Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Januari 06, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ambayo alinukuliwa akisema ipo siku Nchi itauzwa kutokana na madeni

Amesema ameandika Barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na uamuzi huo ni binafsi na hiari, na ameuchukua kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi, Serikali na Chama

#JamiiForums

Mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai tarehe 10 Novemba 2020, alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 baada ya kupata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7. Kura moja ilimkataa. Ndugai alikuwa spika katika Bunge la 11 la 2015 - 2020.

Hapo awali akizungumza Desemba 28 katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa kwani ipo Siku Nchi itapigwa Mnada

“Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.

Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni.


RAIS SAMIA ASHANGAZWA NA SPIKA NDUGAI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alieleza kushangazwa na kauli za Spika wa Bunge Job Ndugai kusimama hadharani na kukosoa mkopo wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO -19 wakati taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake.

Akizungumza Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu, Rais Samia alionyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.

“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025. Inashangaza kuona mtu mwenye uelewa, anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa, ya nini? Au kwa nini tunaendelea kutoa tozo wakati fedha ya mkopo ipo. Mawaziri tupeni hizo takwimu sasa hivi.

"Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo. Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025", amesema Rais Samia.

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

“Naomba kutoa taarifa kwa uma wa watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza

“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge
View attachment 2070821
[emoji849][emoji2960]
 
Shinikizo la kutaka Spika ajiuzulu ktk nafasi yake limeshikiwa bango zaidi na wafuasi wa Mbowe/Chadema.

Niwazi kabisa Spika alikuwa mwiba mkali sana kwa ktk kusimamia sheria na kanuni za mbunge na haswa kwa wapinzani ambao walitaka kuleta mchezo.

Sasa leo hii hatuwezi kushangaa kuona genge la Mbowe likishangilia na kupiga mayowe eti Spika ajiuzulu.

Kamwe wana CCM Makini wasikubali kuingia ktk mtego huuu.

Inatosha na Inatosha sana kwa kitendo cha kiungwana alicho kifanya Spika cha kuomba radhi.

Kamwe tusikubali kuendelea kumdhalalisha Spika wetu aliye fanya kazi kwa umahiri mkubwa na kuisaidia nchi yetu.

Ni vyema wana CCM wakawa makini ktk kipindi hiki cha upepo mbaya, wapaswa kuwa watulivu na nidhamu ya hali ya juu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kazi iendeleee kama kawaida.

Kutuandikia barua kwa herufi kubwa ni dharau kubwa sana... Ni uhaini
Hiyo sio barua, ni tangazo kwa umma
 
20220106_174801.jpg
 
COVID-19 ni Wabunge wa Ndugai ambaye leo kaondoka tena bila heshima
Nao pia waondoke kwasababu si wabunge wa JMT bali wa Ndugai

COVID-19 Waondoke na Mteule wao

JokaKuu
 
Hapo nafikiri somo kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya ndio linaanza kueleweka sasa kwa wana CCM. Walipoambia katiba ya sasa imempa madaraka makubwa mno, kiasi kwamba ukipingana naye unakwenda na maji walikuwa hawaelewi kabisa.

Sasa ndiyo waelewe, kama "mti mbichi ndio umetemdewa hivi, Je! itakuwaje kwa mti mkavu!?". Shoka limeinuka sasa na tayari kukata kila tawi linalonekana kuwa halifai kwa kigezo cha walioushika mpini wake.

Ole wao wale wote wenye kutamani na kikinyemelea kiti kile kitukufu tuelekeapo mwaka 2025.
 
Mkuu nchi zote RAIS ana mamlaka makubwa, hakuna chini Rais akawa hana madaraka makubwa. Itakuwa haina maana ya yeye kuwa RAIS.
... uko sahihi sana Mkuu; Rais kwa vyovyote ni lazima awe the highest authority. Tatizo linakuja pale mamlaka hayo yanapopindukia ni hatari sana!
 
Back
Top Bottom