Kama hakutakuwa na mabadiriko yeyote, basi tarehe 25 February 2014, siku ya Jumanne, mpaka kufika saa kumi na mbili jioni watanzania na Dunia itakuwa imemjua Spika wa Bunge la Katiba mpya ya nchi yetu.
Wajumbe wa Katiba mpya wameishateuliwa, na jana wameripoti Bungeni, tayari wameishamchagua Mwenyekiti wa muda ambaye atasimamia mchakato wa kumpata Spika wa Bunge ambaye ataendesha vikao vyote vya kuipata Katiba mpya.
Mpaka hivi sasa kumejitokeza majina mawili yanayotajwa tajwa sana ktk mchakato wa kuwania kiti hicho. Majina hayo ni la Mhe. Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mwingine ni Mhe. Andrew Chenge, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kuingia ktk siasa na baadae kuteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu. Mhe. Chenge al maarufu kwa jina la "vijisenti" alilazimika kujiuzuru ktk wadhifa wa Uwaziri kwa kashfa ya Rada.
Mhe. Chenge na Mhe. Sitta wote ni wanasheria kitaaluma, wote wanatoka kanda ya ziwa. Ila wanatofautiana kimitizamo. Wakati Mhe. Sitta anaongoza kundi la watanzania wanaopinga ufisadi nchini, Mhe. Chenge yeye ni mhanga wa ufisadi kutokana na kashfa ya Rada. Kundi hili inasemekana linaunga mkono hoja ya mfumo wa Serikali tatu. Taarifa kutoka viunga vya mji wa Dodoma vinadai kuwa, katika kampeni hii Mhe. Chenge anabebwa na kundi la Mhe. Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya Richmond, huku Mhe. Sitta akiungwa mkono na kundi la Mhe. Membe, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kundi hili linaunga mkono hoja ya Serikali mbili zilizopo hivi sasa, ila linataka kero za Muungano zitafutiwe dawa ya kudumu.
Sababu ya kuleta hoja hii hapa ni kutaka kutoa fursa kwa watanzania wanaoipenda nchi yao kutoa maoni yao juu ya mchakato huu wa Katiba mpya na bila kumsahau Spika atakayeliongoza Bunge litakalotuletea "KITABU" kitakacho tutawala kwa kipindi kirefu cha maisha yetu.