrence

Unless you address the underlying cause ya watu kuiba utajaza magereza kwa kufunga watu wezi na kujenga mengine mapya.

Is that what you really want to do?

Kwa nini tunapenda sana ku-avoid the underlying causes of our problems?

Kwa nini tunapenda sana kutumia short cuts to address our fundamental problems?

Kweli udhani kabisa tatizo hapa ni Makinda na akiondolewa kwenye kiti cha uspika basi mambo yatakuwa super? Really?
 
Kwa hiyo kiini cha tatizo ni Makinda?

Makinda aliwekwa pale kwa maslahi ya watawala,bila kuzingatia weledi na uwezo wake kiuongozi,kwa kigezo kwamba yeye ni mwanamke na ni wakati wa bunge kuongozwa na spika mwanamke!
Despite the weakness ya kwenye mfumo mzima wa bunge,spika aliyepita,Samuel Sitta alijitahidi kuongoza bunge kwa kufuata kanuni na sheria.
Ni kweli,Makinda pia ni kigezo kikubwa cha kuporomoka kwa kasi kwa ufanisi wa bunge hili mkuu EMT.
 
Mpenda Yesu Makinda is beyond correction she has to go, abinitio!
 
Hata kama mie sio mtalaamu sana katika masuala ya Bunge na Sheria, lakini tatizo la msingi kwangu naona sio Makinda bali Kanuni za Bunge. Labda kinachokosekana kwa Mama Anne Makinda ni ukosefu wa kutumia busara...kwamba, kila wakati anataka kutumia Kanuni za Bunge hata sehemu ambapo pengine busara ingetumika zaidi.
 
Back
Top Bottom