Spika Dkt. Tulia ashangazwa na wanaosherehekea uamuzi wa Mahakama viongozi kushtakiwa

Spika Dkt. Tulia ashangazwa na wanaosherehekea uamuzi wa Mahakama viongozi kushtakiwa

Sijamuelewa hapa
"Sababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatupa fursa kama Bunge kutunga sheria, inaiagiza Mahakama kutafsiri sheria. Sasa Mahakama ikishatafsiri, ni jukumu letu kama Bunge kuchukua hatua."
Yaani mahakama ikishaamua, wao mdio wachukue hatua, hatua ipi...?
 
Huyu tulia ni epitome ya uchawa hapa Tanzania kwa sasa.
Watu wanawaona kina Mwijaku ndiyo machawa waandamizi lakini Tulia ndiyo Chawa mkuu wa huu utawala.
Madaraka yanalevya na bila shaka yameshamlevya Tulia na kumpofusha kabisa.
Kwa sasa anajiwazia yeye na waliopo madarakani, hajui kesho anaweza asiwe nayo na watakaokuwa nayo watamfunga wakiamua hata kama yeye hataki
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni hasara kubwa kwa Taifa hili kuwa na Spika mpumbavu kama Tulia.
 
Ilikuwaje ukaruhusu Bunge likapitisha Sheria inayokinzana na KATIBA??..wakati u Mwanasheria Nguli kabisa..

Ingependeza kama ungeanza kwa kutuomba RADHI,..shida hiyo AKILI ya kuomba radhi huna..EGO!
Alichomaanisha Kwa sababu Bunge ndiyo linatunga Sheria, wanarudi Tena Mzigoni....!
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amesema ni muhimu wananchi na viongozi waelewe majukumu ya mihimili ya dola na kuheshimu mipaka yake, ili kulinda utawala wa sheria na demokrasia ya kweli.

Akizungumza leo Jumapili Juni 15, 2025 Ikulu jijini Dodoma katika hafla ya kumuapisha Jaji Mkuu mpya George Masaju, Dk Tulia amesema baadhi ya watu husherehekea maamuzi ya Mahakama kama ushindi wa bahati nasibu bila kuelewa msingi wa Katiba.

"Hata hapa juzi eh, Mahakama imetoa uamuzi ambao nimesikia watu mahali wanasherehekea kama wameshinda rotary (bahati nasibu). Nikashangaa sana nikasema hawa ni wanasheria kweli, wanaijua Katiba? Sababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatupa fursa kama Bunge kutunga sheria, inaiagiza Mahakama kutafsiri sheria. Sasa Mahakama ikishatafsiri, ni jukumu letu kama Bunge kuchukua hatua."

Kauli hiyo imekuja kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kubatilisha kifungu cha 4 cha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (Badea) ya 1994 kwa sababu kinakinzana na Katiba, na hivyo kuruhusu uwezekano wa viongozi kushtakiwa.

"Lazima wananchi wafike mahali waelewe kazi ya mihimili hii, na kumuweka Rais mahali anapostahili, kumtofautisha na Jaji Mkuu, Spika, lakini pia kuelewa Rais anavyofanya kazi kama Mkuu wa mhimili mkuu," amesema Dk Tulia.
Hiki kinyang'unya hakikustahili kabisa kuwa Spika.
 
Mungu atupe ujasiri lakini huyu mtu ana Ego ya namna gani? Ni haya haya madaraka au kuna kingine? Aambiwe walikuwepo kina Farao, na falme kubwa zenye nguvu nakuamua kila kitu leo hii wako wapi? Atambue yeye yupo hapo alipo kwakua kuna wengine walishapita nakuondoka hivyo uongozi ni swala la muda hawezi kua na hiyo nguvu anayodhani yupo nayo na kujiona anajua kila kitu milele.Mungu tunakukabidhi hili utashughulika naloo
Mambo ya Walawi 26:19
[19]Nami nitakivunja kiburi cha uwezo wenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa kama shaba;
Kwa Farao umeenda mbali sana.

Mwambie alikuwepo Job Ndugai ambaye alipata hata nafasi ya kufika kwa shemeji wa Yesu Kristo lakini leo ni mtu wa kawaida sana.
 
Sio mimi ni kigogo…
IMG_1566.png
 
Back
Top Bottom