Spika Bunge la Katiba: Mchuano ni kati ya Sitta na Chenge

Spika Bunge la Katiba: Mchuano ni kati ya Sitta na Chenge

Kama hakutakuwa na mabadiriko yeyote, basi tarehe 25 February 2014, siku ya Jumanne, mpaka kufika saa kumi na mbili jioni watanzania na Dunia itakuwa imemjua Spika wa Bunge la Katiba mpya ya nchi yetu.

Wajumbe wa Katiba mpya wameishateuliwa, na jana wameripoti Bungeni, tayari wameishamchagua Mwenyekiti wa muda ambaye atasimamia mchakato wa kumpata Spika wa Bunge ambaye ataendesha vikao vyote vya kuipata Katiba mpya.

Mpaka hivi sasa kumejitokeza majina mawili yanayotajwa tajwa sana ktk mchakato wa kuwania kiti hicho. Majina hayo ni la Mhe. Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mwingine ni Mhe. Andrew Chenge, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kuingia ktk siasa na baadae kuteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu. Mhe. Chenge al maarufu kwa jina la "vijisenti" alilazimika kujiuzuru ktk wadhifa wa Uwaziri kwa kashfa ya Rada.

Mhe. Chenge na Mhe. Sitta wote ni wanasheria kitaaluma, wote wanatoka kanda ya ziwa. Ila wanatofautiana kimitizamo. Wakati Mhe. Sitta anaongoza kundi la watanzania wanaopinga ufisadi nchini, Mhe. Chenge yeye ni mhanga wa ufisadi kutokana na kashfa ya Rada. Kundi hili inasemekana linaunga mkono hoja ya mfumo wa Serikali tatu. Taarifa kutoka viunga vya mji wa Dodoma vinadai kuwa, katika kampeni hii Mhe. Chenge anabebwa na kundi la Mhe. Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya Richmond, huku Mhe. Sitta akiungwa mkono na kundi la Mhe. Membe, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kundi hili linaunga mkono hoja ya Serikali mbili zilizopo hivi sasa, ila linataka kero za Muungano zitafutiwe dawa ya kudumu.

Sababu ya kuleta hoja hii hapa ni kutaka kutoa fursa kwa watanzania wanaoipenda nchi yao kutoa maoni yao juu ya mchakato huu wa Katiba mpya na bila kumsahau Spika atakayeliongoza Bunge litakalotuletea "KITABU" kitakacho tutawala kwa kipindi kirefu cha maisha yetu.
 
mkuu umechanganya hoja zako. tafadhali hebu weka wazi ni kundi lipi linlotaka serikali 2 na lipi needs 3.
 
Mhe. Sitta anaongoza kundi la watanzania wanaopinga ufisadi nchini, (1)Mhe. Chenge yeye ni mhanga wa ufisadi kutokana na kashfa ya Rada. (2)Kundi hili inasemekana linaunga mkono hoja ya mfumo wa Serikali tatu. (2)Kundi hili linaunga mkono hoja ya Serikali mbili zilizopo hivi sasa, ila linataka kero za Muungano zitafutiwe dawa ya kudumu.
Ukiangalia highlight za rangi nilizoweka utagundua kuna tatizo kwa kila kundi kwa upande hasa kwa wanachama wa CDM....1) upande wa rangi nyekundu CDM wanaunga namba (2)
2) Upande wa rangi ya kijani CDM wanaunga namba (1)

Sasa je hawa wajumbe wa CDM watampigia nani hapo??? Ni kwa nini hawasimamishi mtu wao au ndo hakuna mwelewa wa masuala ya sheria ukiachilia mbali Tundu L..?????

Anyways tukiacha masihala Mh Sitta anafaha sanaaa tena sanaaa...
 
Mbona wote ni ccm? Ina maana cdm hawana watu wenye uzoefu
 
Kazi ipo, sina hamu na Tanzania hii hata waseme serikali kumi sawa tu.
 
Ukiangalia highlight za rangi nilizoweka utagundua kuna tatizo kwa kila kundi kwa upande hasa kwa wanachama wa CDM....1) upande wa rangi nyekundu CDM wanaunga namba (2)
2) Upande wa rangi ya kijani CDM wanaunga namba (1)

Sasa je hawa wajumbe wa CDM watampigia nani hapo??? Ni kwa nini hawasimamishi mtu wao au ndo hakuna mwelewa wa masuala ya sheria ukiachilia mbali Tundu L..?????

Anyways tukiacha masihala Mh Sitta anafaha sanaaa tena sanaaa...

Mkuu hebu soma hiyo mada vizuri maana aliyeieeka kajichanganya sana na wewe ikaingia kwenye huo mtego.
 
tungeweza kutofautisha vyama vya siasa na mchakato wa katiba mpya tungefanikiwa sana.
yaani natamani wangejisahaulisha kuhusu siasa nawakajikita katika kutengeneza katiba bora.
 
Hebu fikiria kama wote tutakuwa na na maoni ya kukata tamaa namna yako hii nchi nani ataikpmboa?

Mkuu kweli umenisoma vizuri sana, ukweli nimekata tama, sioni mwanga kabisa hasa kwa kizazi kijacho. Kila harakati ya kujikomboa inakatishwa tamaa sana. Rasilimali kama za gas na mafuta zitasaidia kitu?? Madini yalishindwa tumebaki na handaki na watu kufukuzwa katika mashamba au ardhi zao wapishe wachimbaji na wamezidi kudidimia!!! So sad, lost hope!!
 
Vijisenti= Rada
Sita=Kasi na viwango. Viwango havifui dafu kwa vijisenti.
 
Mleta mada umepika taarifa hizi. Wagombea wote hao ni CCM na wote wanatetea hoja ya serikali mbili ambayo ndiyo sera rasmi ya CCM na inapigiwa debe na makundi yote ndani ya CCM.

Sio Chenge wala Lowassa aliyewahi kuunga mkono hoja ya serikali tatu toka mchakato wa kutungwa kwa katiba mpya kuanza.

Ni Samweli Sitta ndiye aliyewahi kuonyesha kuridhishwa na uzito wa hoja za uwepo wa serikali tatu kwenye rasimu lakini bado alikataa kuunga mkono uwepo wa serikali tatu.

Sio Sitta wala Chenge mwenye nia ya dhati ya kuwa fair kama atakuwa spika wa bunge la Katiba, wote wanakwenda kutetea maslahi ya CCM kwanza.

Binafsi ningependa kuona Spika wa Bunge hili anakuwa sio mwanasiasa(Mtu Ambaye hawakilishi chama) na ikishindikana basi atoke kwenye Chama cha siasa kisicho na Nguvu.
 
Hivi Chenge ni mtu wa aina gani? He keeps on political arena despite the fact that he is alleged of being corrupt. I don't see any thing potential out of him for the next 50 years of the new constitution. I would rather vote for 6. He did well in 2005-2010 in the parliament.
 
Ufisaduro hapana,serikali 2 hapana.Mwingine wa tatu hata kama ni chukua chako mapema ajaribu.
 
Hebu review na edit hii taarifa uliyoileta kwani haieleweki kundi lipi lenye ajenda serikali mbili au tatu...
 
Hivi Chenge ni mtu wa aina gani? He keeps on political arena despite the fact that he is alleged of being corrupt. I don't see any thing potential out of him for the next 50 years of the new constitution. I would rather vote for 6. He did well in 2005-2010 in the parliament.

chenge ni mwanasiasa makini, anafaa kuwa spika
 
Huhuhuhuuu! Mbona mama makinda simuoni? Ok nilikuwa nauliza tu!
 
Back
Top Bottom