Benny Haraba
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 15,670
- 14,647
Nahitaji ufafanuzi kwa wataalamu wa sheria je kazi ya bunge ni kutunga sheria ama kuzipitishaSpika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amesema ni muhimu wananchi na viongozi waelewe majukumu ya mihimili ya dola na kuheshimu mipaka yake, ili kulinda utawala wa sheria na demokrasia ya kweli.
Akizungumza leo Jumapili Juni 15, 2025 Ikulu jijini Dodoma katika hafla ya kumuapisha Jaji Mkuu mpya George Masaju, Dk Tulia amesema baadhi ya watu husherehekea maamuzi ya Mahakama kama ushindi wa bahati nasibu bila kuelewa msingi wa Katiba.
"Hata hapa juzi eh, Mahakama imetoa uamuzi ambao nimesikia watu mahali wanasherehekea kama wameshinda rotary (bahati nasibu). Nikashangaa sana nikasema hawa ni wanasheria kweli, wanaijua Katiba? Sababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatupa fursa kama Bunge kutunga sheria, inaiagiza Mahakama kutafsiri sheria. Sasa Mahakama ikishatafsiri, ni jukumu letu kama Bunge kuchukua hatua."
Kauli hiyo imekuja kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kubatilisha kifungu cha 4 cha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (Badea) ya 1994 kwa sababu kinakinzana na Katiba, na hivyo kuruhusu uwezekano wa viongozi kushtakiwa.
"Lazima wananchi wafike mahali waelewe kazi ya mihimili hii, na kumuweka Rais mahali anapostahili, kumtofautisha na Jaji Mkuu, Spika, lakini pia kuelewa Rais anavyofanya kazi kama Mkuu wa mhimili mkuu," amesema Dk Tulia.
Kuhusu sera, (policies) nafahamu hutengenezwa na wataalamu na kupitishwa na bunge
Swali je kama bunge ni kibogoyo linaweza jadili kikamilifu kuhusu sheria na sera kuhusu madhara ya hapo baadae
Do our members of Parliament in Tanzania have the knowledge to determine the aftermath of policies and laws approved