Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hata mimi kwa hili nampa pongezi, kwa Afrika mtu kuachia madaraka ni ngumu mno. Waafrika tunapenda sana kuwa na madaraka makubwa na kuabudiwa, ndio maana hata mtu akiwa na nafasi au elimu fulani anatamani kuitwa na nafasi hiyo.

Wenye madaraka waige hili, ukiona haupo sawa na wenzako just waache waendelee coz mawazo yenu na dira zenu ni tofauti.

Ninamlaumu tu kwa kuomba msamaha, terrible and technical mistake.
Ni kweli
 
Bunge limebaki kuwa kikaragosi.........mliosema katiba mpya haina umuhimu temeni mate chini.
 
Nakala hajampa Makinda.
Akiniudhi Siku moja mjengoni akitambulisha watu.
1.Waheshimiwa wabunge nikiboronga mjue akinifundisha Makinda.
2.Mgeni wa pili in Dada wa Bashe.
Jamani mumemuona?mweupe tens mumuangalie vizuri,Huyo ndiye alikuwa Spika wa mhimili
 
Lakini sisi Watanzania Ni Watu wagumu sana na Tusio Eleweka Nini Tunataka.

Tanzania Kuna Mihimili 3 na Hii Mihimili haingiliani Kwa Mujibu wa Katiba, NDUGAI alikuwa kiongozi wa Muhimili wenye haki kikatiba ya Kumkosoa Rais Popote Pale kama wataona Mambo Hayaendi sawa. Ndugai Alimkosoa Rais Kwenye Tozo ambazo Tumekuwa Tukilia lia Kila Siku, Na Kwenye Mikopo Ambayo Kiuhalisia Haikuwa sawa Ndani Ya Miezi 6 kutoka T 56 hadi T 70 kitu ambacho Sio Sawa Kabisa.

Kwa hiyo Tumefurahi Muhimili 1 kutikiswa na Muhimili Mwingine? Basi Hakuna Siku Bunge litakuwa na Uwezo wa Kumchallange Rais Popote pale kwa hiki kilichotokea, Tanzania Tuna Mihimili 2 Mahakama na Rais [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Shida aliomba msamaha, hiyo inafuta accountability maana hana msimamo, na hii imefuata shurutisho toka kwa akina msukuma, gwaji, kibajaji and co. So haijaja toka rohoni, kidooooogo kama angejiuzuru jana baada ya kuomba msamaha
 
Mihimili wa bunge umetikiswa na mhimili mwingine...hii si afya kwa nchi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ndugai ni dhaifu sana utajiuzulu vipi hiyo nafasi kosa lake ni lipi. Yeye ni Mtanzania ana haki ya kutoa maoni
 
Karma is the bitch. Dhambi ya kumnyanyasa Lisu haitamuacha. Hata akijiuzulu bado mabalaa yatamwandama
Kama masikhara hivi Matonya chaliiiiii! Dhambi ya usaliti haijawahi kumuacha mtu salama. Mungu hadhihakiwi.

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele (Gal 6:7-8).
 
Mhimili wa bunge haupo,tangia chini ya Nyerere mpaka leo. Labda siku ikitokea speaker anatoka chama tofauti na chama tawala.
Mi pia nawashangaa wanaodai kuwa bunge ni Muhimili huru.
Muhimili huru unadhibitiwa na chama cha siasa!?
Wanachotaka CCM ndicho kinachofanyika bungeni.
Uhuru wa muhimili huo uko vitabuni.
Samuel Sitta na bunge lake la tisa alijaribu kuonyesha uwezo, lakini ulifika muda akaishiwa pumzi.
Baadaye akachinjwa kupitia chama.

Bunge halijawahi kuwa huru, na kwa mujibu wa Katiba tuliyonayo halitakuwa huru.
 
Mihimili wa bunge umetikiswa na mhimili mwingine...hii si afya kwa nchi.
Huu ni uthibitisho na ushahidi kuwa katiba iliyopo haifa

Watu wasijiulize mhimili umetikisaje mwingine, waulize mihimili inafanyaje kazi

Ule mwingine kwani hamuoni unavyofanya madudu na matapu tapu kwa ile kesi maarufu

Ndugai alikuwa mlinzi wa katiba ya 1977 sasa ni mhanga kwasababu haikumlinda kama kiongozi wa mhimili. Aliishi kwa mazoea na ubabe, good riddance
Kaacha joho kaondoka mtupu ! bila heshima yoyote

JokaKuu
 
Back
Top Bottom