Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ndugai kosa la kwanza lilikuwa kuomba msamaha kisha ukajiuzulu, inawezekana ulishinikizwa kufanya hivyo. Lakini hili la kujiuzulu huenda ni somo kwa ulimwengu juu ya mambo ya hovyo yanayo trend Tanzania, kama muhimili unaopaswa kuihoji serikali haujiamini ni nani mwingine anao huo uwezo?


Watanzania tukubali tusikubali ni kwamba Nchi sasa ipo katika sintofahamu kubwa.


Aaarghhh Ndugai bwana mbona umewaacha tena wale Covid-19 mjengoni?😣
 
Kitendo cha kuomba msamaha na kisha kujiuzuru, Naona kama vile Job amekikosea adabu cheo cha uspika. Angekomaa tu na msimamo wake.

Bunge ni muhimili unaojitegemea. Pia Kazi ya Bunge ni kutunga sheria, kukosoa na kuisimamia Serekali. Hivyo Job kuikosoa Serekali ilikuwa haki yake ya Kikatiba.
 
We subiri genuine, kimeishanuka. Address ya nini wakati hakuihitajiki reply. Na Bunge huwa ni moja tu.
 
Habari njema na Nuru mpya Kwa democrasia , uhuru wa kweli na haki katika taifa letu nauona mwanzo mpya Kwa bunge litakalo tekeleza wajibu wake ipasavyo, Sasa tuhamie Kwa wale wa NEC na wanaokwamisha kupatikana katiba mpya .
 
Alitakiwa ajiuzuru bila kuomba ule msamaha na hapo ndipo lengo la anachokiamini kingekuwa hai
Absolutely! Alikosea sana kuomba radhi, hapo nilimshangaa sana. Ila kitendo cha kujiuzulu kwangu ni kitendo cha kishujaa kabisa. Ni watanzania wangapi wakipishana mawazo na watawala wanachukua maamuzi magumu kama haya ya Ndugai na Lowasa?
 
Zama mpya za kuelekea demokrasia halisi
 
Mwendazake aliwafanya watu waka sahau uongozi wakadhani vyeo walivyo navyo ni mali yao. Mungu huwa chukia wanao tesa viumbe wake. Sasa na aseme tena kwamba ana uwezo wa kuzuia mtu asiongee hadi bunge liishe. Asante Mungu usie sinzia. Covid jiandaeni.
 
Bado naendelea kumdharau kwa kushindwa kusimamia kile alichokuwa anakiamini,hakutakiwa kuomba msamaha angekaza mwanzo mwisho halafu akiona upepo siyo ajiuzulu kama hivi.

Alichofanya hapo amewawahi ili kuepuka aibu ya kustaafishwa kwa lazima but kisiasa kwa wenye akili haja-gain chochote.
 
Hana ujumbe wowote huyo alimpinga magufuli kabla hata mwili wakke haujaoza mnafiki mkubwa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Yaani nilishangaa mno kwa vijembe vyake kwa marehemu na kuruhusu mijadala ya kumchafua marehemu. Mnafiki Sana huyu kenge wa Kigogo. Na ubunge astaafu kabisa
 
Duh watu wabaya sana, wameshililiankooni mpaka jamaa kaachia ngazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…